Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Charles W, MD
Ijumaa, 22 Oktoba 2021
Kitunguu swaumu
Umuhimu wa kitunguu swaumu
Kimeundwa na kiundwa kiitwacho allicine ambacho kinaumuhimu kwenye mambo ya tiba
Huwa na viinirishi ,virutubishi na madini tofauti yenye umuhimu mkubwa mwilini kama vile
Madini ya manganese
Vitamin B6
Vitamin C
Selenium
Na nyuzu nyuzi
Pia huwa na calcium, shaba, potassium, phosphorus, madini chuma na vitamin B1 kwa kiasi kidogo.
Faida za kiafya
Faida za kiafya za kitunguu swaumu ni;
Huweza kuponya homa ya mafua kwa kuamsha kinga ya mwili
Hushusha shinikizo la damu la juu
Hupunguza kiasi cha rehamu mbaya kwenye damu na hivyo kuchangia kupunguza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.
Huwa na antoxidant inayolinda kuharibiwa/kuunguzwa kwa chembe chembe hai za mwili
Huongeza umri wa kuishi- kwa sababu huwa na uwezo wa kupambana na magonjwa basi mtu anaweza kuishi maisha marefu kutokana na kutopta tatizo la kuumwa mara kwa mara. Utafiti bado haujaonyesha ni kwa namna gani maisha huongezeka lakini sababu inaweza kuwa uwezo wake wa kupambana na magonjwa.
Huondoa sumu mwilini kama sumu ya lead kwenye damu
Huimarisha afya ya mifupa.
Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 10:55:11
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii