top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

Ijumaa, 10 Aprili 2020

Faida za kiafya za Uyoga
Faida za kiafya za Uyoga

Uyoga ni jamii ya fangasi ambao wanaokuwa kwenye udongo. Uyoga unaozungumziwa hapa ni ule ambao unaliwa kama chakula.


Kuna aina Zaidi ya 2000 za uyoga zinazofahamika duniani. Uyoga unaoliwa hujulikana kwa jina la Agaricus bisporus. Baadhi ya uyoga huwa na sumu, hivyo ni vema kuwa makini unapochagua uyoga.


Virutubisho vya uyoga


 • Madini ya seleniamu, kolini na shaba

 • vitamin C, B, Riboflavin, Niacin, B5

 • Madini ya Ergothioneine

 • Potasiamu

 • Wanga na

 • Beta-glucans


Faida za uyoga


Huweza na antioksidanti:- ambavyo hupambana na kemikali na sumu ya oksijeni inayozalishwa kama mazao ya umetaboli. Kuzidi kwa sumu ya osijeni mwilini hupelekea maradhi mbalimbali sugu. Mfano wa antioksidant ni selenium na choline. Madini ya selenium husaidia kuongeza kinga mwilini.


Husaidia kupunguza hatari ya kupata saratani:- mfano saratani ya mapafu, tezi dume(tezi ya prosteti) na saratani ya matiti- hii ni kutokana na uwepo wa antioksidanti mbalimbali kwenye uyoga Vitamin D kwenye uyoga humkinga mtu na hatari ya kupata saratani.


Hupunguza hatari ya kupata kisukari:- Na kwa walio nacho husaidia kushusha kiwango cha sukari kwenye damu. Hutumika sana kwa wagonjwa wa kisukari kutokana na kuwa na chakula chenye nyuzinyuzi nyingi,


Huupa moyo afya nzuri:- Kutokana na uwepo wa Vitamin C na madini ya potasiamu.


Husaidia afya nzuri kwa mama mjamzito:- Kutokana na kuwa na vitamin folate ambayo ni muhimu katika utengenezaji wa mfumo wa fahamu wa mtoto na kuwezesha kazi mbalimbali za kimetaboli.


Una vitamin nyingi:- Uyoga una wingi wa Vitamin B ambayo ni Riboflavin, B2, Folate, B9, Thiamine, B1, B5 na Niacin


Husaidia umeng’enyaji wa chakula:- Husaidia umeng'enyaji wa chakula kwenda vizuri kutokana na kuwa na nyuzinyuzi kwa wingi.


Hufanya mifupa kuwa imara:- Kwa kuwa uyoga una Vitamin D, husaidia mifupa kuwa imara na yenye nguvu.

Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:16:50
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Encyclopedia of foods a guide for health nutrition ISBN 978-0-12-219803-8 ukurasa wa 245

 2. Mushroom nutrition. https://www.mushroomcouncil.com/nutrition-benefits/. Imechukuliwa 10.04.2020

 3. Medical News Today .Mushroom. https://www.medicalnewstoday.com/articles/278858 Imechukuliwa 10/4/2020

 4. Good House Keeping. Mushroom. https://www.goodhousekeeping.com/health/diet-nutrition/a27633487/mushroom-health-benefits/ Imechukuliwa 10/4/2020

 5. Organic.Facts.Mushroom.https://www.organicfacts.net/health-benefits/vegetable/health-benefits-of-mushroom.html Imechukuliwa 10/4/2020

bottom of page