Mwandishi:
Mhariri:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
Dkt. Peter A, MD
17 Februari 2026, 04:19:27
Tango: Faida za Kiafya
Huwa na kiwango kikubwa cha vitamin K na molybdenum, pia huwa na kiwango kikubwa cha pantothenic acid
Hata hivo madini ya shaba, potassium manganese, phosphorus, biotin na silica, huwa kwa kiwango cha kutosha
Pia tango huwa na vitamin C na B1
Faida za tango mwilini
Asilimia 96 ni maji, maji haya husaidia kutupa maji mwilini endapo upo bize na huna muda wa kunywa maji.
Huondoa joto ndani na nje ya mwili
​
Kula tango, mwili wako utaondokana na kiungulia na pia hata kama mwanga wa jua umekuchoma paka majimaji ya tango na utapata unafuu
Huondoa sumu mwilini
Majimaji yaliyo katika tango hufanya kazi kama fagio na huosha mwili kwa kutoa uchafu kutoka kwenye viungo mbalimbali mwilini, kwa matumizi ya kuzingatia, tango huweza kuyeyuha mawe yaliyotengenezwa kwenye figo
Hukupa vitamin A,B na C, ambazo huinua kinga ya mwili, hukutia nguvu, na kukufanya ujisikie vema.
Huipa ngozi madini rafiki kama magnesium, potassium,na silicon
Husaidia kupunguza uzito
Ukitumia kama supu ama kwenye mchanganyiko wa matunda unaweza kupunguza uzito kwa kiasi kikubwa
Hupambana na saratani
Hulinda mwili dhidi ya saratani mbalimbali na tafiti nyingi zimefanyika kuonyesha uwezo huo.
Tango huwa na kemikali ya polyphenols iitwayo lignans (pinoresinol, lariciresinol, na secoisolariciresinol), ambayo huweza kuzuia kupata saratani za titi,mfuko wa kizazi, kiwanda cha mayai, saratani ya tezi dume. Kemikali ya phytonutrients iitwayo cucurbitacins, hufanya kazi ya kuua chembe saratani hii ni kutokana na tafifi za George Mateljan Foundation
​
Huimarisha shinikizo la damu
​
Ikiwa shinikizo liko juu ama chini watu hao wakila tango kwa utaratibu hujisikia vema na kuimarika.
Juisi ya tango husafisha na kuponya magonjwa ya fizi na kuacha kinywa chako kikiwa na harufu nzuri.
Husaidia mmengenyo wa chakula
Nyuzi lishe katika tango husaidia mpitisho wa chakula katika mfumo wa chakula kuwa rahisi na kuepukana na magonjwa yatokanayo na kukaa kwa chakula mda mrefu tumboni kama saratani.
Hurainisha nywele na kucha
Madini ya Silica, madini ya ajabu katika tango hufanya nwele na kucha kuwa imara na kung'aa
Huweza kutibu maumivu ya misuli na maungio-vitamin na madini katika tango hulifanya kuwa na uwezo wa kuondoa maumivu ya misuli na maungio
Husaidia figo
Hupunguza kiwango cha kemikali ya uric acid na kufanya figo iwe na uwezo wa kufanya kazi vema
Hudhibiti sukari mwilini
Tango huwa na homoni inayohitajika kwenye kongosho ili kuzalisha insulin, hivo kula tango hupelekea uzalishaji mzuri wa insulin na hivo kiwango cha sukari katika damu huwa cha kawaida endapo tango litaliwa ipasavyo kulingana na taratibu
Hupunguza Lehemu
Kemikali inayoitwa sterols iliyo kwenye tango huweza kusaidia kupunguza kiwango cha rehemu mbaya kwenye damu ambayo huweza sababisha magonjwa ya kuganda kwa mafuta kwenye mishipa ya damu na moyo.
Imeandikwa;
22 Oktoba 2021, 11:27:46
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
Burza W, et al. Cucumber (Cucumis sativus L.). Methods Mol Biol. 2006;343:427-38. doi: 10.1385/1-59745-130-4:427. PMID: 16988365.
