top of page

Mwandishi:

Dkt. Mangwella S, M.D

Mhariri:

Dkt. Adolf S, M.D

Jumatatu, 24 Julai 2023

Mimba ya miezi tisa

Mimba ya miezi tisa

Mimba ya miezi tisa ni sawa na mimba ya wiki 33 hadi 36, katika kipindi hiki mabadiliko mbalimbali hutokea mwilini katika kila wiki. Makala hii imeelezea kuhusu mabadiliko yanayotokea katika lila wiki ya mimba ya miezi tisa.

Mimba ya wiki thelathini na tatu (33)

Mtoto hulala kwa muda mrefu na kupata ndoto namapafu yake huwa kwenye hatua za mwisho za ukuaji.

Nini hutokea kwa mtoto
  • Huwa na vipindi virefu vya kusinzia na kupata ndoto

  • Mapafu huwa katika hatua za mwisho za ukuaji tayari kwa upumuaji mara tu atakapozaliwa

Nini hutokea kwa mama

Huendelea kuona dalili na maudhi mbali mbali kama vile kushindwa kupumua, maumivu ya kiuno na mgongo nk.

Mimba ya wiki thelathini na tatu (33)

Kucheza kwa mtoto hupungua kwa kuwa mtoto huwa mkubwa kiasi cha kuchukua nafasi kubwa katika mji wa mimba.

Nini hutokea kwa mtoto
  • Mtoto huwa na urefu wa takribani sentimeta 43 na uzito wa gramu 2400

  • Mapafu huwa yamekomaa na endapo atazaliwa kipindi hiki basi hatakuwa na changamoto yoyote ya upumuaji

  • Kutokana na kuwa mkubwa na nafasi katika mji wa uzazi kuwa ndogo, mtoto hukunja miguu karibu kugusa kiwiliwili hivyo hukosa nafasi ya kujigeuza na kubaki na nafasi ya kuchezesha miguu na mikono tu.

  • Utando mweupe unaofunika ngozi yake huongezeka

Nini hutokea kwa mama
  • Kuanzia wiki hii na kuendelea mama huanza kuhisi kucheza kwa mtoto kunapungua tofauti na awali, badala yake huona na kihisi mtoto akirusha miguu au mikono kwa nguvu zaidi.

  • Hali ya maumivu yanayotokana na kutanuka na kusinyaa kwa misuli ya kizazi huweza kuongezeka

Mimba ya wiki thelathini na nne (34)

Mimba ya wiki thelathini na tano (35)

Mtoto huendela kuongezeka uzito na mwili wake kujiandaa kuishi nje ya tumbo la uzazi. Mama huendelea kuongezeka uzito na kuhisi dalili na maudhi mbali mbali.

Nini hutokea kwa mtoto
  • Mtoto huwa na urefu wa takribani sentimeta 43 na uzito wa gramu 2400

  • Mapafu huwa yamekomaa na endapo atazaliwa kipindi hiki basi hatakuwa na changamoto yoyote ya upumuaji

  • Kutokana na kuwa mkubwa na nafasi katika mji wa uzazi kuwa ndogo, mtoto hukunja miguu karibu kugusa kiwiliwili hivyo hukosa nafasi ya kujigeuza na kubaki na nafasi ya kuchezesha miguu na mikono tu.

  • Utando mweupe unaofunika ngozi yake huongezeka

Nini hutokea kwa mama
  • Kuanzia wiki hii na kuendelea mama huanza kuhisi kucheza kwa mtoto kunapungua tofauti na awali, badala yake huona na kihisi mtoto akirusha miguu au mikono kwa nguvu zaidi.

  • Hali ya maumivu yanayotokana na kutanuka na kusinyaa kwa misuli ya kizazi huweza kuongezeka

Mimba ya wiki thelathini na sita (36)

Viungo vyote vya mtoto huwa vimekoma na mtoto huweza kuishi nje ya mwili wa mama, mama anaweza kupata uchungu muda wowote ule.

Nini hutokea kwa mtoto
  • Kwa sehemu kubwa mifumo na ogani za mwili wake huwa zimekomaa kumuwezesha kuishi nje ya tumbo la uzazi, hata hivyo mtoto anayezaliwa kipindi hiki bado huhesabika kama njiti

  • Uzito wake hufikia takribani gramu 2700

Nini hutokea kwa mama
  • Anaweza kupata uchungu muda wowote kuanzia mwishoni mwa wiki ya 36

  • Mama anaweza kupata msongo na wasiwasi kuhusu leba na malezi ya mtoto hasa ikiwa ni ujauzito wa kwanza

Nini cha kufanya
  • Kama ni ujauzito wa kwanza jifunze kuhusu dalili na viashiria vya uchungu

  • Fanya maandalizi ya kupokea mtoto kiakili, kifedha nk.

  • Pata sapoti kutoka kwa mwenza, marafiki, ndugu na watu walio karibu nawe. Hii itakusaidia kuondoa msongo na wasiwasi.

Imeboreshwa:

Jumatatu, 24 Julai 2023 20:29:08 UTC

Rejea za mada hii:

  1. American Society for Reproductive Medicine; American College of Obstetricians and Gynecologists' Committee on Gynecologic Practice. Prepregnancy counseling: Committee Opinion No. 762. Fertil Steril. 2019 Jan;111(1):32-42. [PubMed]

  2. Berglund A, et al. Preconception health and care (PHC)-a strategy for improved maternal and child health. Ups J Med Sci. 2016 Nov;121(4):216-221. [PMC free article] [PubMed]

  3. Annadurai K, et al. Preconception care: A pragmatic approach for planned pregnancy. J Res Med Sci. 2017;22:26. [PMC free article] [PubMed]

  4. McClatchey T, et al. Missed opportunities: unidentified genetic risk factors in prenatal care. Prenat Diagn. 2018 Jan;38(1):75-79. [PubMed]

  5. Ko SC, et al. Estimated Annual Perinatal Hepatitis B Virus Infections in the United States, 2000-2009. J Pediatric Infect Dis Soc. 2016 Jun;5(2):114-21. [PubMed]

  6. Tohme RA, et al. Hepatitis B virus infection among pregnant women in Haiti: A cross-sectional serosurvey. J Clin Virol. 2016 Mar;76:66-71. [PMC free article] [PubMed]

  7. Bhavadharini B, et al. Screening and diagnosis of gestational diabetes mellitus - relevance to low and middle income countries. Clin Diabetes Endocrinol. 2016;2:13. [PMC free article] [PubMed]

  8. ACOG Practice Bulletin No. 190 Summary: Gestational Diabetes Mellitus. Obstet Gynecol. 2018 Feb;131(2):406-408. [PubMed]

  9. Rule T, et al. Introducing a new collaborative prenatal clinic model. Int J Gynaecol Obstet. 2019 Mar;144(3):248-251. [PubMed]

bottom of page