Nini husababisha ganzi
Updated: Nov 6, 2021

Mtu anapopata ganzi inamaanisha amepoteza hisia kwenye maeneo Fulani ya mwili, hili ni tatizo ambalo linaweza kuambatana na dalili zingine kama kuhisi kuchomwa na sindano au kuwaka moto kwenye maeneo yenye ganzi.
Ni nini husababisha ganzi?
Mara nyingi ganzi hutokea endapo kuna michomo au mgandamizo wa mshipa wa fahamu. Magonjwa aina Fulani kama kisukari huweza kuharibu mishipa mirefu ya fahamu mwilini kama inayopeleka hisia kwenye mikono na miguu na pia huweza kusababisha miguu kupata ganzi.
Baadhi ya hali na magonjwa yanayoweza kusababisha ganzi ni kisukari, upungufu wa vitamin B-12 n.k, Ukoma, Ugonjwa wa laimu, Maambukizi ya kirusi cha Herpes zoster
Kusoma zaidi kuhusu visababishi vya ganzi bonyeza hapa.
Pakua app ya ULY CLINIC kusoma makala nzuri za kiafya na kupata tiba bonyeza hapa
Unaweza kutembelea kurasa yetu ya facebook bonyeza hapa
Usisahau kuwashirikisha watu uwapendao kupakua app ya ULY CLINIC
Karibu ULY CLINIC kwa tiba na ushauri.