Mwandishi:
Mhariri:
ULY CLINIC
Dkt. Benjamin L, MD
16 Juni 2021, 19:41:40
Ondansetron na ujauzito
Ni dawa iliyo kundi la ‘dawa za kuzuia kutapika’ hutumiwa kuzuia kichefuchefu na kutapika kwa wagonjwa wanaotumia dawa za saratani, mionzi au kufuatia upasuaji.
Taarifa nyingi za wanyama na binadamu zinaonyesha kuwa dawa hii ina hatari kidogo ya madhaifu ya kiuumbaji kwa vichanga watakaozaliwa na mama aliyetumia dawa hii, hata hivyo kwenye tafiti nyingi zilizofanyika ni baada ya kipindi cha kwanza cha ujauzito.
Tafiti moja inaonyesha dawa hii inaongeza mara 2 uwezekano wa kupata madhaifu ya kiuumbaji kwenye moyo. Hata hivyo endapo itahitajika kutumika, ni vema ikatumika baada ya kipindi cha kwanza cha ujauzito.
Hakuna taarifa kuhusu madhara kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama aliyetumia dawa hii, hata hivyo dawa hupita na kuingia kwenye maziwa. Licha ya kuingia kwenye maziwa, inaonekana kuwa kiwango kitakachomfikia mtoto baada ya kufyonzwa kwenye utumbo kitakuwa kidogo sana kwenye damu ya mtoto.
Tafiti zaidi zinahitajika kufanyika kutambua kama inamadhara au la kama itatumika wakati wa kunyonyesha.
Ushauri dhidi ya matumizi kwa mama mjamzito
Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kidogo ya madhara kwa kijusi-kichanga
Taarifa za binadamu zinaonyesha hatari kidogo ya madhara kwa kijusi-kichanga ina maaga gani?
Kuna taarifa chache za uzoefu wa matumizi kwa binadamu kutoka kwenye dawa hii au dawa zilizo kundi moja au zinazofanana namna zinavyofanya kazi yake. Ikijumuisha ujauzito miezi mitatu ya kwanza, inaonyesha kuwa, dawa hii haiwakilishi kuwa na hatari yenye mashiko ya kuwa sumu kwa kichanga tumboni kuweza kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika muda wowote ule kwenye ujauzito. Taarifa chache za uzoefu wa matumizi kwa binadamu zinafanya taarifa za uzazi wa wanyama kutokuwa na mashiko.
Ushauri wa matumizi kwa mama anayenyonyesha
Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji
Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji
Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.
ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
1 Julai 2023, 17:20:53
Rejea za mada hii;
1. Guikontes E, Spantideas A, Diakakis J. Ondansetron and hyperemesis gravidarum. Lancet 1992;340:1223.
2. World MJ. Ondansetron and hyperemesis gravidarum. Lancet 1993;341:185.
3. Sullivan CA, Johnson CA, Roach H, Martin RW, Stewart DK, Morrison JC. A prospective, randomized, double-blind comparison of the serotonin antagonist ondansetron to a standardized regimen of promethazine for hyperemesis gravidarum. A preliminary investigation (abstract). Am J Obstet Gynecol 1995;172:299.
4. Sullivan CA, Johnson CA, Roach H, Martin RW, Stewart DK, Morrison JC. A pilot study of intravenous ondansetron for hyperemesis gravidarum. Am J Obstet Gynecol 1996;174:1565–8.
5. Tincello DG, Johnstone MJ. Treatment of hyperemesis gravidarum with the 5-HT 3 antagonist ondansetron (Zofran). Postgrad Med J 1996;72:688–9.
6. Einarson A, Maltepe C, Navioz Y, Kennedy D, Tan MP, Koren G. The safety of ondansetron for nausea and vomiting of pregnancy: a prospective comparative study. Br J Obstet Gynaecol 2004;111:940–3.
7. Anderka M, Mitchell AA, Louik C, Werler MM, Hernandez-Diaz S, Rasmussen SA, and the National Birth Defects Prevention Study. Medications use to treat nausea and vomiting of pregnancy and the risk of selected birth defects. Birth Defects Res (Part A) 2012;94:22–30.
8. Pasternak B, Svanstrom H, Hviid A. Ondansetron in pregnancy and risk of adverse fetal outcomes. NEJM 2013;368:814–23.
9. Koren G. Scary science: ondansetron safety in pregnancy – two opposing results from the same Danish registry. Ther Drug Monit 2014;36:1–2.
10. Andersen JT, Jimenez-Solem E, Andersen NL, et al. Ondansetron use in early pregnancy and the risk of congenital malformations—a registry based nationwide control study. International Society of Pharmaco-epidemiology. Montreal, Canada; 2013. Abstract 25, Pregnancy Session 1. As cited by Koren G. Scary science: ondansetron safety in pregnancy—two opposing results from the same Danish registry. Ther Drug Monit 2014;36:1–2.