top of page

Mwandishi:

Mhhariri

ULY CLINIC

Dkt. Mangwella S, MD

Alhamisi, 11 Februari 2021

Vipele vya tezi Tyson kwenye uume

Vipele vya tezi Tyson kwenye uume

Tezi tyson ni aina ya tezi za mafuta ya mafuta ya ngozi yenye jina la sebaceous zilizohama maeneo yake asilia na hutokea kama jozi kwenye shingo ya uume. Kazi ya tezi hizi ni kutoa mafuta yayaofanya uume uteleze kwenye uke. Vipele hivi vinaweza tokea pande mbili yaani kushoto na kulia lakini huwa havifananani na vipele vya 'Fordyce spots' au Pearly penile papules (PPP). Vipele hivi huwa ni maumbile ya kawaida na havihitaji matibabu. Endapo utahitaji matibabu kwa sababu za kisaikolojia, matibabu yatahusisha;


  • Upasuaji wa kutumia mwanga wa Carbon dioxide. Mwanga huu huyeyusha vipele hivyo.

  • Upasuaji wa mionzi

  • Upasuaji wa kugandisha vipele kwa baridi kali baada ya hapo kuvikata kwa jina la Cryosurgery:

  • Upasuaji wa kukata vipele kwa kwa njia ya kawaida.


Soma zaidi kuhusu vipele vya 'Fordyce spots' au ?Pearly penile papules?(PPP) kwenye makala zingine ndani ay tovuti hii.


Angalia picha kwa uelewa zaidi wa mwonekano wa vipele hivi.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kitiba baada ya kusoma makala hii.

Wasiliana na daktari wa ulyclinic kwa ushauri zaidi na tiba kwa kubofya 'Pata Tiba,  au ''mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii

Imeboreshwa,

26 Oktoba 2021 21:04:20

Rejea za mada hii:

bottom of page