top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Peter A, MD

Ijumaa, 22 Oktoba 2021

Mahindi
Mahindi

Huwa na kiwango kikubawa cha wanga,nyuzinyuzi na protini ambayo hupatikana katika kiini cha mbegu, wanga husaidia kutupa nguvu mwilini na nyuzinyuzi hizi husaidia katika kulahisisha umengenyaji na upitishaji wa chakula kwa haraka katika mfumo wa chakula na protini husaidia kujenga mwili na kuponya majeraha.


Huwa na vitamin A na E na pia mafuta kwa kiwango kidogo na madini ya phosphorus , potassium na kalisium ambayo hupatikana katika ganda(nyuzinyuzi) na kiini chake

Mahindi yakishakobolewa huwa hayana nyuzinyuzi, protini na viinirishe vingine kama vilivyotajwa hapo juu. Matumizi ya unga wa mahindi uliokobolewa ama mahindi yaliyokobolewa huweza kusababisha mtumiaji kupata choo kigumu ama kutokwenda haja kubwa kwa mda mrefu.

Hali hii ya chakula kukaa mda mrefu kwenye mfumo wa chakula huweza pelekea mtu kupata saratani mfumo wa chakula kutokana na kuta za tumbo kukutana na kemikali mbalimbali zilizo kwenye mabaki ya mmeng'enyo wa chakula kwa mda mrefu.

Penda kutumia mahindi yasiyokobolewa kwa afya yako njema, lakini kwa vile kwa sasa mahindi mengi huwekewa dawa ya kuua wadudu ili kufanya yasihalibike. Ukiwa unatumia mahindi ambayo yamewekwa dawa basi hakikisha unayaosha vema ili yasikudhuru, au subiri mpaka dawa iliyowekwa kwenye mahindi iishe mda wake.

Imeboreshwa,
10 Novemba 2021 11:03:14
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

  1. Xuanjun Feng et al. Nutritional and physicochemical characteristics of purple sweet corn juice before and after boiling. https://doi.org/10.1371/journal.pone.0233094. Imechukuliwa 22.10.2021

bottom of page