Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
Jumanne, 6 Aprili 2021
Saratani ya damu (leukemia)
Leukemia ni saratani ya damu inayoshambulia tishu zinazohusika kutengeneza damu ikiwa pamoja na urojo wa mifupa na mfumo wa limfatiki.
Leukemia mara nyingi huathiri chembe nyeupe za damu ambazo hupambana na maradhi mbalimbali. Kuathiriwa kwa chembe hizi hufanya mwili kushindwa kupambana na maradhi kutokana na kinga ya mwili kushuka baada ya shambulio hilo.
Vihatarishi
Vihatarishi vya saratani hii havijulikani lakini zipo sababu hatarishi zinazoweza kupelekea mtu kupata saratani hii ikiwa pamoja na:
Kupigwa na mionzi mikali: Mfano baada ya kupigwa bomu la nyuklia kule Japan,Ongezeko la wagonjwa wa saratani ya leukemia iliongezeka zaidi
Kemikali za sumu: Mfano kemikali inayoitwa Benzene ya inayotumiwa viwandani huweza kusababisha saratani hii Leukemia, uvutaji wa sigara na tumbaku humweka mtu hatarini kupata saratani ya AML
Virusi: Mfano kirusi cha Human T- Cell Lymphotropic Virus type 1-( HTLV-1) Epstein Bar Virus,pia kirusi cha UKIMWI huweza kusababisha saratani ya leukemia
Sababu za jini (vinasaba): Wanaume huathiriwa zaidi kuliko wanawake, pia watu wenye tatizo la sindromu ya Down?s huathiriwa Zaidi
Makundi ya saratani ya leukemia
Leukemia ya muda mfupi
Leukemia sugu
Leukemia ya muda mfupi
Leukemia hii inaambatana na kuongezeka zaidi kwa chembechembe za damu ambazo hazijakomaa katika damu. Chembe hizi huitwa blast. Blast hujizalisha kwa wiki sanga ana pia huwa hazina uwezo wa kufnaya majukumu yake ya kinga mwilini. Ugonjwa huhitaji kutibiwa hima ili kupambana nao
Saratani ya Leukemia ya muda mfupi pia imegawanyika kwenye makundi makuu mawili ambayo ni :
Leukemia ya muda mfupi ya Mayeloblastiki (AML)
Leukemia ya muda mfupi ya limphoblastiki (ALL)
Leukemia ya muda mfupi ya Mayeloblastiki (AML)
Leukemia ya muda mfupi ya Mayeloblastiki (AML): Hii ni aina ya saratani ambayo pana kuwepo seli nyingi za blasts kwenye damu. Seli hizi changa huwa hazina uwezo wa kufnaya kazi za kinga ya mwili. Kuwepo kwa seli hizi chanha husababisha matatizo mwilini na kuleta dalili mbalimbali.
Dalili za mgonjwa mwenye leukemia ya muda mfupi ya Mayeloblastik ni;
Kuvimba kwa ini
Kuvimba kwa Bandama
Kuvimba kwa fizi
Mwili kuchoka
Kupungua uzito
Kupata maambukizi ya magonjwa kurahisi
Matatizo ya damu kuganda
Kuishiwa damu mwilini
Leukemia ya muda mfupi ya limphoblastiki (ALL)
Leukemia ya muda mfupi ya Mayeloblastiki (AML): Hii ni aina ya saratani ambayo pana kuwepo seli nyingi za blasts kwenye damu. Seli hizi changa huwa hazina uwezo wa kufnaya kazi za kinga ya mwili. Kuwepo kwa seli hizi chanha husababisha matatizo mwilini na kuleta dalili mbalimbali.
Dalili za mgonjwa mwenye leukemia ya muda mfupi ya Mayeloblastik
Kuvimba kwa ini
Kuvimba kwa Bandama
Kuvimba kwa fizi
Mwili kuchoka
Kupungua uzito
Kupata maambukizi ya magonjwa kurahisi
Matatizo ya damu kuganda
Kuishiwa damu mwilini
Leukemia ya muda mfupi ya limfoblastiki (ALL)
Hii ni aina ya saratani ya damu ambayo damu inakuwa seli za limfoblasti kwa wingi kwenye damu kulinganisha na aina zingine za saratani.
Kuwepo kwa seli nyingi za limfoblasti hupunguza nafasi ya seli zingine za damu, hivyo mtu anakuwa na upungufu wa seli zingine za damu.
Dalili za mgonjwa mwenye leukemia ya muda mfupi ya limfoblastiki Leukemia
Maumivu ya misuli
Maumivu ya mifupa
Maumivu ya kichwa
Kuvimbwa kwa tezi za limfu
Kuvimba kwa korodani
Uvimbe kwenye mediastina
Kuvimba kwa ini
Kuvimba kwa bandama
Leukemia sugu
Sifa ya saratani hii ni kwamba chembe nyeupe za damu zinazozalishwa, nyingi huwa zimekomaa na zinaweza kufanya baadhi ya majukumu yake ya kinga mwilini. TSaratani hili hutokea taratibu sana na dalili zinaweza zisitambulike kwa haraka mpaka baada ya miaka kadhaa.
Leukemia sugu imegawanyika kwenye makundi makuu mawili:
Leukemia sugu ya myeloid (CML)
Leukemia sugu ya limfositiki (CLL)
Leukemia sugu ya myeloid (CML)
Hii ni aina ya saratani yenye sifa za utengenezwaji na uzalishwaji kwa wingi wa seli za myeloid, hali hii hupelekea kuvimba kwa bandama na kuwa na kiasi kikubwa cha chembe nyeupe za damu.
Asilimia 95 ya wagonjwa wa CML huwa na vinasaba visivyo vya kawaida na asilimia 25 ya wagonjwa huwa hawaonyeshi dalili zozote zile
Dalili za mgonjwa mwenye Leukemia sugu ya myeloid (CML)
Kuchoka sana kwa mwili kusiko na sababu
Kupungua uzito bila sababu
Kupata shida kupumua
Maumivu ya tumbo
Kukosa hamu ya kula
Kutokwa na jasho kwa wingi
Tumbo kujaa
Kupata michubuko kirahisi ya ngozi
Ini kuvimba
Bandama kuvimba
Saratani sugu ya limphositiki leukemia (CLL)
Saratani hii hutokea hasa kwa wagonjwa kati ya umri wa miaka 65 hadi 70 . Aina hii saratani hutokea kwa mwili kushindwa kukuthibiti ukuaji wa seli za B Limphosaiti hivyo hupelekea kinga ya mwili kushuka na utengenezwaji wa seli yeupe za damu kuwa mdogo.
Dalili
Dalili ya mgonjwa mwenye leukemia sugu ya limphositiki ni kama zifuatavyo:
Kupata maambukizi mara kwa mara na kwa urahisi kama vile homa ya mapafu- nimonia
Kushiba mapema kutokana na bandama kuwa kubwa
Kutokwa na damu kirahisi au kuumia kirahisi
Kuvilia kwa damu chini ya ngozi na hivyo kuleta madoa mekundu ya patekio
Mwili kuchoka sana
Homa za mara kwa mara
Jasho nyakati za usiku
Kupungua uzito
Matibabu
Kuna aina mbalimbali za matibabu ya saratani ya leukemia ambayo ni pamoja na;
Tiba ya dawa za Kemotherapi- kemotherapi ni msingi mkubwa wa matibabu ya saratani ya leukemia. Dawa hizi ni kemikali zinazotumika kuua chembe za saratani. Mfano wa dawa ni Vincristine, Methotrexate na Cyclophosphamide.
Kwa kutegemea aina ya saratani unaweza kutumia dozi moja au dozi yenye mchanganyiko wa dawa. Dawa hizi zinaweza kuwa kwenye mfumo wa tembe au dawa za maji kwa ajili ya kuchomwa kwenye mishipa ya damu.
Tiba baiologia
Tiba hii huamuru chembe za ulinzi wa mwili kupambana na chembe za saratani.
Tiba elekezi
Tiba hii hutumia dawa zinazoenda kuvamia hatua Fulani ya uzalishaji wa chembe za saratani. Mfano wa dawa ni imatinib.
Tiba mionzi
Mionzi ya Xray hutumika kuharibu chembe ambazo ni saratani na kusimamisha kuzaliana.
Kupandikizwa tishu za stem
Tishu za stem ni tishu za urojo wa mifupa, daktari atakufanyia atakuweka tishu mpya kwenye mifupa yako ili zizalishe chembechembe nyeupe za damu zisizo na saratani.
Kabla ya kuwekewa tishu za stem, utakuwa kwenye dozi kali ya kemotherapi au mionzi ili kuua chembe zinazozalisha saratani. Utawekewa kwenye mifupa yako tishu za stem kutoka kwako mwenyewe au kwa mtu mwingine.