top of page

Mwandishi:

Mhariri:

ULY CLINIC

16 Oktoba 2021 11:19:16

Sumatriptan kwa mjamzito

Sumatriptan kwa mjamzito

Sumatriptan ni dawa jamii ya serotonin (5-hydroxytryptamine 1 [5-HT]) risepta agonisti inayotumika kutibu kipanda uso kikali. Hupatikana kama kidonge au dawa ya kuchoma chini kwenye ngozi. Sumatriptan imekuwa ikitumika pia kwenye matibabu ya maumivu ya kichwa yaliyokusanyika sehemu moja ya kichwa. Dawa hii hufanana sana na almotriptan, eletriptan, frovatriptan, naratriptan, rizatriptan, na zolmitriptan.


Sumatriptan imesababisha usumu na ulemavu kwenye jamii moja ya spishi yawanyama, hata hivyo dawa hii haionekani kuwa na hatari kubwa kwa binadamu. Hakuna mlolongo wa kuelekweka kwa ulemavu uliotokea kwa wanyama kiasi cha kushindwa kutoa jumuisho kama ulemavu uliotokea unahsiana na dawa. Tafiti hiyo pia haikuweza kutambua ulemavu usio na mashiko kutokana na kukosa mpangilio wa uchunguzi wa mwili. Hata hivyo taarifa bado ni chache kuhusu matumizi ya dawa hii wakati wa ujauzito kutokana na wajawazito wachache wanaotumia dawa hii. Mapitio ya taarifa kuhusu triptan ya mwaka 2008 haikupata ushahidi kuhusianosha dawa hiina ulemavu licha ya kuonyesha kuhusiana na kujifungua kabla ya wakati.


Matumizi wakati wa ujauzito


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari ya wastani


Hakuna (zipo chache) taarifa za binadamu- taarifa za wanyama zinaonyesha kuwepo hatari ya wastani ina maaga gani?


Inawezekana kuwa hakuna taarifa za zoefu wa matumizi ya dawa hii au taarifa za binadamu wajawazito wachache waliotumia dawa hii zimeonyesha kutohusiana kuwa sumu kwa kichangawa tumboni kuweza kusababisha madhaifu ya uumbaji, ukuaji, viungo vya mwili, ufanyaji kazi wa viungo, tabia au kusababisha kifo endapo itatumika. Dawa hii ni sumu kwenye uumbaji wa kijusi( kwenye dozi ambayo haikusababisha sumu kwa mama) kwenye jamii moja mnyama aliyefanyiwa tafiti kwenye dozi ambayo ni sawa au pungufu ya mara kumi ya ile ya binadamu, dozi inayotolewa kuendana na jumla ya eneo la mwili.


Matumizi wakati wa kunyonyesha


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji


Hakuna (chache) taarifa za binadamu- Inaweze patana na unyonyeshaji ina maana gani?

Hakuna taarifa za uzoefu kuhusu matumizi ya dawa hii kwa mama anayenyonyesha au kuna taarifa chache. Taarifa chache zilizopo zinaonyesha kuwa dawa hii haiwasilishi hatari yenye mashiko kwa kichanga anayenyonya maziwa ya mama anayetumia dawa.

ONYO: Usitumie dawa yoyote bila ushauri wa daktari. Dawa zinaweza kuleta madhara mwilini na pia matumizi ya baadhi ya dawa pasipo ushauri na vipimo husababisha  vimelea kuwa sugu dhidi ya dawa hiyo.
ULY clinic inakushauri kuwasiliana na daktari wako unapotaka kuchukua maamuzi yoyote yanayohusu afya yako.
Wasiliana na daktari/Mfamasia wa ULY clinic kwa ushauri na Tiba au kuandikiwa dawa kwa kupiga simu au Kubonyeza Pata tiba chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

1 Julai 2023 16:54:09

Rejea za mada hii;

1. Soldin OP, et al. Triptans in pregnancy. Ther Drug Monit 2008;30:5–9.
2. Product information. Imitrex. GlaxoSmithKline, 2007.
3. Shepard TH. Catalog of Teratogenic Agents. 8th ed. Baltimore, MD: The Johns Hopkins University Press, 1995:397.
4. The Sumatriptan/Naratriptan/Treximet Pregnancy Registry. Interim Report. 1 January 1996 through 30 April 2009. GlaxoSmithKline, August 2009.
5. Eldridge RE, et al. Monitoring birth outcomes in the sumatriptan pregnancy registry (abstract). Teratology 1997;55:48.
6. Shuhaiber S, Pastuszak A, Schick B, Koren G. Pregnancy outcome following gestational exposure to sumatriptan (Imitrex) (abstract). Teratology 1997;55:103.
7. Shuhaiber S, et al. Pregnancy outcome following first trimester exposure to sumatriptan. Neurology 1998;51:581–3.
8. Wilton LV, et al. The outcomes of pregnancy in women exposed to newly marketed drugs in general practice in England. Br J Obstet Gynaecol 1998;105:882–9.
9. Kajantie E, et al. Bilateral cleft lip and palate, hypertelorism and hypoplastic toes. Clin Dysmorphol 2004;13:195–6.
10. Gei A, et al. The effect of sumatriptan on the uterine contractility of human myometrium (abstract). Am J Obstet Gynecol 2001;184:S193.
11. Evans EW, et al. Use of 5-HT1 agonists in pregnancy. Ann Pharmacother 2008;42:543–9.
12. Wojnar-Horton RE, et al. Distribution and excretion of sumatriptan in human milk. Br J Clin Pharmacol 1996;41:217–21.
13. Fullerton T, et al. Sumatriptan: a selective 5-hydroxytryptamine receptor agonist for the acute treatment of migraine. Ann Pharmacother 1992;26:800–8.
14. Committee on Drugs, American Academy of Pediatrics. The transfer of drugs and other chemicals into human milk. Pediatrics 2001;108:776–89.

bottom of page