Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
ULY CLINIC
19 Mei 2025, 20:07:16

Mambo ya kufanya endapo hushiki mimba
Swali la msingi
Mimi ni mwanamke mwenye miaka 27, ni mwaka wangu wa 12 sasa tangu nipo kwenye ndoa lakini sijabahatika kupata mtoto, nifanyaje ili nipate mtoto kitaalamu?
Majibu
Asante kwa swali lako muhimu. Kama umeishi kwenye ndoa kwa zaidi ya mwaka mmoja ukijamiiana bila kutumia njia za uzazi wa mpango na hujapata ujauzito, hali hii kitaalamu huitwa utasa. Kwa kuwa ni miaka 12 sasa bila kupata mtoto, unahitaji tathmini ya kina ya kitabibu wewe na mwenzi wako ili kubaini chanzo na kupata matibabu sahihi.
Hatua za kitaalamu unazopaswa kuchukua ili kusaidiwa kupata mtoto
1. Muone daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi
Atachukua historia ya afya yako na ya mwenzi wako, na kupanga vipimo muhimu.
2. Kufanya vipimo
Vipimo vya mwanamke vinaweza kujumuisha
Ultrasound ya nyonga inayopitia ukeni: Kuchunguza ovari, mji wa mimba (kizazi), mirija ya uzazi.
Kipimo cha kuchunguza mirija ya uzazi (HSG): Kupima kama mirija ya uzazi imeziba au iko wazi.
Kipimo cha homoni: Kupima homoni kama:
FSH (Follicle Stimulating Hormone)
LH (Luteinizing Hormone)
Prolactin
Estradiol
TSH (kwa tezi)
Kipimo cha uovuleshaji: Kuangalia kama yai linatoka kila mwezi.
Vipimo vya mwanaume vinaweza kujumuisha
Kipimo cha mbegu za kiume: Kuchunguza idadi, kasi, na maumbo ya mbegu za kiume.
Ikiwa kuna matatizo, wanaume hupewa matibabu au ushauri wa kitalaamu.
4. Tiba kutegemea kisababishi
Ikiwa tatizo ni la homoni: dawa kama clomiphene citrate au letrozole husaidia kuchochea uzalishaji wa mayai.
Ikiwa kuna matatizo ya mirija au mfuko wa mimba: upasuaji mdogo unaweza kusaidia.
Ikiwa mbegu ni chache au dhaifu: tiba kama kuingiza mbegu moja kwa moja kwenye mfuko wa kizazi au kuchavushwa yai nje ya mji wa mimba inaweza kupendekezwa.
Ikiwa hakuna tatizo lililogundulika: inaweza kuwa ni ugumba usioelezeka (usio na sababu) na matibabu kama kuchavusha yai nje ya mji wa mimba yanaweza kusaidia.
5. Fuatilia mzunguko wako
Tumia kalenda ya hedhi au app ya uzazi kufuatilia siku zako za rutuba. Ushiriki tendo la ndoa karibu na siku za uovuleshaji.
Usikate tamaa
Kuna wanawake waliopata watoto baada ya miaka mingi ya kusubiri wakitumia njia za kitaalamu. Hakikisha unapata msaada kutoka kwa daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi
Nini kingine cha kufahamu
Unapokwenda kwa daktari, hakikisha una majibu ya maswali yaliyo katika dodoso la kutoshika mimba. Bofya linki kusoma maswali.
ULY CLINIC inakushauri uwasiliane na daktari wako kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatua yoyote ile baada ya kusoma majibu haya.
Kupata ushauri zaidi au tiba kutoka kwa daktari wa ULY CLINIC bofya hapa au tumia linki ya Pata tiba
Imeboreshwa,
19 Mei 2025, 20:07:16
Rejea za mada hii
World Health Organization. Infertility definitions and terminology [Internet]. Geneva: WHO; 2020 [cited 2025 May 19]. Available from: https://www.who.int/news-room/fact-sheets/detail/infertility
Zegers-Hochschild F, Adamson GD, Dyer S, Racowsky C, de Mouzon J, Sokol R, et al. The International Glossary on Infertility and Fertility Care, 2017. Fertil Steril. 2017;108(3):393–406.
Practice Committee of the American Society for Reproductive Medicine. Diagnostic evaluation of the infertile female: a committee opinion. Fertil Steril. 2015;103(6):e44–50.
Agarwal A, Mulgund A, Hamada A, Chyatte MR. A unique view on male infertility around the globe. Reprod Biol Endocrinol. 2015;13:37.
National Institute for Health and Care Excellence (NICE). Fertility problems: assessment and treatment. Clinical guideline [CG156]. London: NICE; 2013. Available from: https://www.nice.org.uk/guidance/cg156
Fritz MA, Speroff L. Clinical Gynecologic Endocrinology and Infertility. 8th ed. Philadelphia: Lippincott Williams & Wilkins; 2011.
Fauser BC, Tarlatzis BC, Rebar RW, Legro RS, Balen AH, Lobo R, et al. Consensus on women's health aspects of polycystic ovary syndrome (PCOS): the Amsterdam ESHRE/ASRM-Sponsored 3rd PCOS Consensus Workshop Group. Fertil Steril. 2012;97(1):28–38.e25.