top of page

Imeandikwa na Daktari wa ULY CLINIC

Jumanne, 21 Aprili 2020

Kongosho

Kongosho

Utangulizi

Kongosho ni nini?

Kongosho au pancrease ni tezi iliyopo ndani ya mwili wa binaadamu (na pia wanyama wengine) ndani ya fumbatio chini ya mbavu na upande wa kushoto. Tezi hii imechomoza katitka sehemu ya mwanzoni ya utumbo mwembamba wa chakula (duodenum), nyuma kidogo ya tumbo la chakula na ina urefu wa sentimita 12 hadi 15 na unene wa sentimita 2.5.

Kazi ya tezi kongosho mwilini ni zipi?

Kongosho hufanya kazi kama tezi ya endokrain na teziisiyo ya endokrain. Kazi za endokrain ni uzalishaji wa vichochezi ( homon) na kazi zisizo za ki endokrain ni uzalishaji wa vimeng'enya mbalimbali.

Asilimia 98 ya seli za kongosho huzalisha vimeng'enya na asilimia 2 zilizobaki ni huzalisha homoni.

Kazi ya tezi ya kongosho katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula

Kongosho huzalisha lita moja na nusu ya juisi ya kongosho yenye vimeng'enya vifuatavyo na kazi zake:

• Amylase ya kongosho: Hii humeng'enya chakula cha wanga na kuivunjavunja kuwa wanga rahisi zaidi.
• Lipase ya kongosho: Hii humeng'enya vyakula vya mafuta.
• Trypsin: Hii humeng'enya vyakula vya protini.
• Chymotrypsin: Hii humeng'enya vyakula vya protini.
• Carboxypeptidase: Hii huendelea humeng'enya zaidi protini.
• Nuclease: Hii humengenya sehemu ya vinasaba vilivyomo kwenya chakula.

Kazi ya tezi ya kongosho kwenye mfumo wa homoni ni zipi?


Kazi kubwa ya kongosho ni kurekebisha kiwango cha sukari ya glukosi kwenye damu, kwa kuzalisha homoni ya insulini na glucagon. Pia kongosho inazalisha homoni nyingine ambazo ni somatostatin (kutoka seli za delta) na polypeptide ya kongosho kutoka seli F

Soma zaidi kuhusu kazi za homoni zinazozalishwa na kongosho sehemu nyingine kwenye tovuti hii

Magonjwa ya tezi kongosho ni yapi?

Magonjwa hatari kwa kongosho ni maambukizi ya pankreataitizi na saratani ya kongosho. Ugonjwa wa kisukari aina ya pili unasababiswa na seli za kongosho kushindwa uzalishaji wa kutosha wa homoni ya insulin.

Maambukizi ya kongosho- pankriataitiz ni nini?

Ni kuharibika kwa seli za kongosho. Maambukizi haya yanaweza kuwa ni;

• Maambukizi ya ghafa
• Maambukizi sugu

Nini kinacho sababisha maambukizi ya kongosho??

• Mawe kwenye kifuko cha nyongo(huziba mrija wa kongosho)
• Unywaji wa pombe
• Maambukizi ya baadhi virusi
• Uvimbe kwenye kongosho
• Baadhi ya dawa mfano azathioprine, corticosteroids
• Kuumia mfano kung'atwa na ng'e, upasuaji wa moyo.
• Sababu nyingine zisizojulikana vizuri

Vihatarishi vya kupata maambukizi sugu ya kongosho ni;

• Unywaji wa pombe
• Hali ya Kurithi
• Majeraha
• Kiwanogo cha juu cha madini ya Kalisimau kwenye damu(haipakalsimia)
• Sababu zisizojulikana

Dalili za maambukizi ya kongosho ni zipi?

• Maumivu sehemu ya juu ya tumbo
• Kichefuchefu
• Kutapika
• Maumivu ya tumbo kuelekea mgongoni
• Mapigo ya moyo kwenda kasi zaidi
• Michubuko kuzunguka kitovu na juu ya nyonga
• Macho na ngozi kuwa kuwa na rangi ya njano

Vihatarishi vya kupata saratani ya kongosho?

• Uvutaji wa sigara
• Kimekali kutokana na petroli
• Kurithi vinasaba vyakupata saratani hiyo
• Maambukizi sugu ya kongosho
• Ugonjwa wa sukari
• Uzito mkubwa
• Umri Zaidi ya miaka 65

Wasiliana na daktari wako endapo umeona kuwa una dalili yoyote ile katika maelezo haya kwa ushauri na tiba

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa ushauri na tiba zaidi kwa kupiga namba za simu chini ya tovuti hii au kubonyeza hapa.

Imeboreshwa,

13 Julai 2021 18:47:20

Rejea za mada hii;

1.Kumar and Clark’s clinical medicine 7th edition ISBN 9780702029936 ukurasa wa 377.

2.Principles of anatomy and physiology twelfth edition ISBN 978-0-470-08471-7 by Gerard J. Tortora and Bryan Derrickson ukurasa wa 669.

3.Madesscape: https://emedicine.medscape.com/article/181364-overview . Imechukuliwa 20/04/2020

4. Mayoclinic: https://www.mayoclinic.org/diseases-conditions/pancreatic-cancer/symptoms-causes/syc-20355421. Imechukuliwa tarehe 20/04/2020.
bottom of page