Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Sospeter B, MD
Dkt. Charles W, MD
Alhamisi, 2 Aprili 2020
Faida za kiafya za Parachichi
Parachichi ni tunda linalotokana na mti wa mparachichi, huwa na rangi ya kijani kwa nje na wakati mwingine nyeusi na zambarau kutokana na kila aina.
Ladha ya parachichi huwa kama siagi na Mafuta, na huwa lina wingi wa mafuta na fiber (nyuzi nyuzi)
Tunda hili halifai kupikwa bali hutumika kama tunda la kuweka baada ya kuandaa Kachumbari au unaweza kula lenyewe tu.
Viini vya parachichi
Potassium
Kalisiamu
Fosforasi
Maginiziamu
Vitamin A
Vitamin C
Vitamin E
Foleti
Vitamin K
Vitamin B
Protini
Mafuta
Wanga
Faida zingine za parachichi
Lina mafuta kwa wingi yasiyo na chumvi kwa wingi wala kolestro ambayo ni hatari kwa afya inapozidi kwa hiyo huepusha magonjwa ya moyo
Ni chanzo kizuri cha nyuzilishe ambazo husaidia kukipa uzito kinyesi na kufanya kitole kirahisi
Lina aina ya kirutubisho kiitwacho lutein ambayo ni aina ya vitamin iitwayo karotini
Huongeza nguvu kwa wingi zaidi kuliko kazi zingine
Huongeza maji mwilini
Huongeza wanga kwenye mwili
Huongeza protini mwilini
Huongeza madini ya Potasiamu kwa wingi kupita hadi ndizi
Parachichi ni tunda ambalo ni rafiki wa kupunguza uzito ,hii ni kutokana na tafiti zilizofanywa kwamba watu wanaokula wana uwezo wa kukaa kama masaa 5 wakiwa wametosheka kwa kushiba bila kuona njaa tofauti na wale ambao hawajala
Ni rahisi kutumika na linafaa kuliwa na vyakula vingi pamoja ,kama Kachumbari ,Wali ,makande , maharage na mboga za majani
Parachichi husaidia kutibu na kuzuia saratani. Tafiti zinaonyesha kuwa parachichi lina kemikali ya avocatin B ambayo husaidia kuua chembe zasaratani ya damu
Parachichi husaidia afya ya akili na kukumbuka
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:17:30
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
12provenhealthbenefitshttps://www.healthline.com/nutrition/12-proven-benefits-of-avocado 31/3/2020
Everyday health. What Are the Health Benefits of Avocado, and Can It Help You Lose Weight?. Https://www.everydayhealth.com/diet-nutrition/diet/avocados-health-benefits-nutrition-facts-weight-loss-info-more/ 31/3/2020
Encyclopedia of foods a guide for health nutrition ISBN 978-0-12-219803-8 ukurasa wa 157
ULY clinic maswali na majibu