Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Sospeter M, MD
Alhamisi, 18 Novemba 2021
Kabeji
Kabeji ni mmea kwenye kundi la mbogamboga wenye sifa ya kuwa na kiasi kikubwa cha vitamin C na K
Aina za kabeji
Kuna aina kadhaa za kabeji na hiyo ni kutokana na rangi zake ambazo ni nyeupe, kijani na nyekundu. katika mkala hii tutazungumzia kabeji ya kijani/nyeupe, aina hii ya kabeji imekua maarufu kutokana na urahisi wa kupatikana maeneo mabalimbali ya mshamba pamoja masoko.
Zao hili limethibitishwa na mashirika mengi ya vyakula kuwa linafaa kwa matumizi ya binadamu na ni salama kwa afya. Kabeji inaweza tumiwa kwa namna mbalimbali mfano kama mboga, kiungo kwenye chakula, pia ianeza kutumika ikiwa mbichi, kupikwa/kuchemshwa bila kusahau kuchanagnywa na mbogamboga nyingine (kachumbari).
Viinilishe vinavyopatikana kwenye kabeji
Mafuta
Protini
Kabohaidreti
Madini
Vitamini
Madini
Maji
Nyuzilishe
Sukari
Viinilishe vinavyopatikana kwenye kabeji yenye gramu 100
Nishati = 25kcal
Protini = 1.3g
Mafuta = 0.1g
Kabohaidreti = 6g
Nyuzilishe = 2.5g
Sukari = 3.2g
Maji = 90g
Madini yanayopatikana kwenye kabeji yenye gramu 100
Potashiamu = 170mg
Sodiamu = 18mg
Madini chuma = 36mg
Magineziamu = 11mg
Manganizi = 1.5mg
Fosifolasi = 25mg
Vitamini zinazopatikana kwenye kabeji yenye gramu 100
Vitamini A = 5mcg
Karotini Alifa = 30mg
Karotini Beta = 38mg
Vitamini B1 = 1mg
Vitamini B2 = 1mg
Vitamini B3 = 1mg
Vitamini B5 = 1mg
Vitamini B6 = 1mg
Vitamini B9 = 40mcg
Vitamini C = 35mg
Vitamini E = 1mg
Vitamini K = 60mg
Faida za kiafya zitokananazo na utumiaji wa kabeji
Huongeza kinga ya mwili
Husaidia mjongeo wa viungo
Huimarifa afya ya ngozi na mifupa pamoja na mifupa
Hupunguza hatari ya kupatwa na kansa kwa asilimia 7%
Husaidia mmemng`enyo wa chakula
Hupunguza na kurekebisha shinikioz la juu la damu
Husaidia damu kuganda haraka kwa damu pale mtu apatapo jeraha
Hupunguza mafuta yasiyohitajika mwilini
Imeboreshwa,
18 Novemba 2021 10:13:44
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Decoteau, et al (2000). Vegetable crops. Prentice hall. P. 174. Isbn 978-0-13-956996-8.
Tse, get al. (2014). "cruciferous vegetables and risk of colorectal neoplasms: a systematic review and meta-analysis". Nutrition and cancer. 66 (1): 128–139.
Encyclopedia of cultivated plants: from acacia to zinnia. Abc-clio. 2013. P. 169. Isbn 978-1-59884-775-8.
Dalby, andrew (2013). Food in the ancient world from a to z. Routledge. P. 67. Isbn 978-1-135-95422-2.