top of page
Mwandishi:
Imeboreshwa:
ULY CLINIC
6 Juni 2022, 17:50:11

Kukosa ujuzi laini wa kimota
Kukosa ujuzi laini wa kimota maana yake nini?
Kukosa ujuzi laini wa kimota ni madhaifu ya misuli midogo ya mikono kushindwa kufanya matendo yanayohitaji kufanywa kwa ustadi kutokana na magonjwa kwenye mfumo wa fahamu.
Mfano, kushindwa kufanya vitendo vifuatavyo hudhihirisha kukosa ujuzi laini wa kimota;
Kushika peni
Kupiga gitaa
Kuchora
Kushika kikombe
Kijiko
Kuokota kitu kwa vidole
Kufunga tai
Kukata kitu na mkasi
N.k
Kukosa ujuzi laini wa kimota huonekana utotoni kwa mtoto kuchelewa zaidi ya kawaidakupata maendeleo ya ukuaji wake.
Imeandikwa:
23 Julai 2021, 23:50:18
bottom of page
