Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Sima A, CO
Dkt. Adolf S, MD
Jumanne, 5 Mei 2020
Faida za Mboga za majani
Ili uwe na afya njema ni lazima kutumia mbogaza majani. Mboga za majani hubeba kwa wingi vitamin, madini na nyuzinyuzi zinazosaidia mfumo wa chakula kumeng’enya chakula. Faida za mboga za majani hutegemea aina ya mboga ya majani.
Aina mbalimbali za mboga za majani na faida zake
Spinach
Mboga hii ya majani huwa na wingi wa madini chuma, kalisiamu, magnesium na Folate Pamoja na antioksidanti, Vitamin K, A na Vitamin C, madini na vitamin zilizo kwenye mboga hii humpa mtu uwezo wa kuona vizuri, kuimarisha mifupa na kusaidia damu kuganda mapema unapoumia
Kale
Ni mboga ya majani jamii ya kabeji, mboga hii hutoa nishati,vitamin A na C pamoja na K , husaidia kupunguza mafuta kwa wingi na uzito ikitumiwa kama juisi pia hupunguza shinikizo la juu la damu.
Broccoli
Ni mboga ya majani jamii ya mboga kabeji, Mboga hii huwa na nishati kwa wingi, Vitamin C na K, kula kwa wingi mboga hii huweza kupelekea kupunguza hatari ya magonjwa ya saratani ,Mboga hii hupunguza hatari ya kupata saratani ya matiti.
Kunde
Ni moja ya mboga za majani kwa majani yake na mbegu yake ikiwa bado mbichi ,huwa na wingi wa nishati, nyuzinyuzi ,protini , Vitamini A, B,C ,E na K.
Mboga hii huwa na faida zifuatazo;
Huwa na mafuta kidogo ambayo husaidia kuthibiti uzito kupita kiasi.
Huwa na nyuzi nyuzi na virutubisho vidogo vidogo vinavyosaidia umeng’enyaji wa chakula tumboni na kufanya chakula kisikae muda mrefu tumboni.
Huwa na wingi wa protini ambayo husaidia kuponya mwili n majeraha na utengenezaji wa homoni
Husaidia kuongeza kinga za mwili kutokana na kuwa na antioxidant nyingi kama flavonoids, carotenoid na polyphenols
Husaidia kuondoa mikunyazi kwenye ngozi kutokana na kuwa na Vitamin E kwa wingi
Husaidia kuthibiti sukari mwilini kutokana na kuwa na protini kwa wingi na nyuzi nyuzi ambazo huthibiti umeng’enyaji wa chakula cha sukari
Kuwa na wingi wa Vitamin B1, B2 na folate husaidia kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:11:41
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
MedicalNewToday.HealthiestVegetables.https://www.medicalnewstoday.com/articles/323319. Imechukuliwa 16/4/2020
HealthyEating.VegetablesFood.https://www.healthyeating.org/healthy-eating/all-star-foods/vegetables. Imechukuliwa 16/4/2020
OrganicFacts.Vegetables.https://www.organicfacts.net/health-benefits/vegetable. Imechukuliwa 16/4/2020
Encyclopedia of foods a guide for health nutrition ISBN 978-0-12-219803-8 ukurasa wa 211