top of page

Tafiti ya matumizi ya ULYALOPEC01, zao litokanalo na mimea asili kama tiba asili ya upara (alopecia)

Utangulizi

ULY CLINIC imedhamini utengenezaji wa zao la ULYALOPEC01 ili kutumika katika tafiti ya kuthibitisha uwezo wa mimea mbalimbali ya asili katika matibabu ya upara kwa wanaume na wanawake. Zao la ULYALOPEC01 limetengenezwa kutoka kwenye mimea asili na hutumika kwa kupaka kwenye ngozi ya kichwa. Tafiti mbalimbali kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika vimeonyesha kuwa mimea iliyotumika kutengeneza zao la ULYALOPEC01 huwa na uwezo mkubwa Zaidi ya kutibu tatizo la upara(alopecia)

 

Je ULYALOPEC01 inalipiwa?

 

Hapana!

 

ULYALOPEC01 kwenye tafiti hii ya upara inatolewa pasipo malipo

Je ULYALOPEC01 kwa muda gani?

 

Mara baada ya kutimiza vigezo vya tafiti na kukubali kushiriki, utapatiwa zao la ULYALOPEC01 mara mbili tu, yaani kila baada ya miezi mitatu. Miezi sita ni muda unaotosha kuonyesha matokeo mazuri zaidi kama ilivyo onyeshwa na tafiti mbalimbali zilizoainishwa kwenye rejea ya kurasa hii.

 

Napataje maelezo zaidi kuhusu zao ULYALOPEC01?

Maelezo Zaidi kuhusu ULYALOPEC01 yanapatikana kwa kubofya hapa

Ili kuomba ushiriki kwenye tafiti hii, jaza taarifa zako kwa usahihi hapa chini kisha bofya kitufe cha kutuma

Kanusho

Licha ya kujiridhisha kuwa zao ULYALOPEC01 limetokana na mimea asili na hivyo kutokuwa na madhara kama likitumika kwa kupaka tu, ULY CLINIC haitahusika na madhara yoyote yatakayojitokeza kwako.

Kama unakubaliana na 'kanusho hili' utapaswa kuthibitisha kwa kuandika kwenye kiboksi hapa chini maneno yafuatayo;

'Nakubali kushiriki kwa akili zangu timamu na maamuzi haya nimeyafanya mwenyewe bila shinikizo la mtu au ULYCLINIC'

Au kama haupo tayari andikamaneno yanayofuata

'Sikubali kushiriki tafiti hii, nimefanya maamuzi haya nikiwa na akili zangu timamu bila shinikizo la mtu au ULYCLINIC'

Kuna makosa katika ujazaji wa fomu, tafadhari rudia tena na kutuma

Maombi yako yametumwa, utapata majibu mara baada ya kupitiwa. Asante

bottom of page