top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Sospeter B, MD

Dkt. Mangwella S, MD

Ijumaa, 10 Aprili 2020

Faida za kiafya za Samaki
Faida za kiafya za Samaki

Samaki ni moja ya chakula chenye protini na virutubisho kwa wingi vyenye umuhimu mwilini. Protini huweza kutoa nguvu na kuimarisha misuli kwa ajili ya kufanya kazi.


Protini na virutubisho vilivyo kwenye samaki huimarisha afya ya Ini, ubongo na uwezo wako wa kulala. Unashauriwa kula samaki kwenye mlo wako ili uweze kupata faida hizi.


Mafuta yaliyopo kwenye samaki hayasababishi magonjwa ya moyo kama yalivyo mafuta ya viumbe wengine. Baadhi ya samaki huwa na Mafuta ya omega 3 kwa wingi, tafiti zinaonyesha Mafuta haya humkinga mtu dhidi ya magonjwa ya moyo. Mafuta haya pia hupunguza kolestro aina ya LDL kwenye damu


Virutubisho vya samaki


 • Vitamin B

 • Chuma

 • Potasiamu

 • Magneziamu

 • Fosforazi

 • Iodine kwa samaki wa baharini

 • Calcium


Samaki gani mzuri ununue?


Samaki mbichi


Huyu ni samaki ambaye bado hajakatwa na anaonekana na umbo la samaki (si nyama ya samaki) na kawaida yake utaenda kumuandaa nyumbani. Samaki huyu huwa ametolewa kwenye maji muda sio mrefu ,mabaka yake ya Ngozi huwa hayajakwanguliwa na nyama yake haivutiki kirahisi na huwa na shombo. SAmaki huyu huwa mzuri sana kwani huwa bado hajaharibika.


Steki ya nyama ya samaki


Samaki hawa huwa hawana harufu ya shombo ,epuka kununua samaki ambaye nyama yake inavutika na rangi yake imepotea.


Samaki aliyewekwa kwenye jokofu


Epuka kununua samaki mkavu, kwani anaweza kuwa amekaa muda mrefu na ameharibika. Nunua samaki akiwa ameyeyuka kutoka kwenye barafu, mwangalie pia kama ni mzima kutokana na maelezo yah apo juu.


Samaki aliyefukizwa


Samaki aliyefukizwa katika moshi au ametuzwa na chumvi au samaki ambaye hana harufu ya samaki


Faida za samaki


Hupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo-Samaki huwa na Mafuta ya omega-3 fati asidi ambayo husaidia hatari ya kupata magonjwa ya moyo.


Hupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa Alzheimer’ ambayo huharibu uwezo kumbukumbu. Samaki haswa wa baharini hupunguza kusinyaa kwa ubongo kunakoambatana na kuongezeka kwa umri.


Husaidia kupunguza dalili za sonona- Tafiti zinaonyesha mtu mwenye huzuni endapo akatumia dawa zake vizuri pamoja na samaki huweza kumsaidia, pia wapo samaki ambao husaidia kuondoa tatizo hili endapo wakiliwa.


Ni chanzo kikuu cha Vitamin D:- Mifupa ya samaki huwa na vitamin D kwa wingi na huimarisha mifupa.


Husaidia uimara wa macho na afya ya macho kuwa imara-hii ni kutokana na Mafuta ya omega 3 fati asidi.


Huweza kusaidia kulala vizuri- Watumiaji wa samaki wengi huwa na uwezo wa kulala kupata usingizi bila shida.


Husaidia kuondoa chunusi - Matumizi ya samaki husaidia kusafisha ngozi na kuondoa chunusi

Husaidia kupunguza dalili za athraitizi ya Rheumatoid(baridi yabisi)- Matumizi ya samaki husaidia kupunguza uvimbe na maumivu ndani ya maungio ya mwili.


Ni chanzo kizuri cha protini isiyokuwa na mafuta mengi ambayo ni hatari kwa mwili.


Husaidia kupunguza kolestro aina ya LDL mwilini- Kolestro aina ya LDL huongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.


Husaidia kupunguza shida magonjwa ya moyo, kuferi kwa moyona kiharusi:- UWezo huu ni kutokana na kuwa na uwezo wake wa kupunguza mafuta, kupunguza madhara ya sumu ya oksijeni kwa kupunguza kiasi cha kolestro aina ya LDL.Hupunguza hatari ya kupata magonjwa yanayoshusha kinga ya mwili:- Kutokana na kuwa na vitamin D kwa wingi, vitamin D husaidia kuongeza kinga ya mwili.


Faida zingine

 • Hupunguza hatari ya kupata saratani ya kinywa ,utumbo na koo

 • Hupunguza hatari ya kupata shinikizo la juu la damu

 • Hupunguza dalili Koma hedhi

 • Husaidia kutibu magonjwa ya Ini

 • Huchochea afya ya ubongo na kumbukumbu

 • Husaidia kupunguza hatari ugonjwa wa pumu kwa watoto wadogo

Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:17:08
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Eat this not that.Advantage of fish for health. https://www.eatthis.com/health-benefits-of-fish/ Imechukuliwa 10/4/2020

 2. Health line. Advantage of fish. https://www.healthline.com/nutrition/11-health-benefits-of-fish .Imechukuliwa 10/4/2020

 3. Ecowatch.Benefits of eating fish. https://www.ecowatch.com/amp/11-amazing-health-benefits-of-eating-fish-1882045590 Imechukuliwa 10/4/2020

 4. Encyclopedia of foods a guide for health nutrition ISBN 978-0-12-219803-8 ukurasa wa 313-316

bottom of page