top of page

Namna sahihi ya kuvaa kondomu| ULY CLINIC

Watu wengi wamekuwa wakiuliza maswali yafuatayo kwenye email kupitia tovuti hii;

 • Je kondomu inavaliwaje?

 • Kondomu ina uwezo wa kukinga magonjwa gani ya zinaa?

 • Kondomu inauwezo wa kukinga maambukizi ya UKIMWI?

Makala hii ni mahususi kujibu maswali hayo na kutoa maelezo zaidi kuhusu kondomu


Kondomu ni nini?


Kondomu ni kifaa kinachovaliwa kwenye uume wakati wa ngono, ili kuzuia shahawa zisiingie ukeni na pia kukinga mambukizi ya magonjwa ya zinaa. Kondomu imeanza kutumika miaka ya 1920.


Kuna aina mbalimbali za kondomu zinazofahamika ambzazo ni kondomu ya kike na kiume, na aina ya kondomu kutokana na kampaundi. Aina za kondomu kutokana na nini kimetengeneza kondomu ni Kondomu ya latex, Kondomu ya polyurethane na Kondomu ya Polyisoprene, kondomu ya raba na kondomu ya utumbo wa kondoo.


Aina za kondomu zinazofahamika sana ni;

 • Kondomu ya latex

 • Kondomu ya polyurethane

 • Kondomu ya Polyisoprene

Kwenye tafiti zilizofanywa na wanasayansi zinaonyesha kuwa kondomu ya latex ina uwezo mkubwa wa kukinga maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na UKIMWI endapo itatumika kwa usahihi. Hata hivyo, kondomu ya polyurethane au polyisoprene inaweza kutumika kama mbadala wa watuw enye aleji(mzio) na kondomu ya latex.


Umuhimu wa kondomu


Kondomu inauwezo wa kukulinda na maradhi yafuatayo endapo itatumiwa ipasavyo;


Je kondomu inauwezo wa kukukinga kwa asilimia 100 magonjwa ya zinaa na ukimwi?


Jibu rahisi ni HAPANA


Licha ya kondomu kuwa na uwezo wa kukukinga na magonjwa ya zinaa, tafiti zinaonyesha kuwa haziwezi kukukinga kwa asilimia 100. Hii inaweza kuchangiwa na mambo mbalimbali ikiwa pamoja na matumizi yasiyo sahihi au kutotumia mara zote. Unashauriwa kufahamu namna sahihi ya kutumia kondomu ili kupata ulinzi wake mkubwa.


Virusi vya UKIMWI havizuiliki kwa asilimia 100 kwa kutumia kondomu, endapo hufahamu matumizi sahihi ya kondomu, tumia dawa za kinga dhidi ya maambukizi kama PrEP kwa usalama zaidi.


Zingatia njia zingine pia za kujikinga na maambukizi ikiwa pamoja na kuacha kufanya ngono au kuwa na mpenzi mwaminifu aliyepima magonjwa ya zinaa pamoja na UKIMWI.


Namna sahihi ya kuvaa kondomu


 • Tumia kondomu mpya kwa kila tendo moja la ngono ya uke kwa uume, ume kwa midomo, ume kwa njia ya haja kubwa.

 • Unapovaa kondomu, fungua kwa umakini katika mstari uliochorwa kuonyesha sehemu ya kufungulia kisha itoe kwa vidole. Usitumie kucha kutoa kwani inaweza kutoboa kondomu

 • Shika kondomu yako kwenye ncha (kama kwenye picha kushoto) na kisha weka kwenye kilele cha uume uliosimama, sehemu ya mkunjo inatakiwa kuwa juu ili kukusaidia kuikunjurua kirahisi kwenye mpini wa uume. Acha nafasi kati ya kondomu na uume (kama inavyoonekana kwenye picha ya ndizi mwanzo wa makala hii) ili kusaidia kukusanya manii mwishoni mwa tendo la ngono. Mwombe mpenzi wako akusaidie kukuvalisha.

 • Wakati unakunjurua kondomu kwenye mpini wa uume(kama picha chini ya maelezo haya), hakikisha umeshika ncha yake kwa vidole, hii itasaidia kuacha nafasi kidogo kwa ajili ya kukusanya manii.

 • Baada ya kumaliza kufanya ngono, kabla uume haujalala kabisa, shika ringi ya kondomu kisha vua kwa kuitelemsha chini kiumakini ili kukinga kumwaga manii. Funga kondomu iliyovuliwa ili manii isimwagike kisha itupe sehemu ambapo mtu mwingine hataishika.

 • Endapo unahisi wakati wa tendo kondomu imepasuka, acha ngono mara moja, vua kondomu iliyopasuka na kisha vaa kondomu mpya ili kuendelea na ngono.

 • Hakikisha unatumia vilainishi vya uke wakati unafanya ngono ili kusaidia kupunguza msuguano. Unawza kutumia vilainishi vya kimiminika.

 • Vilainishi kama mafuta ya Vaseline, petroleum jelly, massage na ya kupikia hayatakiwa kutumika kwa sababu huweza kulainisha kondomu na kufanya ipasuke kirahisi.Mambo ya kuzingatia

 • Tumia kondomu ambayo bado haijaisha muda wake wa matumizi

 • Tumia kondomu inayofiti, yaani isiyopwaya kwenye uke au uume

 • Tumia kondomu mpya kwa kila tendo jipya la ngono

 • Acha nafasi kati ya kichwa cha uume na kondomu kwa ajili ya kukusanya manii

 • Vua kondomu kabla ya uume kusinyaa kwa kushika ringi ya kondomu

 • Usitumie vilainishi visivyo maalumu kwa ajili ya tendo la kujamiana kuzuia kondomu kupasuka

 • Kondomu zilizotengenezwa kwa latex hukinga maambukizi ya magonjwa ya zinaa pamoja na UKIMWI zaidi ya aina nyingine za kondomu.


Rejea za mada hii;


1. Allen, Michael J. (2011). The Anthem Anthology of Victorian Sonnets. Anthem Press. p. 51. ISBN 9781843318484. https://books.google.co.tz/books?id=GQxdE8Ryz9YC&pg=PR51&redir_esc=y#v=onepage&q&f=false. Imechukuliwa 17.01.20213. Medical news today. What are condoms and how are they used?. https://www.medicalnewstoday.com/articles/152833. Imechukuliwa 16.01.2021


4. Health New York Government. Frequently Asked Questions (FAQs) About Condoms. https://www.health.ny.gov/diseases/aids/consumers/condoms/faqs.htm#. Imechukuliwa 16.01.2021


5. CDC. Condom Fact Sheet In Brief. https://www.cdc.gov/condomeffectiveness/brief.html. Imechukuliwa 16.01.20217. CDC. Fact Sheet for Public Health Personnel. https://www.cdc.gov/condomeffectiveness/docs/Condoms_and_STDS.pdf. Imechukuliwa 16.01.2021

398 views0 comments

Recent Posts

See All

Comentarios


bottom of page