Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
Alhamisi, 11 Februari 2021
Pearly penile papule
Makala hii imezungumzia kuhusu tatizo la vipele kwenye ngozi ya uume linaloitwa kwa jina tiba 'Pearly penile papules' (PPP). Soma pia kuhusu vilele vya Fordyce Spots.
Pearly penile papules ni vepele vinavyotokea kwa watu wengi duniani, vipele hivi huchukuliwa kama vipele vya kawaida wala si saratani na havina mahusiano na magonjwa ya zinaa. Sifa ya vipelevya PPP huwa ni, huwa laini vyenye umbo la kuba (wakati mwingine hufanana na chunusi ndogo), hutokea kwenye shingo ya kichwa cha uume, haivitoi usaha na huweza kuwa kwenye mistari miwili au zaidi. Vipele vya PPP hutokea wakati wa ujana au miaka ya mwanzo ya kuwa mtu mzima.
Ingawa vipele vya PPP vinafanana na vipele vingine vya magonjwa ya zinaa, PPP huwa havina mahusiano yoyote na magonjwa ya zinaa na wala havina mahusiano na saratani na wala havihitaji matibabu isipokuwa kwa watu ambao wanahofu kuhusu mwonekano wao wa maumbile.
Dalili
Vipele vya PPP huwa havileti dalili yoyote ile kwa mtu lakini huwa na mwonekano wa;
Vilele vingi vidogo vyenye umbo la kuba kwenye shingo ya uume(chini ya kichwa cha uume)
Vipele huwa kwenye mistari miwili au zaidi
Upele huweza kuwa mdono kama uzi
Hutokea sana kwa vijana wadogo na haswa wale wasiotahiliwa
Visababishi
Vipele vya PPP havisababishwi na kitu chochote kile, huchukuliwa kuwa ni aina tofauti ya maumbile ya uume. Pia ikumbukwe kuwa vipele vya PPP huwa haviambukizwi na pia havibadiliki kuwa saratani.
Vipimo
Vipimo vingi vitafanyika kutofautisha vipele hivi na magonjwa ya zinaa, endapo magonjwa ya zinaa hayapo na kipimo cha historogy kimeonyesha kuwa ni uvimbe wa kawaida, hutahitaji kuhangaika tena kupima vipimo vingine.
Matibabu
Endapo vipele vya PPP vimethibitika kwa vipimo, hakuna haja ya kupata matibabu. Unatakiwa kupata ushauri wa kisaikolojia na kujikubali kuwa ni hali ya kawaida. Endapo lakini unahitaji kuviondoa, kuna aina mbalimbali za matibabu zinaweza kutumika kuondoa vipele kama vile;
Upasuaji wa kutumia mwanga wa Carbon dioxide. Mwanga huu huyeyusha vipele hivyo.
Radiosurgery
Upasuaji wa kugandisha vipele kwa baridi kali baada ya hapo kuvikata kwa jina la Cryosurgery:
Upasuaji wa kukata vipele kwa kwa njia ya kawaida.