Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Peter R, CO
Dkt. Benjamin L, MD
Jumamosi, 4 Desemba 2021
Lozi
Lozi ni karanga inayotoka kwenye matunda ya mti wa Mlozi wenye asili ya Irani lakini kwa sasa umesambaa sehemu mbalimbali duniani. Karanga ya lozi imekua inapendekezwa kutumika kwa binadamu kwa kuwa huwa na virutubisho na vitamin kwa kujenga na kuboresha afya.
Viinilishe vinavyopatikana kwenye lozi
Protini
Kabohaidreti
Nyuzilishe
Sukari
Vitamini
Madini
Mafuta
Viinilishe vinavyopatikana kwenye lozi yenye gramu 100
Nishati = 579kcal
Protini = 21.2g
Kabohaidreti = 21.6g
Nyuzilishe = 12.5g
Mafuta = 49.9g
Maji = 4.4g
Madini yanayopatiokana kwenye lozi yenye gramu 100
Zinki = 3.1mg
Kopa = 0.99mg
Kalisiumu = 264mg
Chuma = 3.72mg
Magnesium = 268mg
Potasium = 705mg
Sodiamu = 1mg
Manganese = 2.3mg
Fosfolasi = 484mg
Vitamini zinazopatikana kwenye lozi yenye gramu 100
Vitamini A =1IU
Vitamini B1 = 0211mg
Vitamini B2 = 1mg
Viatmini B3 =3.385mg
Vitamini B5 = 0.5mg
Vitamini B6 = 0.143mg
Vitamini B9 = 50mcg
Vitamini E = 25.6mg
Faida za lozi
Ulaji wa karanga ya lozi husaidia;
Kupunguza na kurekebisha uzito usiohitajika mwilini.
Kuupa mwili nguvu na kupunguza njaa
Kuongeza kinga ya mwili
Kuimarisha afya ya moyo na kukukinga dhidi ya maradhi ya moyo
Kupunguza mafuta mafuta yasiyohitajika mwilini
Kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu
Kuimarisha afya ya ngozi na nywele
Kuimarisha afya ya akili
Imeboreshwa,
4 Desemba 2021, 16:32:32
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Harris LJ, ed. (2013). Improving the Safety and Quality of Nuts. Elsevier, Woodhead Publishing Series in Food Science, Technology and Nutrition. pp. 36–37. ISBN 978-0-85709-748-4.
Rushing, et al (2019). "Aflatoxin B1: A review on metabolism, toxicity, occurrence in food, occupational exposure, and detoxification methods". Food and Chemical Toxicology. 124: 81–100.
Gradziel, T.M. (2011). "Origin and Dissemination of Almonds". In J. Janick (ed.). Horticultural Reviews. 38. Wiley-Blackwell. p. 55.
Barreca, Davide et al. “Almonds (Prunus Dulcis Mill. D. A. Webb): A Source of Nutrients and Health-Promoting Compounds.” Nutrients vol. 12,3 672. 1 Mar. 2020, doi:10.3390/nu12030672
de Souza R.G.M, et al. Nuts and Human Health Outcomes: A Systematic Review. Nutrients. 2017;9:1311.
Chen C.-Y, et al. nutrition and health perspective on almonds. J. Sci. Agric. Food Sci. 2006;86:2245–2250.