Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Charles W, MD
Alhamisi, 9 Aprili 2020

Faida za kiafya za Glukosi
Ni sukari inayotumika na seli nyingi katika mwili. Sukari hii huzipa organi mbalimbali nguvu na uwezo wa kufanya kazi. Pasipo sukari ogani za mwili hushindwa kufanya kazi na mwili kuishiwa nguvu, wakati mwingine sukari ikishuka chini ya kiwango kinachotakiwa mtu huzimia na kupoteza fahamu.
Glukosi ni sukari katika wanga kwenye kundi la sukari jamii ya monosakaraidi
Aina zingine za Monosakaraidi
Fruktozi
Galaktozi
Ribozi
Vyakula vyenye glukosiGlukosi
Vyakula vya wanga kama mchele,mikate,ngano,viazi ,mihogo
Vyakula vya protini kama Nyama,samaki
Vyakula vya mafuta kama siagi na parachichi
Jinsi gani mwili huweza kuthibiti kiwango cha glukosi?
Pale unapokula chakula chenye Glukosi na kuingia mwilini , vimeng'enya mbalimbali vya hubadili chakula cha wanga na kuwa sukari ya glukosi. Glukosi hufyonzwa kwenye utumbo mwembamba na kuingia kwenye damu kwa ajili ya kwenda kwenye seli mbalimbali za mwili au ini kwa ajili ya kuhifadhiwa.
Kiwango cha glukosi kinapopanda kwenye damu mara baada ya kula, tezi ya kongosho hutoa homoni ya Insulin ambayo hutumika kuthibiti kiwango cha glukosi kwenye damu. Kiwango cha glukosi kikiwa juu kuliko mahitaji Ini kwa msaada wa homoni ya glukosi huhifadhi sukari hiyo kwenye mfumo wa glycogen na kuitunza kwa matumizi ya baadae.
Kiwango cha glukosi kikiwa kidogo kwenye damu, tezi za kongosho hutoa homoni ijulikanayo kama glucagon inayofanya kazi ya kubadili glykojeni iliyotuzwa kwenye Ini kuwa glukosi ili iweze tumika na seli mbalimbali mwilini.
Hivyo kiwango cha glukosi kwenye damu huendelea kuwa cha kawaida kulingana na viwango vinavyokubalika kitiba.
Dalili za mtu mwenye glukosi nyingi kwenye damu ni:
Kupata kiu ya maji mara kwa mara
Maumivu ya kichwa
Kuona ukungu
Kukojoa mara kwa mara
Mwili kuchoka na kuwa dhaifu
Kupungua uzito
Dalili za mtu mwenye upungufu wa glukosi
Njaa
Kutetemeka
Kuwa na woga na wasiwasi
Kuchoka
Kutokwa na jasho sana na ghafla
Ngozi kuwa nyeupe
Kupata usingizi
Kizunguzungu
Glukosi ikiwa chini kabisa huweza kuzimia ama kukosa fahamu na kutokuona vizuri
Vipimo
Ili kuweza kujua wingi wa sukari, damu huchukuliwa kwenye kidole na kupimwa na kifaa kinachoitwa glukometa
Kiwango cha sukari cha kawaida ni kipi?
Kwa mtu aliyefunga kiwango kinatakiwa kuwa chini ya 5.6mmol/dl ( mfungo wa masaa nane)
Kwa mtu amabaye amekula chakula saa moja kabla ya kupima kiwango cha glukosi kinatakiwa kuwa chini ya 11.1mmol/dl
Matibabu
Mgonjwa mwenye Diabetes Mellitus 1 kisukari cha kuzaliwa nacho au cha utotoni hutumia homoni ya insulin kwenye matibabu yake. Soma Zaidi kuhusu kisukari aina ya 1 katika tivuti hii
Mgonjwa mwenye kisukari aina ya pili hutumia dawa za vidonge kupunguza kiwango cha sukari kwenye damu mfano; Metformin, glipizide, glyburide, gliclazide, glimepiride, acarbose, miglitol na voglibose. Soma Zaidi kwenye Makala ya kisukari aina ya 2 kwenye tovuti hii.
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021, 11:07:00
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
NCBIOralHypoglycaemichttps://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK482386/ 8/4/2020
WebMdHypoglycaemiahttps://www.webmd.com/diabetes/hypoglycemia-overview Imechukuliwa 8/4/2020
HealthLineHypoglycaemiahttps://www.healthline.com/health/hypoglycemia Imechukuliwa 8/4/2020
WebMdHyperglcaemiahttps://www.webmd.com/diabetes/guide/diabetes-hyperglycemia Imechukuliwa 8/4/2020
.MedicalNewTodayHyperglycaemiahttps://www.medicalnewstoday.com/articles/313138 Imechukuliwa 8/4/2020
Mayo clinic. Diabetes. https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/diabetes/diagnosis-treatment/drc-20371451. Imechukuliwa 8/4/2020