top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, CO

Dkt. Sospeter B, MD

Jumamosi, 4 Desemba 2021

Bibo
Bibo

Bibo ni tunda linatokana na mti aina ya mbibo, matunda haya huwa yanakua na rangi nyekundu au rangi ya njano na sifa yake kuu ni Tunda lenye mbegu kwa nje. Nchini Tanzania Matunda haya hulimwa kwa wingi kutoka mikoa ya kusini na yanapatikana Tanzania nzima. Bibo ni maarufu kwa ladha yake, utamu wake pia mbegu (karanga) imekua ikitumika kwa matumizi mbalimbali.Tunaeza kutumia Bibo kutengenezea juisi, Mvinyo na hata kulitafuna lenyewe.Kama yaliyvyo matunda mengine, Bibo pia lina viritubisho na viinilishe vya kutosheleza kile kinachotakiwa ndani ya mwili wa Binadamu.


Viinilishe vinavyopatikanakwenye Bibo


 • Protini

 • Mafuta

 • Maji

 • Nyuzilishe

 • Sukari

 • Madini

 • Kabohaidreti


Viinilishe vinavyopatikanakwenye Bibo lenye gramu 100


 • Nishati = 391kcal

 • Mafuta = 17g

 • Kabohaidreti = 59g

 • Nyuzilishe = 6.5g

 • Sukari = 43g

 • Maji


Madini yanayopatikana kwenye Bibo lenye gramu 100


 • Kalishiamu =43mg

 • Madini Chuma = 3.1mg

 • Potashiamu = 696mg

 • Sodiamu = 185mg


Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Bibo


 • Kuimarisha afya ya Ubongo

 • Kuimarisha afya ya Moyo

 • Kuimarisha kinga ya mwili

 • Kuimarisha afya ya ngozi

 • Kuimarisha mfumo wa mmeng`enyo wa chakula

 • Kuimarisha afya ya mfupa

 • Kuimarisha afya ya kinywa

Imeboreshwa,
4 Desemba 2021 15:06:14
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Vasconcelos MS, et al. Anti-inflammatory and wound healing potential of cashew apple juice (Anacardium occidentale L.) in mice. Exp Biol Med.

 2. Patil PJ. Indian cashew food. Integr Food Nutr Metab. 2017;4(2):1–5.

 3. Hu FB, Manson JE, Willett WC. Types of dietary fat and risk of coronary heart disease: a critical review. J Am Coll Nutr. 2001;20:5–19.

 4. Barros EM, et al. A yeast isolated from cashew apple juice and its ability to produce first- and second-generation ethanol. Appl Biochem Biotechnol. 2014;174:2762–2776.

 5. https://uc.xyz/14LBMi?pub=link [Effects of Mulberry Fruit ( Morus alba L.) Consumption on Health Outcomes: A Mini-Review - PubMed] Imepitiwa tarehe 2/12/2021

bottom of page