top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, M.D

Mhariri:

Dkt. Adolf S, M.D

Jumatatu, 24 Julai 2023

Mimba ya miezi kumi

Mimba ya miezi kumi

Mimba ya miezi kumi ni sawa na mimba ya wiki 37 hadi 40, katika kipindi hiki mabadiliko mbalimbali hutokea mwilini katika kila wiki. Makala hii imeelezea kuhusu mabadiliko yanayotokea katika kila wiki ya mimba ya miezi kumi.


Mimba ya wiki thelathini na saba (37)


Mambo ya kufahamu
  • Huashiria miezi tisa ya ujauzito ambapo zinakuwa zimesalia wiki 3 tu kufikia tarehe ya makadirio ya kujifungua.

  • Ujauzito huhesabika umekomaa na mama anaweza kujifungua muda wowote kuanzia wiki ya 37 hadi wiki ya 40, kwani ni asilimia ndogo ya wanawake hufikia tarehe ya makadirio ya kujifungua.

  • Mtoto anayezaliwa kuanzia wiki hii huwa amekomaa na mwili wake huwa tayari kuishi mazingira ya duniani.


Nini cha kufanya

Fanya mazoezi ya kutayarisha nyonga yako kwa ajili ya leba (kusoma zaidi kuhusu mazoezi ya kujiandaa na leba tembelea.


Mimba ya wiki thalathini na nane (38)

Kitangulizi cha mtoto asilimia kubwa huwa kichwa,huingia kwenye nyonga tayari kwa kutoka nje ya tumbo la uzazi. Hali hii huanza wiki ya 34 na kuendelea na wakati mwingine hutokea leba inapoanza.

Ute mzito unaoziba shingo ya kizazi huanza kuondoka na mama huona ute huo kwenye nguo za ndani au wakati wa kukojoa.


Mimba ya wiki thelathini na tisa (39)

Katika wiki hii inasalia wiki moja tu kufikia tarehe ya makadirio ya kujifungua, japokuwa leba inaweza kuanza muda wowote.


Hadi kufikia mwisho wa wiki ya 37 mtoto huwa na uzito wa takribani gramu 3000 hadi 4000 na urefu wa sentimeta 48 hadi 55. Ikumbukwe kuwa urefu na uzito wa mtoto hutokana na sababu mbali mbali kama vile vinasaba, lishe ya mama wakati wa ujauzito nk.


Mimba ya wiki arobaini (40)

Hii ni wiki ya mwisho inayokamilisha miezi 9 ya ujauzito, pia huwa ni wiki ya tarehe ya makadirio ya kujifungua kutoka hedhi ya mwisho.


Mama anapojifungua wiki hii huhesabika kuwa amefikia tarehe yake ya makadirio ya kujifungua, japokuwa anaweza kujifungua kuanzia wiki ya 37 au akachelewa hadi kufikia wiki 42 (kusoma zaidi kuhusu ujauzito uliopitiliza tembelea)

Imeboreshwa:

Jumatatu, 24 Julai 2023 20:40:12 UTC

Rejea za mada hii:

  1. American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]

  2. Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]

  3. Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]

  4. McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]

  5. Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]

  6. Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]

  7. Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]

  8. ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]

  9. Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]

bottom of page