Tafiti 'Matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari'
Habari ndugu mtumiaji wa tovuti ya ULY CLINIC
Matumizi yasiyo sahihi ya dawa jamii ya ‘antibiotic’ na ‘antifungal’ zinazotibu magonjwa mbalimbali kama kisonono, TB, UTI, tonses, nimonia, homa ya matumbo, fangasi ukeni n.k, husababisha vimelea kuwa sugu na kutotibika na dawa hizo.
Tafiti nyingi zimefanyika kuangalia ukubwa wa tatizo la usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa na zinaonyesha kuwepo na ongezeko la wimbi kubwa la usugu wa vimelea vya maradhi kwenye dawa za kutibu maambukizi ya bakteria na fangasi. Tatizo hili linaweza kudhuru watu wa umri wowote na taifa lolote lile na huongeza gharama kwa wagonjwa na kukaa hospitali kwa muda mrefu.
Lengo la tafiti hii ni kuangalia 'matumizi ya dawa mtandaoni bila ushauri wa daktari' tatizo linaloweza kupelekea kutokea kwa 'Usugu wa vimelea kwenye dawa'. Tafiti hii ni mahususi katika kukusanya taarifa zinazohusu 'Usugu wa vimelea kwenye dawa' na vitu vinavyochangia kusababisha matumizi ya dawa pasipo ushauri wa daktari. Kwa kujaza taarifa hizi utasaidia kuboresha utoaji wa huduma za afya na matumizi sahihi ya dawa. ULY clinic inazingatia sera yake ya usiri wa taarifa zako, pia haikusanyi taarifa kuhusu emaili wala jina lako.
Ombi: Tafadhari jaza taarifa sahihi na kwa uaminifu katika vyumba 11 vilivyo hapa chini. Asante kwa kushiriki.
