top of page

Kuna umuhimu wa kupima afya mara kwa mara?

Updated: Nov 6, 2021


Ni mara ngapi unatakiwa kucheki afya yako katika mwaka hata kama haumwi?


Kumekuwa na usemi kwamba kila mara unabidi ucheki afya yako ili kujizuia na magonjwa yanayoweza kutokea na kudhoofisha afya yako. Kupima afya ya mwili mzima mara kwa mara kumekuwa kukiambatana na kutambua baadhi ya magonjwa mapema zaidi na kuyapatia tiba.


Hata hivyo tafiti za afya nyingi zinaonyesha kuwa tabia ya mtu kupima afya yake mara kwa mara au kila baada ya mwaka hata kama haumwi, huwa haina manufaa sana ukilinganisha na mtu anayepima tu mara mwili wake unapokuwa unajihisi vibaya.

Jambo la msimgi ambalo linatakiwa kufanyika na limeonyesha kuwa na umuhimu zaidi katika kuzuia magonjwa, ni kuwa na daktari wa familia. Daktari huyu hujua historia nzima ya wana familia na hivyo ni rahisi kujua nini kina shida kwenye familia wakati husika.


Vipimo vya kila baada ya mwaka kwa kupita havina umuhimu kiafya na vinaweza kukufanya uumwe zaidi

Watu wenye afya njema wanatakiwa kupata vipimo endapo tu wanavihatarishi vya kupata magonjwa au shida fulani na wanaosemekana kuwa wana vihatarishi vya magonjwa fulani. Isipokuwa hivyo majibu ya baadhi ya vipimo yanaweza kumpa hofu mtu na kumfanya aumwe zaidi kwa kuwa na hofu. Hakuna mtaalamu asiyejua kwamba baadhi ya vipimo huwa vinaonekana kuwa havipo kawaida na hivyo kutafsiriwa kama vinavyoonekana, na kumsababisha mtu kuanza kupata matibabu yasiyopaswa au kufanyiwa vipimo zaidi mara kwa mara pasipo kuwa na ugonjwa ndani ya mwili. Mfano mtu anaweza kuanza kufanyiwa vipimo vya moyo, vipimo vya mionzi na hivi vipimo huwa na madhara kwa mtu kisaikolojia na madhara kutokana na kufanyiwa kipimo husika.


Nini cha kufanya sasa?

Hakikisha una daktari wa familia ambaye anafahamu afya yako vizuri na mtumie huyo kuomba ushauri wakati gani unatakiwa kupima kipimo na kwanini ufanye kipimo hiki, ikiwezekana uliza madhara yatakayotokea kama usipopima. Kuwa na daktari wako kutasaidia sana kupata matibabu mara utakapokuwa na shida na kuna punguza gharama za wasiwasi na kupata majibu ya kuwa una ugonjwa wakati hauna kabisa.


Mtu mzima anahitaji kupima afya yake wakati gani?

 • Unahitaji kupima afya yako endapo una hali zifuatazo

 • Ukiwa unaumwa

 • Ukiwa na dalili zinazoashiria unaumwa au unaelekea kuumwa

 • Kutibu magonjwa sugu mfano magonjwa ya figo moyo n.k

 • Kutambua utendaki kazi wa dawa mpya ulizopewa

 • Kusaidia kujua madhara ya vihatarishi vya kupata magonjwa kwa wanaovuta sigara au watu wanene kupita kiasi(BMI zaidi ya 30)

 • Endapo una ujauzito

 • Kama unamahitaji binafsi mfano kupanga uzazi n.k

 • Kwa ajili ya sababu binafsi mfano umeombwa kujaza medical form n.k

Je vipi kuhusu kucheki afya kwa ajili ya kujikinga na magonjwa mbalimbali?

Kujikinga na maradhi yanayo fahamika kutokea nijambo la muhimu kufanyika

Kila mtu anatakiwa kupata chanjo zilizo shauriwa ili kujikinga na magonjwa mbalimbali pia kufanya vipimo vinavyo shauriwa kufanyika ili kuangalia kama ana shida inayoweza kutokea mfano saratani ya shingoya kizazi n.k

Vipimo gani ni muhimu sana kufanyika?

 • Shinikizo la juu la damu

 • Saratani ya shingo ya kizazi

 • Kiwango cha rehamu kwenye damu(cholesterol)

 • Kisukari

 • Saratani ya titi

 • Saratani ya utumbo

 • Kudhoofika kwa mifupa

 • Kuvimba kwa mishipa mikubwa ya damu ya tumboni

 • Maambukizi ya virusi vya ukimwi

 • Afya ya tezi dume

Ukiwa na daktari wa familia anayejua afya yako vema atakupa ushauri wakati gani wa kufanya vipimo hivyo na kila baada yam da gani. Baadhi ya vipimo unavyoweza kufanya mwenyewe ukiwa nyumbani ni pamoja na kipimo cha BMI, kipimo cha shinikizo la damu. N.k hata hivyo daktari wako atakuwa na kazi ya kukufanyia vipimo hivi huna haja ya kuhangaika.


Soma kuhusu mazoezi na je mwili wako upo imara kiasi gani katika tovuti yetu ili ujifunze zaidi.


Usisahau kuwashirikisha watu uwapendao kupakua app ya ULY CLINIC

Karibu ULY CLINIC kwa tiba na ushauri.

543 views0 comments

Recent Posts

See All

Comments


bottom of page