Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Benjamin l, MD
Alhamisi, 18 Novemba 2021

Asali
Asali ni kimiminika kizito chenye ladha tamu kinachozalishwa na nyuki kutoka kwenye nta ya miti na maua mbalimbali. Zaohili limejizolea umaarufu duniani kote tangu enzi na enzi na hiyo ni kutokana na umuhimu wake katika afya Mwanadamu kutokana na kuwa na virutubisho muhimu kwa biandamu.
Kuna aina mbili za asali ambazo zimegawanya kutokana na aina ya nyuki anayetengeneza, Asali ya nyuki wadogo na Asali ya nyuki wakubwa. Maelezo yaliyo katika makala hii imeelezea asali kwa ujumla.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye asali
Protini
Sukari
Kabohaidreti
Nyuzilishe
Vitamini
Madini
Maji
Mafuta
Viinilishe vinavyopatikana kwenye asali yenye gramu 100
Protini = 0.3g
Nishati = 304kcal
Sukari = 82.12g
Nyuzilishe = 0.2g
Maji = 17.10g
Mafuta = 0.1g
Madini yanavyopatikana kwenye asali yenye gramu 100
Kalishiamu = 6mg
Madini Chuma = 0.42mg
Magineziamu = 2mg
Fosifolasi = 4mg
Potashiamu = 52mg
Sodiamu = 4mg
Zinki = 0.2mg
Vitamini zinavyopatikana kwenye asali yenye gramu 100
Vitamini B2 = 0.038mg
Vitamini B3 = 0.121mg
Vitamini B5 = 0.068mg
Vitamini B6 = 0.024mg
Vitamini B9 = 2ug
Vitamini C = 0.5mg
Faida zitokanazo na asali
Husaidia katika mfumo wa mmeng`enyo wa chakula
Kulainisha koo
Kuboresha afya ya ngozi
Huongeza kinga ya mwili
Hutumika kutibu majeraha
Kuimarisha kinga ya mwili
Imeboreshwa,
18 Novemba 2021, 07:20:30
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Rachel Hajar, et al (2008). Encyclopedia of the History of Science, Technology and Medicine in Non-Western Cultures. Springer. p. 89.
Kwakman, P. H; Zaat, S. A (2012). "Antibacterial components of honey". IUBMB Life. 64 (1): 48–55.
Maddocks, et al (2013). "Honey: a sweet solution to the growing problem of antimicrobial resistance?". Future Microbiology. 8 (11): 1419–1429.
Molan, P; Rhodes, T (June 2015). "Honey: A Biologic Wound Dressing". Wounds. 27 (6): 141–51.
Boukraâ, et al (2014). Honey in Traditional and Modern Medicine. CRC Press. p. 126. ISBN 9781439840160.