Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, MD
Dkt. Benjamin L, MD
Jumatatu, 21 Machi 2022
Dungusi kakati (tunda)
Ni matunda yanayoliwa yatokanayo na mmea wa maua uitwao Peary kutoka kundi Opuntia katika familia ya Cactus.
Matunda haya ni maarufu kwa sababu ya umbo lake la nje lenye miiba pia kutokana na utamu uliosheheni vitamini na virutubisho muhimu kwa mwanadamu bila kusahau harufu yake nzuri.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Matunda ya Peari
Mafuta
Madini
Nyuzilishe
Protini
Vitamini
Kabohaidreti
Maji
Kemikali muhimu zinazopatikana kwenye Matunda ya Peari
Kwenye matunda ya peari kuna kemikali muhimu ambazo ni Vanillic Acid,Catechins na Gallic Acid
Viinilishe vinavyopatikana kwenye Matunda ya Peari yenye gramu 100
Nishati = 41kcal
Mafuta = 0.1g
Maji = 87.6g
Kabohaidreti = 9.6g
Nyuzilishe = 3.6g
Protini = 0.7g
Vitamini zinazopatikana kwenye Matunda ya dungusi kakati yenye gramu 100
Vitamini A = 2mcg
Vitamini B1 = 0.041mg
Vitamini B2 = 0.06mg
Vitamini B3 = 0.460mg
Viatmini B6 = 0.6mg
Vitamini B9 = 6mcg
Vitamini C = 14mg
Vitamini E =0.7mg
Vitamini K = 2.7mg
Madini yanayopatikana kwenye Matunda ya dungusi kakati yenye gramu 100
Kalishiamu = 56mg
Kopa = 0.08mg
Madini Chuma = 0.3mg
Magineziamu = 85mg
Fosifolasi = 24mg
Potashiamu = 220mg
Sodiamu = 5mg
Zinki = 0.12mg
Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Matunda ya dungusi kakati
Husaidia kuimarisha afya /utendaji kazi wa Moyo pamoja na kuzuia magonjwa mbalimbali yashambuliayo Moyo.
Husawazisha shinikizo la damu ikiwemo pia kuzuia shinikizo la juu la damu.
Hupunguza na kuweka msawazo wa uzito mwilini.
Husawazisha kiwango cha sukari mwilini na kupunguza athari za kupatwa na ugonjwa wa kisukari.
Husaidia kupunguza athari za kupatwa na ugonjwa wa kansa za aina mbalimbali.
Imeboreshwa,
24 Machi 2022 07:11:14
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Prickly_pears. https://www.nutritionvalue.org/Prickly_pears%2C_raw_nutritional_value.html?size=100+g.. Imechukuliwa tarehe 1 February 2022.
Silva MA, Albuquerque TG, Pereira P, Ramalho R, Vicente F, Oliveira MBPP, Costa HS. Opuntia ficus-indica (L.) Mill.: A Multi-Benefit Potential to Be Exploited. Molecules. 2021 Feb 11;26(4):951. doi: 10.3390/molecules26040951. PMID: 33670110; PMCID: PMC7916838. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/33670110/. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.
Onakpoya IJ, O'Sullivan J, Heneghan CJ. The effect of cactus pear (Opuntia ficus-indica) on body weight and cardiovascular risk factors: a systematic review and meta-analysis of randomized clinical trials. Nutrition. 2015 May;31(5):640-6. doi: 10.1016/j.nut.2014.11.015. Epub 2014 Dec 19. PMID: 25837206. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/25837206/. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.
Effects of the Consumption of Prickly Pear Cacti (Opuntia spp.) and its Products on Blood Glucose Levels and Insulin: A Systematic Review. Written by Caroline A. Gouws, Ekavi N. Georgousopoulou et al. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6572313/. Imechukuliwa tarehe 4 February 2022.