Mwandishi:
Mhhariri
ULY CLINIC
Dkt. Mangwella S, MD
Alhamisi, 11 Februari 2021

Vipele vya Fordyce spots kwenye uume
Fordyce spots ni vipele vidogo vyenye rangi ya njano au nyeupe vinavyotokea kwenye kichwa au mpini wa uume, baadhi ya vipele hutokea kwenye maeneo kati ya mstari wa mpini na uume. Vipele hivi huwa havina sifa ya kuwa kwenye mstari kama vipele vya Pearly penile papules (PPP), huweza tokea kama kipele kimoja au vingi zaidi.
Vipele vya Fordyce spots hutokana tezi zya mafuta ya ngozi ya ‘sebaceous’ tezi ambayo haina vinyweleo.
Vipele hivi vinaweza tokea ndani ya mashavu ya mdomo, kwenye midomo na hutokea sana kwa watu wazima
Vipele vya tezi Tyson kwenye uume
Tezi tyson ni aina ya tezi zinazozalisha mafuta kwenye ngozi zenye jina la sebaceous zilizohama maeneo yake asilia na hutokea kama jozi kwenye shingo ya uume. Kazi ya tezi hizi ni kutoa mafuta yayaofanya uume uteleze kwenye uke. Vipele hivi vinaweza tokea pande mbili yaani kushoto na kulia lakini huwa havifananani na vipele vya 'Fordyce spots' au Pearly penile papules (PPP).
Vipele hivi ni sehemu ya maumbile ya kawaida na hivyo havihitaji matibabu. Endapo utahitaji matibabu kwa sababu za kisaikolojia, matibabu yatahusisha;
Upasuaji wa kutumia mwanga wa Carbon dioxide. Mwanga huu huyeyusha vipele hivyo.
Upasuaji wa mionzi
Upasuaji wa kugandisha vipele kwa baridi kali baada ya hapo kuvikata kwa jina la Cryosurgery:
Upasuaji wa kukata vipele kwa kwa njia ya kawaida.
Angalia picha kwa uelewa zaidi wa mwonekano wa vipele hivi.