Mwandishi:
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
Dkt. Mangwella S, MD
Ijumaa, 17 Desemba 2021
Mafuta ya Omega 3
Mafuta ya Omega 3 huhusika kusimamia suala zima la ugandishaji damu na ujenzi wa kuta za chembe hai za ubongo. Licha ya kuwa na umuhimu mkubwa, huwa hayatengenezwi mwilini bali hupatikana kwa kula vyakula vyenye mafuta haya.
Faida za mafuta ya omega 3
Mafuta ya omega 3 huwa na faida zifuatazo ambazo zimeonekana kwenye tafiti mbalimbali;
Hukinga mwili kupata maradhi ya moyo na kiharusi
Hukinga mwili dhidi ya saratani
Hukinga mwili dhidi ya magonjwa ya michomo tumboni
Hukinga mwili dhidi ya maradhi yanayotokana na shambulio binafsi la kinga ya mwili kama baridi yasibi (rheumatoid arhtritis) na lupus
Vyakula vyenye mafuta ya omega 3
Mafuta ya omega 3 hupatikana kwenye vyakula vifuatavyo;
Samaki wa waishio katika maji baridi kama sangara huwa na kiasi kikubwa sana cha mafuta haya
Maharage ya soya
Nazi
Mboga za majani kama Spinach, kabegi, chainizi n.k
Mchanganyiko wa matunda yenye rangi ya kijani
Imeboreshwa,
17 Desemba 2021 10:16:06
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Kristina Novotny, et al. Omega-3 Fatty Acids. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK564314/. Imechukuliwa 17.12.2021.
Gammone, et al. “Omega-3 Polyunsaturated Fatty Acids: Benefits and Endpoints in Sport.” Nutrients vol. 11,1 46. 27 Dec. 2018, doi:10.3390/nu11010046.