top of page

Imeandikwa na daktari wa ULY clinic

Maumivu ya Korodani na pumbu

Maumivu ya korodani (pumbu) ni maumivu yanayoweza kutokea kwenye korodani moja au zote mbili, maumivu hayo chanzo chake kinaweza kuwa ni kwenye korodani, au sehemu nyingine  mwilini.

 

Visababishi

Kuna hali na magonjwa mbalimbali yanayoweza kusababisha maumivu ya korodani, majeraha madogo pia yanaweza kuambatana na aumivu makali kutokana na korodani kuwa na mishipa mingi ya fahamu inayoongeza hisia za maumivu.

Wakati gani uhofu na kumwona daktari haraka?

Unahitaji kumwona daktari endapo maumivu yanaambatana na kichefuchefu, homa, kutapika na damu kwenye mkojo- hii humaanisha mawe kwenye figo au maambukizi kwenye mfumo wa juu wa mkojo au maumivu ni makali sana na ya ghafla- hii humaanisha pumbu zimejisokota na zinakosa damu. Ukichelewa utapoteza pumbu yako(zako) na pumbu hiyo haitaweza kuzalisha mbegu tena. Kujisokota kwa pumbu kunaweza kutokea kwenye pumbu moja au zote na kweney umri wowote ule, hata hivyo hutokea sana kwa vijana wadogo.

Endapo maumivu ni ya muda mrefu na yanaambatana na uvimbe maeneo ya pumbu, panga kuonana na daktari wako kwa tiba.

 

Visababishi

 

Hali na magonjwa yanayoweza kusababisha maumivu ya korodani  huweza kuanzia kwenye maeneo ya kinena, tumboni au sehemu nyingine yoyote ile mfano kwenye kuwa na mawe kwenye figo, kuwa na ngiri. Hata hivyo visababishi sio siku zote vinaweza kufahamika.

Hapa chini vimeorodheshwa baadhi ya visababishi vinavyojulikana kuleta maumivu ya korodani;

 • Dayabetiki nyuropathi(kwa wagonjwa wa kisukari)

 • Epididimaitizi

 • Haidrosili(busha)

 • Maumivu yasiyofahamika kisababishi

 • Henia maeneo ya kinena

 • Mawe kwenye figo

 • Ugonjwa wa mumps

 • Ochaitizi

 • Maambukizi kwenye tezi dume

 • Uvimbe kwenyepumbu

 • Spematosili

 • Kupigwa au kuumizwa kwenye pumbu

 • Kujisokota kwa pumbu

 • Maambukizi ya UTI

 • Varikosili

 

Matibabu ya nyumbani

 • Fanya mambo yafuatayo ili kupunguza maumivu ya pumbu/korodani

 • Kunywa dawa za kupunguza maumivukama vile aspirini, ibuprofen au parasetamo isipokuwa kama daktari wako amekupa maelekezo mengine. Aspirini haitakiwi kutumika kwa watoto chini ya umri wamiaka mitatu, watoto wanaopona kutoka kwenye homa ya tetekuwanga aumafua hawatakiwi kutumia dawa hii.

 • Tumia kitu chochote kuifanya korodani iwe juu wakati unalala chini

 

Vipimo

 

Vipimo hufaanyika ili kuthibitisha tatizo ambalo daktari atakuwa ameliona, wakati mwingine si lazima vipimo kufanyika kwa sababu kuna matatizo ambayo daktari atayatambua kutoka kwenye uchunguzi wa awali wa mwili na historia ya tatizo lako. Baadhi ya vipimo ambavyo unaweza fanyiwa ni;

 

 • Urinalysis  na culture kwa wagonjwa wote

 • Kipimo cha magonjwa ya zinaa( endapo unatokwana usaha, au kuwa positive kwenye kipimo cha urinalysis au kuwa na maumivu wakati wa kukojoa)

 • Ultrasound ili kujiridhisha kwamba pumbu hazijajisokota kama kuna utata

 • Vipimo vingine vinavyotokana na visababishi alivyoona daktari

Kumbuka endapo vipimo vimekuja vya kawaida, chanzo cha maumivu kinaweza kuwa sehemu nyingine ya mwili.

 

Matibabu

Matibabu huelekezwakwenyekisababishi alichokitambua daktari wako, huweza kuwa matibabu ya dharura kama upasuaji kama shida ni kujisokota kwa pumbu au kupata mapumziko kitandani.

Dawa za maumivu kama morphine na dawa zingine jamii ya opioid hutumika kupunguza maumivu ya ghafla na makali. Dawa za antibayotiki pia hushauriwa endapo kisababishi ni epididimaitizi au ochaitizi inayosababishwa na bakteria


 

ULY Clinic inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako endao umeona kuwa unadalili au tatizo kutokana na kusoma makala hii

Wasiliana na daktari wa ULY Clinic kwa ushauri zaidi na Tiba kupitia namba za simu au kubonyeza kitufe cha Pata Tiba chini ya tovuti hii. Au bonyeza hapa

Imeboreshwa mara ya mwisho 27.06.2020

Rejea za mada hii

 1. Eyre RC. Evaluation of acute scrotal pain in adults. https://www.uptodate.com/contents/acute-scrotal-pain-in-adults. Imechukuliwa 27.06.2020

 2. PUBMED. Scrotal pain. https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/6726967/. Imechukuliwa 27.06.2020

 3. Scrotal pain. Uptodate. https://www.uptodate.com/contents/causes-of-painless-scrotal-swelling-in-children-and-adolescents. Imechukuliwa 27.06.2020

 4. Scrotal pain. Merck Manual Professional Version. https://www.merckmanuals.com/professional/genitourinary-disorders/symptoms-of-genitourinary-disorders/scrotal-pain. Imechukuliwa 27.06.2020

bottom of page