top of page

Mzio wa dawa

Mwandishi:

ULY CLINIC

21 Julai 2021 19:08:39

Mzio wa dawa

Mzio wa dawa maana yake ni nini?


Mzio wa dawa ni mwitikio wa kinga za mwili kwenye kiini cha ka dawa kilichoingia kwenye damu. Mwitikio huu huleta madhara mwilini


Mzio wa dawa hutofautiana kati ya dawa moja na nyingine na mtu mmoja na mwingine, baadhi ya watu wanaweza wasiwe na mzio na dawa ambayo ina mzio na mtu mwingine.


Mfano dawa aina ya “penicilline” au dawa zenye ‘Sulphur’ zina uwigo mpana wa kusababisha mzio ambao unaweza kuwa hatari sana kwa baadhi ya watu.

Imeboreshwa,

6 Juni 2022 15:01:27

bottom of page