Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Sospeter B, MD
Ijumaa, 12 Novemba 2021
Vyakula vyenye oxalate nyingi
Oxalate ni kampaundi inayopatikana kwenye vyakula mbalimbali vya nafaka na mimea na pia hutolewa na mwili kama zao la umetaboli. Matumizi ya vyakula vyenye oxalate kwa wingi husababisha mawe kwenye figo.
Ni kiasi gani cha oxalate kinahitajika kwa siku?
Vyanzo vya kiafya vinashauri kupata chini ya miligramu 100 za oxalate kwa siku. Hata hivyo watu hutumia kiasi cha miligramu 200 hadi 300 kwa siku, kiasi mara 2 hadi 3 ya kiasi kianchoshauriwa kwa siku. Unapaswa kuwasiliana na daktari wako kukushauri kama unapaswa kupuguza kiasi cha oxalate unachotumia kwa siku.
Vyakula vyenye oxalate kwa wingi
Vyakula vyenye oxalate kwa wingi ni
Maharagwe
Bia
Mzizi beet
Chocolate
Tende
Kahawa
Matunda madogodogo
Cranberries
Spinach
Karanga
Machungwa
Rhubarb.
Soda (cola)
Maharagwe ya soya
Maziwa ya soya
Spinach
Viazi vitamu
Chai nyeusi
Tofu
Ngano
Kiasi cha oxalate kwa kila chakula
Baadhi ya vyakula na kiwango cha oxalate katika miligramu vimeelezewa hapa chini.
Spinach
Nusu kikombe cha mboga iliyopikwa huwa na miligramu 755 za oxalate
Maziwa ya soya
Mililita 1 ya tofu ya soya huwa na miligramu 0.9 za oxalate
Mililita 250 za maziwa ya soya huwa na gramu 336 za oxalate
Lozi
Gramu 28 za karanga ya lozi ( sawa na punji 22) huwa na miligramu 122 za oxalate.
Viazi
Kiazi saizi ya kati kilichookwa huwa na miligramu 97 za oxalate
Beet
Mililita 250 za sharubati ya beet huwa na miligramu 152 za oxalate.
Maharagwe ya navy
Mililita 125 za maharagwe haya huwa na miligramu 76 za oxalate
Mililita 250 za sharubati ya raspberi huwa na miligramu 48 za oxalate
Tende
Licha ya kuwa na sukari kwa wingi, tende moja huwa na miligramu 24 za oxalate
Unawezaje kupunguza kiwasi cha oxalate mwilini?
Vyakula vingi vya mimea tunavyokula huwa nan a oxalate lakini pia huwa na madini pamoja na virutubisho vingine muhimu sana mwilini. Ili kupunguza hatari ya kupata madhara ya kufanyika kwa mawe kwenye figo kutokana na vyakula vyenye oxalate kwa wingi fanya mambo yafuatayo;
Kunywa maji ya kutosha kila siku kama huna shida inayokuzuia kunywa maji. Maji husaidia kusafisha mwili na kuondoa kampaundi ya oxalate.
Kula vyakula vyenye calcium kwa wingi. Calcium huungana na oxalate wakati wa mmeng’enyo wa chakula na kufanya ishindwe kufyonzwa vema.
Dhibiti kiasi cha sodium na sukari unachotumia kwa siku. Sodium na sukari huongeza hatari ya kutengenezwa kwa mawe ndani ya figo.
Pata kiasi cha vitamin C kinachoshauriwa kiafya kwa siku. Kula vitamin C kwa wingi huchangia ongezeko la oxalic acid na utengenezwaji wa mawe ndani ya figo
Pika mboga za majani kabla ya kula ili kupunguza kiasi cha kampaundi ya oxalate.
Imeboreshwa,
13 Novemba 2021, 07:23:43
Bofya hapa kusoma zaidi kuhusu namna ya kuandaa vyakula mbalimbali vinavyoweza kukukinga dhidi ya magonjwa ya shinikizo la damu la juu na Kisukari, pia kuupa mwili wako uwezo wa kudhibiti magonjwa ya kisukari na shinikizo la juu la damu(presha).
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba zaidi kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya baada ya kusoma makala hii.
Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kutumia namba za simu au kubonyeza link ya Pata Tiba chini ya tovuti hii
Rejea za mada hii
UMHS. Foods High in Oxalate. https://www.uofmhealth.org/health-library/aa166321. Imechukuliwa 12.11.2021
WebMD. Food high in oxalate. https://www.webmd.com/diet/foods-high-in-oxalates#2-3. Imechukuliwa 12.11.2021
Cleveland clinic. Kidney Stones: Oxalate-Controlled Diet. https://my.clevelandclinic.org/health/articles/11066-kidney-stones-oxalate-controlled-diet. Imechukuliwa 12.11.2021
Mitchell, Tanecia et al. “Dietary oxalate and kidney stone formation.” American journal of physiology. Renal physiology vol. 316,3 (2019): F409-F413. doi:10.1152/ajprenal.00373.2018
Noonan SC, et al. Oxalate content of foods and its effect on humans. Asia Pac J Clin Nutr. 1999 Mar;8(1):64-74. PMID: 24393738.
D'Alessandro, et al. “Which Diet for Calcium Stone Patients: A Real-World Approach to Preventive Care.” Nutrients vol. 11,5 1182. 27 May. 2019, doi:10.3390/nu11051182.
Brinkley L, et al. Bioavailability of oxalate in foods. Urology. 1981 Jun;17(6):534-8. doi: 10.1016/0090-4295(81)90069-8. PMID: 7245443.
Brinkley LJ, Gregory J, Pak CY. A further study of oxalate bioavailability in foods. J Urol. 1990 Jul;144(1):94-6. doi: 10.1016/s0022-5347(17)39377-1. PMID: 2359186.