top of page

Forum Comments

Doxycycline inatumikaje jamani?
In Majadiliano na Wataalamu
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULYCLINIC
ULYCLINIC
16 Mei 2023
Kwa maelezo zaidi, tazama video hii
Content media
Kujifungua ni wiki ngapi?
In Majadiliano na Wataalamu
Azuma inatibu gono?
In Majadiliano na Wataalamu
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULYCLINIC
ULYCLINIC
04 Jan 2023
0621122578
Kiwango cha damu mwilini ni ngapi?
In Majadiliano na Wataalamu
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULYCLINIC
ULYCLINIC
04 Jan 2023
Karibu
Nini matokeo ya vipimo vya HIV (Bioline)
In Majadiliano na Wataalamu
Rangi ya kinyesi cha mtoto
In Majadiliano na Wataalamu
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULYCLINIC
ULYCLINIC
13 Feb 2022
Best Answer
Content media
1
0
Kujifungua ni wiki ngapi?
In Majadiliano na Wataalamu
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULYCLINIC
ULYCLINIC
09 Feb 2022
ttps://youtu.be/-glj98daTDQ
Content media
Kwanini kutapika nyongo kwa mama mjamzito?
In Majadiliano na Wataalamu
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULYCLINIC
ULYCLINIC
31 Jan 2022
Content media
1
0
Dalili za ukimwi ni zipi?
In Majadiliano na Wataalamu
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULYCLINIC
ULYCLINIC
31 Jan 2022
Content media
1
0
Nini matokeo ya vipimo vya HIV (Bioline)
In Majadiliano na Wataalamu
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULYCLINIC
ULYCLINIC
31 Okt 2021
Dilisha la matazamio Window period ya HIV au dilisha la matazamio la vipimo vya VVU ni muda utakaopita tangu kupata maabukizi na kabla ya kutambulika kuwa na maambukizi ya VVU kwa kutumia aina fulani ya kipimo. Muda huu hutofautiana kati ya kipimo na kipimo, kati ya mtu mmoja na mwingine na hutegemea aina ya sampuli pia iliyotumika yaani damu ya mishipa au ya kidole au sampuli ya mate. Dilisha la matazamio ni muda gani? Vipimo vingi vya haraka vya VVU vinavyotambua maambukizi kwa kutambua uwepo wa immunoglobin G, M na antijeni p24 ya kirusi huwa na dilisha la matazamio kati ya siku 45 hadi 90( sawa na miezi mitatu) hii ina maansha asilimia 99 ya watu walio na maambukizi ya VVU watatambulika ndani ya kipindi cha siku 45 hadi 90. Vipimo vya VVU Kuna madaraja manne ya vipimo vya kutambua VVU, vipimo dalaja la nne ni vipimo vinavyoweza kutambua kwa muda mfupi zaidi ukilindaganisha dalaja la la pili na kwanza ambayo huchukua takribani siku 90 kutambua asilimia 99 ya watu waliopata maambukizi. Kipimo cha HIV SD bioline kipo kwenye daraja la tatu la vipimo vya VVU. Maelezo kwa undani ya muda wa matazamio ya vipimo mbalimbali vya VVU unayapata kwenye linki hii. Rejea za mada hii; British HIV Association, British Association for Sexual Health and HIV and British Infection Association. Adult HIV Testing Guidelines 2020. Kevin P. et al. Time Until Emergence of HIV Test Reactivity Following Infection With HIV-1: Implications for Interpreting Test Results and Retesting After Exposure, Clinical Infectious Diseases, Volume 64, Issue 1, 1 January 2017, Pages 53–59, https://doi.org/10.1093/cid/ciw666 Delaney KP et al. Time from HIV infection to earliest detection for 4 FDA-approved point-of-care tests. https://www.croiconference.org/abstract/time-hiv-infection-earliest-detection-4-fda-approved-point-care-tests/. Imechukuliwa 31.10.2021 Avert. How do hiv tests work and what's involved?. https://www.avert.org/hiv-testing/whats-involved. Imechukuliwa 31.10.2021
1
0
Kazi ya dawa ya pedzinc mwilini
In Majadiliano na Wataalamu
Siku za mzunguko wa hedhi
In Majadiliano na Wataalamu
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULYCLINIC
ULYCLINIC
31 Jul 2021
Njia za kufahamu idadi ya siku za mzunguko wa hedhi Mwanamke anaweza kutambua idadi ya siku za mzunguko wa hedhi kuwa ni kwa kutumia kalenda au vikokoteo mbalimbali. Matumizi ya kalenda Ili kufahamu dadi ya siku za mzunguko wa hedhi moja na nyingine, unapaswa kuwa na kalenda yako pamoja na kalamu au penseli kisha; Zungushia duara kwenye tarehe ambayo damu ya hedhi imeanza kutoka na tarehe hedhi itakapokata Mwezi unaofuata zungushia mduara tena kwenye tarehe hiyo ya kuona hedhi na tarehe ya kumaliza hedhi na fanya hivi kwa angalau miezi mitatu Baada ya kuzungushia mduara kwenye tarehe kwa kipindi cha miezi mitatu ufanyaje? Baada ya miezi ya kuzungushia tarehe angalau kwa miezi mitatu fanya mahesabu madogo yanayofuata; Hesababu idadi ya siku kuanzia hedhi moja kuanza hadi siku moja nyuma kabla ya hedhi ya mwezi unaofuata kuanza- idadi ya siku utakazopata ni sawa na idadi ya siku katika mzunguko wako wa hedhi wa mwezi mmoja. Ili kupata uhakika wa idadi sahihi ya siku za mzunguko wako wa hedhi, tafuta wastani wa siku za mzunguko wa hedhi kwa kipindi cha angalau miezi mitatu yaani mfano, idadi ya siku za mzunguko wa hedhi kwa mwezi wa kwanza ulipoanza kuhesabu ni 28, idadi ya mwezi unaofuata ni 27 na idadi ya mwezi wa tatu ni 29, wastani wa mzunguko wa hedhi kwa muda wa miezi mitatu hii utakuwa sawa na; (28+ 27+29)/3 = 84/3= 28 Hivyo mzunguko wako wa hedhi ni wa siku 28 Mahesabu ya mfano kutoka kwenye picha Katika mwezi januari, idadi ya siku za mzunguko wa hedhi ni siku 32, mwezi februari ni siku 32 na mwezi machi ni siku 32, wastani au idadi ya siku za mzunguko wa hedhi kwa miezi mitatu ni sawa na (32+32+32)/3 = 96/3= siku 32 Hivyo idadi ya siku za mzunguko wa hedhi ni siku 32. Namna ya kufahamu wastani wa siku za damu ya hedhi Ili kufahamu wastani wa idadi ya siku za damu ya hedhi, tafuta wastani wa jumla ya idadi ya siku katika miezi mitatu Mfano mwezi wa kwanza uliingia siku 6, mwezi wa pili ni siku 4 na mwezi wa tatu ni siku 5, wastani wa siku zako za hedhi ni sawa na; (6+5+7)/3= 18/3= 6 Hivyo wastani wa siku za damu ya hedhi ni siku 6 Je kuna faida za kufahamu idadi ya siku za mzunguko wa hedhi? Ndio kuna faida nyingi za kufahamu mzunguko wako wa hedhi una siku ngapi hii ni pamoja na kukuwezesha kupata tarehe sahihi ya kujifungua kama ukitumia kikokoteo cha tarehe ta kujifungua na pia kujiandaa kufahamu ni lini utaingia hedhi inayofuata na lini utakuwa kwneye siku za hatari kwa kusoma kalenda yako. Rejea za makala hii; The society of obstetric and gynecologist of Canada. Normal period. https://www.yourperiod.ca/normal-periods/menstrual-cycle-basics/. Imechukuliwa 31.07.2021 Menstruation Calculator. https://healthengine.com.au/info/menstruation-calculator. Imechukuliwa 31.07.2021 Menstrual Cycle. https://www.womenshealth.gov/menstrual-cycle. Imechukuliwa 31.07.2021 ULY CLINIC. Mzunguko wa hedhi. https://www.ulyclinic.com/mzunguko-wa-hedhi. Imechukuliwa 31.07.2021 Beverly G Reed, MD, et al. The Normal Menstrual Cycle and the Control of Ovulation. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK279054/. Imechukuliwa 31.07.2021 Laurie Wideman, et al. Accuracy of Calendar-Based Methods for Assigning Menstrual Cycle Phase in Women. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC3658377/. Imechukuliwa 31.07.2021
Content media
1
0
Azuma inatibu gono?
In Majadiliano na Wataalamu
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULYCLINIC
ULYCLINIC
13 Jul 2021
Azuma inatibu gono? Ndio! Azuma inaweza kutibu gono kama gono hiyo imesababishwa na bakteria Neisseria gonorrhoeae na sio usaha uliosababishwa na magonjwa mengine ya zinaa. Wanaume wengi hudhani kuwa kutokwa na usaha sehemu za siri husababishwa na gono tu na hivyo huwapelekea kutumia Azithromycin bila ushauri wa daktari. Hili ni kosa linalopaswa kuachwa mara moja kwa kuwa husababisha madhara zaidi ya faida ambayo ni; Usugu wa vimelea vya maradhi kweye dawa hiyo Dawa kupoteza uwezo wa dawa kutibu ugonjwa huo Kuoneza sumu mwilini. Dawa yoyote ile iwe ya asili au hospitali ni sumu mwilini, hivyo inapaswa kuepukwa kwa namna yoyote ile Gharama zaidi za matibabu. Usugu wa vimelea unapotokea, dawa hii haiwezi kukutibu tena, na hivyo utahitajika kutibiwa na dawa nyingine. Dawa nyingine inayoweza kukutibu inaweza kufahamika bada ya kipimo cha culture and sensitivity ambacho ni gharama na dawa yenyewe itakuwa gharama pia. Kutokwa usaha sehemu za siri husababishwa na nini? Endapo (mwanaume) utafahamu kuwa kutokwa na usaha sehemu za siri huweza kusababishwa na ugonjwa wowote ule wa zinaa kama klamidia, kisonono, trikomoniasisi, basi acha kutumia AZUMA au dawa yoyote ila kushauriwa na daktari wako. Ongea na daktari kufahamu ni dawa gani inafaa kwako. Kumbuka Mtu anapotokwa usaha kwenye uume anapofika hospitali, hutibiwa kama mgonjwa wa magonjwa ya zinaa yaani klamidia, kisonono, na trikomoniasisi kwa dawa zaidi ya aina moja na si AZUMA tu kama wengi wanavyofanya. Penda kujisomea zaidi kuhusu chanzo cha dalili zako na kuwasiliana na daktari kabla ya kufanya uamuzi binafsi wowote. Wapi unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu magonjwa ya zinaa? Unaweza kupata taarifa zaidi kuhusu magonjwa ya zinaa kwa daktari wako. Kupata taarifa zaidi kuhusu magonjwa ya zinaa na namna yanavyotibiwa, kupitia makala za ULY CLINIC bofya hapa. Video ya maelezo ya ziada kuhusu azuma Makala hii imejibu maswali haya Azuma inatibu gono? Kwanini nimetumia azuma na sijapona dalili za gono Natokwa usaha kwenye uume nimetumia gono sijapona ni kwanini? Visababishi vingine vya uume kutoa usaha Maoni yako Toa maoni yako kuhusu hili kisha utajibiwa maswali yako na daktari wa ULY CLINIC, au tuma email kupitia linki ya 'mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii. Rejea za mada hii; @ ULY CLINIC. Dawa za kutibu gono. https://www.ulyclinic.com/dawa-gono. Imechukuliwa 13.07.2021 @ULY CLINIC. Dalili za gono. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/Dalili-za-Gono%28kisonono%29. Imechukuliwa 13.07.2021 @ULYCLINIC. Magonjwa ya zinaa. https://www.ulyclinic.com/magonjwa-na-saratani/Magonjwa-ya-zinaa. Imechukuliwa 13.07.2021 @ULY CLINIC. Uume kutoa usaha. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/Uume-kutoa-usaha. Imechukuliwa 13.07.2021 @ ULYCLINIC. Usaha sehemu za siri. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/Usaha-sehemu-za-siri . Imechukuliwa 13.07.2021 @ULYCLINIC. Azithromycin. https://www.ulyclinic.com/dawa/Azithromycin. Imechukuliwa 13.07.2021
1
0
Dalili za gono kwa mwanamke ni zipi?
In Majadiliano na Wataalamu
Dr.Sospeter Mangwella, MD
ULYCLINIC
ULYCLINIC
02 Jul 2021
Dalili za gono kwa wanawake Dalili za gono au gonorrhea (hufahamika pia kama gonorea au kisonono) kwa wanawake na wanaume huwa hazina utofauti mkubwa isipokuwa kuchelewa kuonekana kwa wanawake. Tafiti zinaonyesha ni asilimia 20 hadi 50 tu ya wanawake walioambukizwa gono huwa wanaonyesha dalili. Hata hivyo dalili za gono kwa wanaume huonekana haraka. Soma zaidi kuhusu dalili za gono kwa wanaume sehemu nyingine ya tovuti hii. Dalili hizo hizo ni zipi? Endapo dalili za gono kwa wanawake zitatokea, zifuatazo huwa miongoni mwa dalili; Kutoka ute, usaha au maji machafu ukeni Kutokwa na ute wenye harufu kali ukeni Maumivu makali wakati wa tendo la ndoa Kutokwa na ute wenye rangi ya njano, kijani au nyingine tofauti na kawaida ukeni Matibabu ya gono kwa wanawake Licha ya kuchelewa kutokea na kuwa na utofauti mdogo, matibabu ya gono hususisha matumizi ya dawa za antibiotiki zinazolenga kuua vimelea vya magonjwa yote ya zinaa endapo yataonekana kwenye vipimo ambayo ni kisonono, pangusa, trikomoniasisi, kaswende, chunjua na herpes. Orodha ya dawa za gono zinapatikana katika makala ya 'dawa za gono' au kwa kubofya hapa. Majina mengine ya dalili za gono Dalili za gono hufahamika na wagonjwa kwa majina ya 'dalili za kisonono', 'kutokwa usaha kwenye uume', kutokwa uchafu unaonuka ukeni,'kutokwa uchafu rangi ya njano au kijani au kahawia sehemu za siri' na 'ugonjwa wa zinaa' Wapi utapata maelezo zaidi kuhusi gono kwa wanawake? Kwa maelezo zaidi kuhusu gono na dalili za gono au 'dalili za kisonono' ingia kwa kubofya hapa Mambo muhimu kufahamu kukumbuka kuhusu dalili za gono kwa wanawake Dalili za gono zinaweza kufanana na magonjwa mengine ya zinaa, hakikisha siku zote unawasiliana na daktari wako kabla ya kujipa ugonjwa na kufanya matibabu pasipo ushauri wa daktari wako. Wapi unaweza kupata msaada zaidi? Endapo una maswali zaidi, wasiliana na daktari wako kwa ushauri na tiba. Waweza wasiliana pia na daktari wa ULY CLINIC moja kwa moja kupitia kitufe cha 'mawasiliano yetu' chini ya tovuti hii. Rejea za mada hii ULYCLINIC. Dalili za gono. https://www.ulyclinic.com/dalili-za-ugonjwa/Dalili-za-Gono%28kisonono%29. Imechukuliwa 02.07.2021 ULY CLINIC. Dawa za gono. https://www.ulyclinic.com/dawa-gono. Imechukuliwa 02.07.2021 NHS. STIs. https://www.nhs.uk/conditions/sexually-transmitted-infections-stis/. Imechukuliwa 02.07.2021 ULY CLINIC. rangi ya ute ukeni na maana yake kiafya. https://www.ulyclinic.com/post/rangi-ya-majimaji-ukeni-na-maana-zake-kiafya-uly-clinic. Imechukuliwa 02.07.2021
1
0

Dr.Sospeter Mangwella, MD

Admin
ULYCLINIC
+4
More actions
bottom of page