Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
Alhamisi, 16 Desemba 2021

Uji wa mahindi
Hutengenezwa kwa punje za mahindi zilizolowekwa kwenye maji.
Viungo
Mpaka sasa, ni kawaida kuandaa kwa kutumia viungo hivi:
Unga wa mahindi (kati ya gramu 100 hadi 200 kwenye lita moja ya maji).
Aina mbalimbali za matunda.
Maziwa (yaweza kuwa ya soya).
Pilonsillo/panela (sukari ya kahawia) au sukari ya miwa.
Vanilla au mdalasini.
Uandaaji
Mchanganyiko wa viungo hupashwa kwenye moto mdogo, bila kuchemsha, kisha kinywaji hutumika kikiwa cha moto. Kinywjai hiki hutumika kama chakula cha asubuhi kinachotia nguvu pamoja na sambusa (iliyojazwa unga wa mahindi).
Aina za atole
Kuna aina mbalimbali za Atole, kwa mfano:
Champurrado (chokoleti nzito ya Atole, ya moto):
Hutoka katika atole, ambayo hupatikana kwa kuongeza chokoleti na kuichemsha hadi mchanganyiko unakuwa mzito.
Chilate (mahindi yaliyokaangwa, tangawizi, na atole yenye pilipili manga)
Pilipili ya unga huongezwa kwenye mahindi yaliyokaangwa, unga wa chokoleti, bizari,tangawizi na mdalasini. Hutumika ikiwa ya moto pamoja na sukari za kienyeji.
Emolienti ya kiperu
Dawa ya kunywa kutoka peru iliyotengenezwa kwa shayiri na mimea tiba
Inaaminika kuwa emolienti ilikuwa tayari ikiwa imeandaliwa kwa mimea tiba tu. Inaweza kuongeza punje za shayiri, mbegu za pamba na limau ili kutengeneza kinywaji kamili.
Kwa sasa aina mbalimbali za emolienti zinapatikana, lakini zote zina shayiri, mbegu za pamba na mimea ya tiba kwa pamoja.
Kiungo cha kungumanga (lepidium meyenii) kinaweza kuongeza nguvu ya tendo la ndoa, ukucha wa paka (uncaria tomentosa) kuimarisha kinga na mimea mingine ya tiba. Emolienti hasa hutumika ikiwa ya moto, ikiwa baridi pia, iwe asubuhi na kifungua kinywa au mchana.
Sifa
Kuongeza mkojo
Hukinga kufanyika kwa mawe kwenye figo
Hulainisha choo
Huimarisha mmeng’enyo wa chakula
Hupunguza kiwango cha lehemu
Hupunguza ufyonzwaji wa sukari tumboni. (Kutokana na kuwa na nyuzinyuzi zinazoyeyuka za shariyi na mbegu za pamaba)
Imeboreshwa,
16 Desemba 2021, 18:56:43
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
No, Huiwon et al. “Purple corn extract alleviates 2,4-dinitrochlorobenzene-induced atopic dermatitis-like phenotypes in BALB/c mice.” Animal cells and systems vol. 25,5 272-282. 8 Sep. 2021, doi:10.1080/19768354.2021.1974938.
Pollitt E, et al. Nutrition in early life and the fulfillment of intellectual potential. J Nutr. 1995 Apr;125(4 Suppl):1111S-1118S. doi: 10.1093/jn/125.suppl_4.1111S. PMID: 7536831.
Brown JL, et al. Malnutrition, poverty and intellectual development. Sci Am. 1996 Feb;274(2):38-43. doi: 10.1038/scientificamerican0296-38. PMID: 8560214.