top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY CLINIC

​

Homa

 

Homa kitabibu humaanisha kuongezeka kwa joto la mwili zaidi ya lile la kawaida(nyuzi joto  za sentigredi 37), mara nyingi husababishwa na ugonjwa unaoendelea mwilini. Mtu akipata  homa inamaanisha mwili umetambua kuna kitu kisicho cha kawaida kinaendelea. Katika tiba homa pia hujulikana kwa jina la hyperthermia, pyrexia na kupanda kwa joto la mwili.

​

Kwa watu wazima, homa inaweza  kusababisha mtu kujihisi vibaya, hata hivyo huna haja ya kuogopa endapo homa si kali au si zaidi ya nyuzi joto za sentigrade 39.4. Homa kwa watoto hata ikiongezeka kwa kiasi kidogo, mara nyingi huweza kumaanisha kuna tatizo la hatari ndani ya mwili wa mtoto.

Homa huweza kupotea ndani ya siu chache, matumizi ya dawa pia yanaweza kutuliza homa. Dawa za kutuliza homa haziwezi kuondoa chanzo cha homa, hivyo ni vema kuwasiliana na daktari ili kujua tatizo ni nini hata baada ya homa kutulia baada ya kunywa dawa za kutuliza homa.

 

Je unashauriwa kutumia dawa za kutuliza homa kabla ya kuwasiliana na daktari?

 

Dawa za kutuliza homa au zile za kutuliza maumivu mara nyingi hazishauriwi kutumika, hii ni kwa sababu hufisha ishara mbalimbali ambazo daktari angeziona ili kutambua kirahisi ni nini kinachosababisha homa hiyo. Hata hivyo unaweza kuwasiliana na mtaalamu wa afya mara moja kwa ushauri ili akuambie kama kuaa umuhimu wa kutumia dawa au la kabla ya kumwona. ULY Clinic ipo tayari kukusaidia kwa huduma ya ushauri  na tiba kuhusu nini cha kufanya kupitia namba za simu chini ya tovuti hii.

 

Dalili za homa

 

Dalili za homa hutegemea kisababishi, pamoja na hivyo huweza kuja pamoja na;

​

  • Kutokwa na jasho

  • Kutetemeka mwili

  • Maumivu ya kichwa

  • Maumivu ya misuli

  • Kukosa hamu ya kula

  • Mtoto kulialiabila kubembelezeka

  • Kuishiwa maji mwilini

  • Uchovu wa mwili

  • Kupata degedege kwa watoto kati ya miezi 6 na miaka mitano

 

Namna gani ya kutambua kuwa una homa

 

Homa inaweza kutambuliwa kwa kutumia kipimajoto,  vipimajoto vipo vya aina nyingi ambavyo ni;

​

  • Vipima joto vya kwapani

  • Vipima joto vya kinywa

  • Vipima joto vya paji la uso

  • Vipimajoto vya njia ya haja kubwa

  • Vipima joto vya masikio

​

Kumbuka;Unawezakuhisi kuwa unahoma na hali huna homa, ni vema kujua joto lako la mwili kwa kutumia kipima joto, nunua kipima joto ukae nacho nyumbani kwani ni muhimu sana na utamsaidia daktari  kufanya maamuzi ya kitiba endapo umempigia simu wakatiumepima joto lao au mtoto wako.

 

Kipimajoto gani ni kizuri?

 

Kama unataka kununua kipimajoto chako, ni vema kupata kipima joto cha njia ya haja kubwa au kile cha kuweka kinywani. Vipima joto hivi ni vizuri na vinaleta majibu sahihi zaidi kwa kuwa husoma joto la ndnai ya mwili.

 

Joto la kawaida ni nyuzi joto za sentigredi ngapi?

 

Joto la kawaida la mwili ni nyuzi za sentigredi 37, hata hivyo joto linaweza kutofautiana kwa pointi kadhaa mfano nyuzi joto 36.1hadi nyuzi joto 37.2 huchukuliwa kama joto la kawaida.

 

Ni wakati gani umwone daktari?

​

Baadhi ya wakati, homa husababishwa na sababu ambazo hupaswi kuwa na hofu kama vile;

​

  • Mazoezi makali

  • Kuingia hedhi au kuingia siku za kuchavushwa kwa yai(ovulesheni)

  • Mabadiliko ya hali ya hewa(asubuhi joto la mwili huwa chini kidogo na machana huwa juu kidogo kutokana na kupigwa na mwangawa jua)

 

Unapaswa kutafuta msaada wa haraka endapo mtoto  ana hali zifuatazo;

​

  • Kichanga kupata homa isiyo na sababu au watoto chini ya mwaka mmoja na joto la mwili ni zaidi ya nyuzi joto za sentigredi 37.9 na kuendelea. Licha ya kuwa na dalili zingine kama zilivyoorodheshwa hapo juu

  • Mtoto amepata chanjo hivi karibuni

  • Ana maambukizi au tatizo kubwa la kiafya linalofahamika mfano kuwa na kinga za mwili za chini au matumizi ya dawa za kushusha kinga za mwili

  • Kwa mtoto mdogo zaidi ya mwaka mmoja endapo amekuwa mchovu, mkali, hali ya kutapika kunakojirdia  maumivu ya kichwa, tumbo, kuharisha au dalili zingine

  • Endapo mtoto zaidi ya mwaka mmoja aliachwa ndani ya gari lenye joto.

  • Endapo homa kwa mtoto iimedumu zaidi ya siku tatu bila kupotea

  • Endapo mtoto wa zaidi ya mwaka mmoja anashindwa kukuangalia macho kwa macho na ana homa

  • Mtoto kutoacha kulia licha ya kubembelezwa

  • Maumivu ya kifua

  • Kupumua kwa shida

  • Kushindwa kutembea/kusimama

 

Kwa watu wazima mwone daktari endapo joto limepanda zaidi ya nyuzi 39.4 digrii za sentigredi pamoja na;

​

 

 

Ni nini husababisha homa?

 

Homa hutokea endapo sehemu ya mwili inayoitwa hypothalamus ikiamuru kiwango cha joto ndani ya mwili kupanda kutoka cha kawaida (nyuzi joto 37 za sentigredi) kwenda cha juu. Kiwango kikipanda  mwili huitikia kwa kuhisi baridi kali, kutetemeka na kujongea kwa misuli ili joto hilo lifikie pale ambapo tezi ya hypothalamus imeamuru lifikiwe. Hii hutokea makusudi ili kupambana na maambukizi yaliyoingia ndani ya mwili.

​

Mara nyingi  visababishi vya homa vinaweza kujulikana, hata hivyo kuna wakati huwa havifahamiki kabisa.

 

Visababishi vya homa vinvyojulikana huwa pamoja na;

 

  • Maambukizi mbalimbali kama ya bakteria kwenye ogani na mifumo mbalimbali mwilini(mapafu, ini, figo, mfumo wa mkojo n.k, maambukizi ya vimelea vya malaria n.k)

  • Maambukizi ya virusi

  • Kukaa kwenye joto kali

  • Kiharusi

  • Matumizi ya dawa ya kulevya kama kokeini na amphetamine

  • Magonjwa Fulani ya mwili kama homa ya rheumatoidi athraitizi, lupasi, inflamatori baweli

  • Vimbe za saratani

  • Madhaifu ya homoni mwilini kama hyperthyroidism

  • Matumizi ya dawa aina zingine kama zile za kushusha shinikizo la damu au kifafa

  • Kutumia baadhi ya chanjo kama vile chanjo ya dondakoo, tetenasi na pneumococcal

  • Sababu zisizojulikana

 

Madhara ya homa

 

Kwa watoto kuanzia miezi sita na miaka mi 5, wanaweza kupata degedege kutokana na homa, mbali na degedege hupoteza fahamu na kutetemeka sehemu zote za mwili kama mtu mwenye pepo pia hutokea.

​

Ni vema kuwasiliana na daktari haraka kupata uchunguzi maana degedege la mara kwa mara huweza kupelekea kupata mtindio wa ubongo na kifafa siku za mbeleni.

 

Endapo mtoto atapata degedege fanya mambo yafuatayo;

​

  • Mlaze mtoto kifudifudi kwenye sakafu

  • Ondoa vitu vyenye ncha kali kwenye mazingira ya karibu na mtoto

  • Legeza nguo zilizobana

  • Mshike mtoto ili kuzuia kujiumiza kwa kugonga vitu vilivyokaribu naye au sakafu

  • Usiweke kitu chochote kwenye kinywa cha mtoto

  • Ondoa chochote kilichopo kwenye kinywa cha mtoto baada ya degedege kutulia(usiweke kidole wakati degedege linaendelea kuepukwa kung’atwa

  • Mpeleke mtoto hospitali mapema u piga namba za simu kw huduma ya kwanza ukiwa nyumbani

 

Je unaweza kujikinga kupata homa?

 

Inaweza kuwa ngumu kujikinga kupata homa, hata hivyo kuna vitu unavyoweza kufanya ili kujikinga kama vile;

​

  • Kupunguza hatari ya kupata maambukizi kwa kunawa mikono yako kabla ya kula baada ya kwenda chooni, baada ya kutoka kwenye mkusanyiko wa watuw engi, baada ya kutoka kwa mtu anayeumwa, baada ya kuhudumia mifugo na baada ya kusafiri kwenye usafiri wa watu wengi

  • Beba kitakasa mikono endapo huwezi kupata maji ya kunawa haswa unapokuwa unasafiri kwenye usafiri wa watu wengi, kwenda hospitali kusalimu wagonjwa au kukutana na mtu anayeumwa au kuhudumia mtu anayeumwa

  • Zuia kugusa maeneo ya uso wako na kinywani maana huweza kupitisha maambukizi na kuingia mwilini mwako

  • Funika kinywa unapopiga chafya, au geukia upande mwingine unapokuwa unapiga chafya, kisha nawa mikono ili usishike maeneo na kuwaambukiza wengine

  • Usitumie vyombo vya watoto  kama vile vikombe vya maji na beseni za kuogea

 

Matibabu ya homa ukiwa nyumbani ni yapi?

 

Matibabu nyumbani huwa pamoja na;

​

  • Kupunguza idadi ya nguo mwilini

  • Kukanda mwili kwa kutumia kitambaa cha baridi

  • Kunywa majiya kutosha mara kwa mara hii huweza kuzuia pia kupoteza maji mwilini kutokana na homa

  • Kupata muda wa kupumzika ili kuupa mwili nguvu ya kupambana na maradhiyaliyoingia mwilini. Hata hivyo hakikisha unafanya shughuli ndogondogo na kula mlo kamili

  • Kutumia dawa za kununua duka la dawa bariki kama parasetamo, aspirini(zuia dawa hii kutumika kwa watoto chini ya miaka mitatu kuzuia kupata tatizo la kufisha la sindromu ya Reye’s) 

 

ULY CLINIC inakushauri siku zote utafute ushauri kutoka kwa daktari wako kabla ya kuchukua hatu yoyote ile inayodhuru afya yako

 

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa kutumia namba za simu au kubonyeza neno Pata Tiba chini ya tovuti hii.

 

Imeboreshwa mara ya mwisho, 28.07.2020

​

Rejea za mada hii

​

  1. Fever. Healthline. https://www.healthline.com/health/fever. Imechukuliwa 28.06.2020

  2. Goldman L, et al., eds. Approach to fever or suspected infection in the normal host. In: Goldman-Cecil Medicine. 25th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2016. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.06.2020

  3. Fever. Merck Manual Professional Version. https://www.merckmanuals.com/professional/infectious-diseases/biology-of-infectious-disease/fever. Imechukuliwa 28.06.2020

  4. Fever in infants and children. Merck Manual Professional Version. https://www.merckmanuals.com/professional/pediatrics/symptoms-in-infants-and-children/fever-in-infants-and-children. Imechukuliwa 28.06.2020

  5. Temperature regulation and the pathogenesis of fever. In: Mandell, Douglas, and Bennett's Principles and Practice of Infectious Diseases. 9th ed. Elsevier; 2020. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.06.2020

  6. Fever. In: Nelson Textbook of Pediatrics. 20th ed. Philadelphia, Pa.: Elsevier; 2016. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.06.2020

  7. Ward MA. Fever in infants and children: Pathophysiology and management. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.06.2020

  8. Rosen's Emergency Medicine: Concepts and Clinical Practice. 8th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2014. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.06.2020

  9. Fever. Emergencies A-Z. American College of Emergency Physicians. http://www.emergencycareforyou.org/Emergency-101/Emergencies-A-Z/Fever. Imechukuliwa 28.06.2020

  10. Fever in the adult patient. In: Rosen's Emergency Medicine: Concepts and Clinical Practice. 8th ed. Philadelphia, Pa.: Saunders Elsevier; 2014. https://www.clinicalkey.com. Imechukuliwa 28.06.2020

  11. Approach to the adult with fever of unknown origin. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 28.06.2020

  12. Febrile seizures fact sheet. National Institute of Neurological Disorders and Stroke. https://www.ninds.nih.gov/Disorders/Patient-Caregiver-Education/Fact-Sheets/Febrile-Seizures-Fact-Sheet. Imechukuliwa 28.06.2020

  13. When and how to wash your hands. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/handwashing/when-how-handwashing.html. Imechukuliwa 28.06.2020

  14. How to protect yourself & others. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/coronavirus/2019-ncov/prevent-getting-sick/prevention.html. Imechukuliwa 28.06.2020

  15. WebMD. Fever. https://www.webmd.com/first-aid/fevers-causes-symptoms-treatments#2. Imechukuliwa 28.06.2020

bottom of page