top of page

Mwandishi:

Mhhariri

ULY CLINIC

Dkt. Sospeter M, MD

Jumatatu, 14 Juni 2021

Thalasimia

Thalasimia

Thalasimia (thalassemia) ni ugonjwa wa damu wa kurithi unaosababisha uzalishaji wa kiwango kidogo kuliko kawaida cha himoglobin. Himoglobin hufanya kazi muhimu ya kubeba oksijeni kwenye damu na kupeleka kwenye seli ambapo huwa na kazi muhimuya kufanya ziweze kuishi na kutengeneza nguvu, mgonjwa mwenye upungufu wa himoglobin hupata dalili za kuchoka sana na kuishiwa pumzi ambazo ni dalili za upungufu wa damu.


Endapo una thalasimia, si lazima kupata matibabu kama dalili ni za wastani, isipokuwa unapopata dalili kali, utahitaji kuwa unaongezewa damu.


Thalasimia husabaishwa na nini?


Thalasimia husababishwa na mabadiliko ya jeni ya seli zinazotegeneza himoglobin. Mabadiliko haya husafilishwa kutoka kwa wazazi kwenda kwa mtoto.


Himoglobin imeundwa na mikufu miwili alpha na beta inayoweza kuathiriwa na mabadiliko ya jeni. Uzalishaji wa mikufu ya hemoglobin alfa na beta hupungua na kupelekea kupata thalasimia alfa au beta kwa wagonjwa wenye mabadiliko katika jeni za hemoglobin.


Dalili za thalassemia huanza kuonekana wakati gani?


Kwa kuwa thalasimia ni ugonjwa wa kurithi, baadhi ya watoto huanza kuonyesha dalili wakiwa tumboni, mara baada ya kuzaliwa na wengine ndani ya miaka miwili ya kwanza. Watoto ambaye jeni moja tu ndo ina tatizo,hata onyesha dalili yoyote.


Dalili za thalasimia


Dalili za thalasimia hutegemea aina ya thalasimia, idadi ya jeni zenye mapungufu zilizorithiwa na aina ya himoglobin zilizoathiriwa. Dalili kwa ujumla zinazoonekana ni za upungufu wa damu ambazo zipo kwenye makundi yafuatayo;


Dalili za thalasimia kutokanana upungufu wa damu

 • Upungufu kiasi wa damu

 • Upungufu wastani wa damu

 • Upungufu mkali wa damu


Dalili za thalasimia kutokana na aina ya thalasemia

 • Dalili za thalasimia alfa

 • Dalili za thalasimia beta


Kwa maelezo zaidi, soma vipengele vinavyofuata


Upungufu kiasi wa damu


 • Watu waliobeba jeni moja ya thalasimia alfa au beta, hupata dalili kiasi au kutopata dalili kabisa za ugonjwa. Unaweza kupata dalili ya uchovu na mara nyingi huweza kuchanganywa na upungufu wa damu wa madini chuma.

 • Upungufu wa kiasi hadi wastani wa damu


Dalili


 • Ukuaji wa taratibu na kuchelewa barehe

 • Madhaifu ya mifupa ya uso na kuvunjika kirahisi kwa mifupa

 • Kuvimba kwa bandama

 • Upungufu mkali wa damu

 • Dalili zake hutokea ndani ya miaka miwili ya maisha ambazo ni

 • Kuishiwa damu mara kwa mara

 • Kukosa hamu ya kula

 • Kupauka kwa ngozi

 • Uchovu mkali

 • Kukojoa mkojo uliopauka

 • Kuchelewa kukua na kubarehe

 • Njano kwenye macho na ngozi

 • Kutanuka kwa moyo, ini na bandama

 • Madhaifu ya mifupa haswa ya uso


Dalili za thalasimia alfa


Jeni nne zinahusika kutengeneza mikufu ya himoglobin alfa, unarithi jeni mbili kutoka kwa kila mzazi.

Kurithi jeni moja yenye shida, husababisha kutoonekana kwa dalili yoyote ya ugonjwa wa thalasimia, hata hivyo unauwezo wa kusafirisha jeni yenye shida kwa mtoto wako.


Ukirithi jeni mbili zenye shida


Utapata dalili za wastani na utaitwa mbeba jeni ya thalasimia


Ukirithi jeni tatu zenye shida- dalili zitakuwa za wastani na kali


Endapo mtoto amerithi jeni nne za thalasimia alfa mara nyingi hufia tumboni au muda mfupi baada ya kuzaliwa au atahitaji kuwa anaongezewa damu maisha yake yote na mara chache sana kupandikizwa shina jipya la rojo ya mifupa ili kuweza kuzalisha chembe za damu zisizo na tatizo.


Dalili za thalasimiabeta

Kuna jeni mbili ambazo zinahusika kutengeneza mikufu ya hemoblobin beta, unarithi jeni moja kutoka kwa kila mzazi.


Ukirithi jeni moja ya beta himoglobin, utapata dailili za wastani. Thalasimia aina hii hufahamika kwa jina jingine la thalasimia ndogo au thalasimia beta


Ukirithi jeni mbili zenye shida kutoka kwa wazazi, dalili za wastani na kali hutokea. Thalasimia aina hii hufahamika pia kwa jina jingine la thalasimia kubwa au upungufu wa damu wa Cooley


Vihatarishi


Kwa sababu thalasimia ni ugonjwa ni wa kurithi, vifuatavyo huwa vihatarishi vya kupata ugonjwa wa thalasimia.


Kuwa na historia ya ugonjwa wa thalasimia kwenye familia au ukoo

Kuwa na asili ya Bara la Afrika/ Amerika, Mediterania na kusini mashariki mwa bara la Ulaya


Madhara


Madhara ya thalasimia ni;


 • Kuzidi kiwango cha madini chuma

 • Maambukizi

 • Madhaifu ya mifupa

 • Kuvimba bandama

 • Ukuaji duni

 • Matatizo ya moyo


Kuzidi kiwango cha madini chuma

Mara nyingi husababishwa na ugonjwa au kuongezewa damu mara kwa mara. Kuzidi huko huambatana na uharibu moyo, ini na mfumo wa homoni mwilini.


Maambukizi ya mara kwa mara

Wagonjwa wa thalasimia huwa na hatari ya kupata maambukizi ya mara kwa mara, haswa endapo wamefanyiwa upasuaji wa kutoa bandama.


Mifupa kuwa dhaifu

Thalasimia husababisha kutanuka kwa rojo ya mifupa ili kuongeza uzalishaji wa himoglobin, hii hupelekea kupanuka kwa mifupa na kuleta mwonekano wan je wa umbile lisilo la kawaida katika mifupa ya uso, uso na udhaifu wa mifupa inayopelekea kuvunjika kirahisi.


Kuvimba bandama na matatizo ya moyo

Bandama hufanya kazi ya kuchuja chembe za damu zenye matatizo kisha kuziharibu na pia kazi nyingine ya muhimu ni kuzalisha kinga ya mwili dhidi ya baadhi ya maradhi kwa ajina la antibodi.


Bandama likifanya kazi za kuharibu hemoglobin zenye shida kwa muda mrefu, hupelekea kuvimba na kuleta mwonekano wa nje wa tumbo kubwa . Kuvimba kwa bandama huongeza hatari ya kupata upungufu wa damu kwa sababu huongeza uharibifu wa chembe nyekundu za damu hata ulizoongezewa.


Unaweza kushauriwa na daktari kufanya upasuaji wa kuondoa bandama endapo unapata dalili za kuishiwa damu mara kwa mara na umevimba bandama.


Matatizo ya moyo

Kwa sababu ya upungufu wa damu, watoto wenye thalasimia huwa na hatari ya kupata mapigo yasiyo kawaida na kuferi moyo.


Ukuaji duni na kuchelewa barehe

Kwa sababu ya upungufu wa damu, mtoto atakuwa taratibu na kuchelewa pata barehe


Kinga


Mara nyingi ni vigumu kuzuia kupata ugonjwa wa thalasimia haswa endapo umeoana na mtu bila kupima vinasaba. Endapo una jeni za thalasimi au wewe na mpenzi wako wote mna historia ya thalasimia kwenye ukoo unashauriwa kuonana na daktari wa jeni kwa ushauri wa nini cha kufanya.


Hata hivyo pia, unaweza kutumia njia zingine za uzazi kama vle kuchavusha yai nje ya kizazi kisha kupandikizwa kwa kijusi ambaye hana shida ya thalasimia kwenye mji wako wa mimba ili kukua kama kawaida. Tekinolojia hii inapatikana kwenye baadhi ya nchi.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kitiba baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata Tiba,  au ''mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

26 Oktoba 2021 21:04:28

Rejea za mada hii:

1.Jameson JL, et al., eds. Disorders of hemoglobin. Harrison's Principles of Internal Medicine. 20th ed. The McGraw-Hill Companies; 2018. https://accessmedicine.mhmedical.com. Imechukuliwa 14.06.2021

2.National Heart, Lung, and Blood Institute. Thalassemias. https://www.nhlbi.nih.gov/health-topics/thalassemias. Imechukuliwa 14.06.2021

3.Benz EJ. Clinical manifestations and diagnosis of the thalassemia. https://www.uptodate.com/contents/search. Imechukuliwa 14.06.2021

4.Centers for Disease Control. A guide to living with thalassemia. https://www.cdc.gov/ncbddd/thalassemia/living.html. Imechukuliwa 14.06.2021

5.What is Thalassemia?. https://www.cdc.gov/ncbddd/thalassemia/facts.html. Imechukuliwa 14.06.2021

6.NIH. Thalassemia. https://www.nhlbi.nih.gov/health-topics/thalassemias. Imechukuliwa 14.06.2021

bottom of page