top of page

Kiunga mwana

Mwandishi:

ULY CLINIC

17 Julai 2021 13:12:34

Kiunga mwana

Kiunga mwana ni nini?


Kiunga mwana ni mkusanyiko wa mishipa ya damu ya vena na arteri iliyofunikwa kwa pamoja na kuta ya tishu na hivyo kuifanya iwe na mwonekano wa kamba nyeupe inayoteleza. Kiunga mwana huwa na kazi ya kuunga mtoto na mama kupitia kondo la nyuma. Kazi yake kuu ni kusafirisha virutubisho na hewa ya oksijeni kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto pia kutoa uchafu kutoka kwa mtoto kwenda kwa mama. Uchafu huo ni pamoja na hewa ya kabon dayoksaidi na mazao ya umetaboli.


Baada tu ya mtoto kuzaliwa kiunga mwana hukatwa na kipande kidogo huachwa ili kianguke chenyewe baada ya wiki 1 hadi 2 toka mtoto amezaliwa. Watu wengi hufahamu kiunga mwana kuwa ni kitovu lakini maana kweli ya kitovu ni shina lililobaki baada ya kiunga mwana kudondoka.

Imeboreshwa,

6 Juni 2022 15:13:11

bottom of page