top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Peter A, MD

Ijumaa, 22 Oktoba 2021

Jira
Jira

Jira ni mbegu inayotoka katika mmea wa kingdom plantae na Genus-Cuminum), unga wake unatumika kama kiungo cha kupikia hasa pilau na huleta radha na harufu nzuri, lakini kiungo hiki kina kazi nyingi katika mwili.


Bala la ulaya, Afrika ya kaskazini na Amerika ya kusini ni sehemu pekee inayotumia sana kiungo hiki kwa shighuli mbalimbali. Kwa zaidi ya miaka 5000 katika nchi ya Misri wanatumia Jira kama kiungo na moja ya dawa inayosaidia(mchanganyiko na vitu vingine) kukaushia miili ya watu waliokufa au kwa lugha ya kiingereza mummification.

Faida za jira mwilini


Zifuatazo ni kazi za Jira kwa ajiri ya matibabu ya mwili.

  • Jira inasaidia katika mfumo wa umeng’enyaji wa chakula, inasaidia uzalishaji wa vimeng’enya vya kongosho hivyo uzalishaji wa vimengenya husaidia katika umeng’enyaji wa chakula.

  • Katika mfumo wa fahamu, Jira inasaidia kuongeza kumbukumbu na kupunguza msongo wa mawazo.

  • Inapunguza sumu katika mwili.

  • Jira pia inasaidia watu wenye kisukari ch ukubwani-kisukari aina ya 2, husaidia homoni insulin kutumika vizuri katika mwili yaani huongeza usafirishaji wa sukari katika kwenda ndani ya seli kwa ajili ya matumizi.

  • Inasaidia kwa watu wenye pumu kwa kutanua mirija ya hewa

  • Inasaidia kuongeza kinga ya mwili.

  • Pia kwa wanawake waliofika kipindi cha koma hedhi, jira inasaidia kuimalisha mifupa yao kipindi hiki.

Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:03:21
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. Johri, R K. “Cuminum cyminum and Carum carvi: An update.” Pharmacognosy reviews vol. 5,9 (2011): 63-72. doi:10.4103/0973-7847.79101

bottom of page