top of page

Ripoti matokeo ya matumizi ya dawa wakati wa ujauzito

​

Je unatumia au utatumia dawa gani kwenye ujauzito ulionao sasa?

​

​

Taarifa nyingi kwa sasa kuhusu madhara au matokeo ya matumizi ya dawa wakati wa ujauzito, zimetokana na tafiti mbalimbali zinazofanyika kwa wanyama na binadamu. Taarifa hizo ni muhimu katika kuamua kwamba dawa aina fulani itumike kwenye kipindi fulani cha ujauzito au la. 

 

Kupitia kurasa hii ya ULY CLINIC utaweza kuripoti kuhusu matumizi ya dawa unazotumia sasa ukiwa mjamzito na matokeo yake baada ya kujifungua. Unaombwa kuwa mwaminifu kujaza taarifa zilizoulizwa hapa chini ili kuwezesha kupata taarifa sahihi zitakazosaidia kushauri mamlaka za dawa na watoa huduma za afya kuhusu matokeo ya matumizi ya dawa hiyo(hizo) na je endapo isitumike au itumike kwa kipindi gani katika ujauzito.

​

Kumbuka tafiti za sasa ndizo msingi wa matatuzi na ushauri wa maisha ya kesho. Kutoa taarifa sahihi, itasaidia kuboresha huduma za afya.

Neno siri

​

Ili kutengeneza neno siri ambalo utalitumia kuripoti matokeo ya matumizi ya dawa baada ya kujifungua au mimba kutoka, tafadhari fuata maelekezo hapa chini

​

Neno siri lako ni vema likawa lile ambalo utalikumbuka, ni vema baada ya kutengeneza ukaandika pembeni kwenye karatasi au sehemu ambayo unafikiria utaweza kulipata utakapolihitaji.

 

Mapendekezo ya neno siri yanatakiwa kuwa hivi,  Neno unalopenda, namba tatu unazopenda tarehemwezi  na mwaka uliozaliwa

 

Mfano neno ninalopenda ni kisarawe, namba tatu ninazopenda ni 102 tarehe niliyozaliwa ni 20 mwezi ni 11 mwaka ni 1988) hivyo kwa kuunganisha neno siri langu litakuwa kisarawe10220111988 

Taarifa zako zimetumwa kikamilifu.

Asante kwa kuchangia taarifa. Kumbuka endapo utajifungua au mimba kutoka kumbuka kurejea jaza fomu kwa kubofya kitufe cha 'Matokeo ya matumizi ya dawa baada ya ukomo wa  ujauzito'

Kuna taarifa zinakosekana kwenye fomu yako au mtandao unasumbua, tafadhari rudia tena kujaza na kutuma

Matokeo ya matumizi ya dawa baada ya ukomo wa ujauzito

​

Bofya kitufe chini ya maelezo haya endapo unataka kutoa taarifa baada ya mimba kutoka au kujifungua salama. Hii ni kwa wale tu ambao ujauzito umefikia kikomo, endapo ujauzito wako unaendelea basi subiri mpaka utakapofikia kikomo kisha urejee kuta taarifa hizo muhimu.

bottom of page