Imeandikwa na madaktari wa ULY-Clinic
​
Goita
Katika mwaka 1656, Thomas Wharton alielezea asili tofauti ya kile alichokiita tezi ya shingo ama tezi ya thairoid na kuitofautisha na tezi koo, kwa sababu muundo huo ulikuwa ukifahamika kwamba tezi ya thairoid ni tezi ya koo ,tokea enzi za mzungu anayeitwa Andreas Vesalius katika karne ya 16. Ilikuwa takribani miaka 200 na zaidi kabla utambuzi wa tezi shingo kutambuliwa ama kuelezewa.
Mtu mzima ana tezi shingo ama tezi ya thyroid yenye uzito wa gramu 10 hadi 25, tezi shingo ina sehemu kuu 2 na sehemu hizi zimeshikamanishwa na ukuta unaoitwa isthmus. Karibia asilimia 50 ya tezi ya thyroid huwa inaonyesha kuwa na kijioteo cha tezi katikati ya isthmus na kinaumbo la piramidi(pembetatu).
Goita ni tezi ya thyroid iliyokuwa kupita kiasi, inaweza kuwa imesambaa kwa mapana ama kuwa na manundu manundu. Goita inaweza kukua na kufika mabegani ama wakati mwingine bila hata kuonekana kukua mbele ya shingo ama kuonekana kabisa
Kwa sababu ya mahusiano ya kianatomia(maumbile) kati ya tezi shingo, kolomeo la hewa, koo na mishipa ya fahamu ya laryngeal ya juu na ya chini(inferior and superior laryngeal nerve) na mrija wa kupitisha chakula, kukua kwa tezi hii kunaweza kusababisha mgandamizo kwenye maeneo hayo na kuzalisha dalili mbalimbali zinazotokana na migandamizo kwnenye maeneo husika. Uzalishaji wa homoni katika goita unaweza kuwa wa kiasi cha kawaida ama kuzalishwa kwa wingi, hapa tunaita goita lenye sumu ama toxic goita
Dalili za goita
​
Goita inaweza kujitokeza na dalili tofauti, kama zifuatazo
-
Uvimbe mbele ya shingo
-
Kupumua kwa shida/kupata shida wakati wa kuvuta pumzi
-
Kutoa sauti za miruzi ama sauti kubaadilika
-
Kushindwa kumeza chakula
-
Kuhisi joto sana mwilini ama kupata njaa sana
-
Kuhisi baridi na
-
Dalili zingine za wingi ama upungufu wa homoni ya thyroid mwilini
ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote ile ya kiafya.
​
​
Imeboreshwa,14.06.2020
​
Rejea za mada hii
​
-
Goiter. American Thyroid Association. http://www.thyroid.org/what-is-a-goiter/. Imechukuliwa 14.06.2020
-
Goiter. Hormone Health Network. https://www.hormone.org/diseases-and-conditions/goiter. Imechukuliwa 14.06.2020
-
Iodine deficiency. American Thyroid Association. http://www.thyroid.org/iodine-deficiency/. Imechukuliwa 14.06.2020
-
Simple nontoxic goiter (euthyroid goiter). Merck Manual Professional Version. https://www.merckmanuals.com/professional/endocrine-and-metabolic-disorders/thyroid-disorders/simple-nontoxic-goiter. Imechukuliwa 14.06.2020
-
NIH. Walsh JP. Managing thyroid disease in general practice. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/27510349/. Imechukuliwa 14.06.2020
-
Smith PW, et al. Thyroid. In: Sabiston Textbook of Surgery: The Biological Basis of Modern Surgical Practice. 20th ed. Saunders Elsevier; 2019. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 14.06.2020
-
Goldman L, et al., eds. Thyroid. In: Goldman-Cecil Medicine. 25th ed. Saunders Elsevier; 2016. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 14.06.2020
-
Flint PW, et al. Disorders of the thyroid gland. In: Cummings Otolaryngology: Head & Neck Surgery. 6th ed. Saunders Elsevier; 2015. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 14.06.2020
-
Medeiros-Neto G, et al. Iodine-deficiency disorders. In: Endocrinology: Adult and Pediatric. 7th ed. Saunders Elsevier; 2016. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 14.06.2020