Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Charles W, MD
Ijumaa, 22 Oktoba 2021
Embe
Embe ni matunda yatokanayo na miti ya miembe inayopatikana kwenye familia ya mangifera.
Kikombe kimoja cha juisi ya embe huwa na mguvu ya kilo karoli 100, hivyo huwa ni kinywaji kinachotoa nishati ya kutosha kwenye mwili.
Embe huwa na vitamin aina mbalimbali zifikazo 20 zikiwepo vitamin A,B6 na C kwa wingi, pia huwa na madini ya folic acid. Kwa namna hii hufanya embe kuwa tunda zuri sana
Madini ya shaba pia hupatikana katika embe ambayo husaidia katika kinga za mwili, mifupa na chembe nyekundu za damu
Viinirishe vinavyopatikana kwenye Embe
Mafuta
Kabohaidreti
Nyuzilishe
Protini
Sukari
Madini
Vitamini
Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Embe
Tunda la Embe lina kemikali muhimu ambazo ni Gallic Acid na Ellagic Acid
Viinirishe vinavyopatikana kwenye tunda la Embe
Nishati= 60kcl
Jumla ya mafuta = 0.4g
Sodiamu= 1mg
Kabohaidreti = 15g
Sukari = 14g
Nyuzilishe = 1.6g
Protini = 0.8g
Maji = 83.46g
Kalishiamu= 11mg
Potashiamu = 168mg
Madini chuma = 0.2mg
Madini yanayopatikana kwenye Tunda la Embe lenye Gramu 100
Madini chuma = 0.2mg
Kalishiamu = 11mg
Magineziamu =10mg
Kopa = 0.11mg
Fosifolasi = 14mg
Potashiamu = 168mg
Sodiamu = 1mg
Floraidi = 3.3mg
Vitamini zinazopatikana kwenye Tunda la Embe lenye gramu 100
Vitamin A = 54mcg
Vitamini B1 = 0.028mg
Vitamini B2 = 0.038mg
Vitamini B3 = 0.669mg
Vitamini B5 = 0.197mg
Vitamini B6 =0.119mg
Vitamini B9 = 43mcg
Vitamini C = 36.4mg
Vitamini E = 090mg
Vitamini K = 4.2mcg
Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa tunda la Embe
Kuimarisha na kuongeza kinga ya mwili
Kupunguza kasi ya kupatwa na ugonjwa wa kansa.
Kulainisha choo
Kusaidia kuongeza uharaka wa damu kuganda pindi itokapo nje ya mishipa
Kuimarisha afya ya kongosho pamoja kuzuia kupatwa na ugonjwa wa kisukari
Imeboreshwa,
22 Januari 2022 17:33:50
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Lauricella, Marianna et al. “Multifaceted Health Benefits of Mangifera indica L. (Mango): The Inestimable Value of Orchards Recently Planted in Sicilian Rural Areas.” Nutrients vol. 9,5 525. 20 May. 2017, doi:10.3390/nu9050525
Mango, nutritional value. https://www.nutritionvalue.org/Mangos%2C_raw_nutritional_value.html?size=100+g&utm_source=share-by-url. Imechukuliwa tarehe 1 December 2021
Shahidi F, Wanasundara PK. Phenolic antioxidants. Crit Rev Food Sci Nutr. 1992;32(1):67-103. doi: 10.1080/10408399209527581. PMID: 1290586.
Farina V., Corona O., Mineo V., D’Asaro A., Barone F. Qualitative characteristics of Mango fruits (Mangifera indica L.), which have undergone preservation (Italian) Acta Italus Hortus. 2013;12:70–73.