top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

Dkt. Benjamin L, MD

23 Agosti 2021 18:56:15

Cetirizine kwa mjamzito

Cetirizine kwa mjamzito

Cetirizine ni dawa isiyosababisha madhaifu ya kimaumbile kwa wanyama na pia hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa dawa jamii ya antihistamine (ikiwa pamoja na cetirizine) zina hatari kubwa ya kusababisha madhaifu ya uumbaji wa mtoto wakati anakua tumboni.


Licha ya taarifa hiyo, idadi ya wajawazito waliofanyiwa tafiti ni ndogo sana kuweza tumika thibitisha usalama wake kwa mjamzito. Ingawa cetirizine imeonekana kutoambatana na madhaifu ya uumbaji kwa mtoto, kama kuna ulazima wa kuitumia au kutumia dawa jamii yake, dawa dalaja la kwanza zitumike kama mbadala (haswa kipindi cha kwanza cha ujauzito), mfano mzuri wa dawa hizo ni chlorpheniramine au tripelennamine.


Cetirizine na loratadine huchukuliwa kuwa na hatari kidogo isipokuwa kipindi cha kwanza cha ujauzito (miezi mitatu ya kwanza).


Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwa cetirizine ina hatari kidogo


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwa cetirizine ina hatari kidogo ina maana gani?

Inawezekana kuwa hakuna taarifa za zoefu wa matumizi ya cetrizine au taarifa za binadamu wajawazito wachache waliotumia dawa hii zimeonyesha kutokuwa sumu kichanga tumboni kiasi cha kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo kama itatumiwa wakati huu. Dawa hii si sumu kwenye uumbaji wa kijusi (kwa dozi ambayo haikusababisha sumu kwa mama) kwa jamii zote za wanyama waliofanyiwa tafiti kwa kutumia dozi ambayo ni sawa au pungufu ya mara kumi ya ile ya binadamu, dozi inayotolewa kuendana na jumla ya eneo la mwili


Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji ina maana gani?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya cetrizine kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa cetrizine haina hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama aliyetumia dawa hii.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 17:20:53

Rejea za mada hii:

1. Mazzotta P, et al. Treating allergic rhinitis in pregnancy. Safety considerations. Drug Saf 1999;20:361–75.

2. Horak F, et al. Comparative tolerability of second generation antihistamines. Drug Saf 1999;20:385–401.

3. Position Statement of a Joint Committee of the American College of Obstetricians and Gynecologists and the American College of Allergy, Asthma and Immunology. The use of newer asthma and allergy medications during pregnancy. Ann Allergy Asthma Immunol 2000;84:475–80.

4. Product information. Zyrtec. Pfizer, 2001.

5. Einarson A, et al. Prospective controlled study of hydroxyzine and cetirizine in pregnancy. Ann Allergy Asthma Immunol 1997;78:183–6.

6. Schatz M, et al. Antihistamines and pregnancy. Ann Allergy Asthma Immunol 1997;78:157–9.

7. Wilton LV,et al. The outcomes of pregnancy in women exposed to newly marketed drugs in general practice in England. Br J Obstet Gynaecol 1998;105:882–9.

8. Einarson A, et al. The antiemetic effect of cetirizine during pregnancy. Ann Pharmacol 2000;34:1486–7.


9. Weber-Schoendorfer C, et al. The safety of cetirizine during pregnancy—a prospective
observational cohort study. Reprod Toxicol 2008;26:19–23.

bottom of page