top of page

Mwandishi:

Mhariri:

Dkt. Peter R, CO

Jumapili, 27 Machi 2022

Tanipu
Tanipu

Tanipu ni zao la mbogamboga litokanalo na mizizi kutoka katika familia ya Brasssicaceae. Zao hili hutumika kama chakula/mboga baada ya kupikwa ili kupata faida inayotakiwa.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Tanipu


 • Mafuta

 • Madini

 • Sukari

 • Nyuzilishe

 • Protini

 • Vitamini

 • Kabohaidreti

 • Maji


Kemikali muhimu inayopatikana kwenye Tanipu


Tunda la tanipu lina kemikali muhimu ambazo ni Gluconapin na Glucobrassicanapin.


Viinilishe vinavyopatikana kwenye Tanipu yenye gramu 100


 • Nishati = 28kcal

 • Mafuta = 0.1g

 • Maji = 91.87g

 • Kabohaidreti = 6.4g

 • Sukari = 3.8g

 • Nyuzilishe = 1.8g

 • Protini = 0.9g


Vitamini zinazopatikana kwenye Tanipu yenye gramu 100


 • Vitamini B1 = 0.04mg

 • Vitamini B2 = 0.03mg

 • Vitamini B3 = 0.4mg

 • Viatmini B5 = 0.6mg

 • Vitamini B6 = 0.09mg

 • Vitamini B9 = 15mcg

 • Vitamini C = 21mg

 • Vitamini E =0.3mg

 • Vitamini K = 0.7mg


Madini yanayopatikana kwenye Tanipu yenye gramu 100


 • Kalishiamu = 30mg

 • Kopa = 0.09mg

 • Madini Chuma = 0.3mg

 • Magineziamu = 11mg

 • Manganaizi = 0.134mg

 • Fosifolasi = 27mg

 • Potashiamu = 191mg

 • Sodiamu = 67mg

 • Zinki = 0.27mg


Faida za kiafya zitokanazo na ulaji wa Tanipu


 • Kuimarisha mzunguko wa damu mwilini, afya ya moyo na kuzuia tatizo la shinikizo la juu la damu

 • Kusaidia mfumo wa mmeng`enyo wa chakula

 • Kuimarisha na kuongeza kinga ya mwili

 • Kuimarisha mifupa

 • Kuzuia athari za kupatwa aina mbalimbali za kansa

 • Kupunguza /kuzuia athari zitokanazo na uginjwa wa gauti maumivu ya mda mrefu Pamoja na baridi yabisi

Imeboreshwa,
27 Machi 2022 17:31:17
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
 

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii

Rejea za mada hii

 1. Turnips. https://www.nutritionvalue.org/Turnips%2C_raw_nutritional_value.html?size=100+g. Imechukuliwa tarehe 10 January 2022.

 2. Paul S, Geng CA, Yang TH, Yang YP, Chen JJ. Phytochemical and Health-Beneficial Progress of Turnip (Brassica rapa). J Food Sci. 2019 Jan;84(1):19-30. doi: 10.1111/1750-3841.14417. Epub 2018 Dec 18. PMID: 30561035. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/30561035/. Imechukuliwa tarehe 10 January 2022.

 3. Fernandes F, Valentão P, Sousa C, et al. Chemical and antioxidative assessment of dietary turnip (Brassica rapa var. rapa L.). Food Chemistry. 2007;105(3):1003–10. 10.1016/j.foodchem.2007.04.063. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC7888597/. Imechukuliwa tarehe 10 January 2022.

bottom of page