Mwandishi:
ULY CLINIC
Mhariri:
Dkt. Benjamin L, MD
Ijumaa, 6 Agosti 2021
Kucheza kwa mtoto tumboni
Kucheza kwa mtoto tumboni hutokea pale mama anapopata hisia za mtoto kujigeuza, kupiga teke, ngumi au kufanya mjongeo wowote ule unaoleta shinikizo kwenye ukuta wa tumbo la uzazi. Hii ni ishara ya awali ya uzima wa mfumo wa fahamu, mifupa na misuli ya mtoto.
Kuna umuhimu wa kufahamu kama mtoto anacheza tumboni?
Dalili hii humwashilia kuwa ndani ya tumbo lako la uzazi kuna kiumbe anayeishi na ujauzito wako upo katika kipindi cha pili cha ujauzito
Sifa za uchezaji wa mtoto hutofautiana kipindi na kipindi na ujauzito na ujauzito. Ni jambo la msingi ukafahamu mtoto wako anacheza mara ngapi ili uweze kutambua ni wakati gani mapigo yamepugnua na uwasiliane na daktari kwa uchunguzi.
Mtoto huanza kucheza tumboni ujauzito ukiwa na wiki ngapi?
Umri wa kuanza kupata hisia za mtoto kucheza tumboni hutegemea uzoefu wa mama kwenye ujauzito. Mama mwenye uzazo zaidi ya mmoja hupata hisia mapema zaidi ya yule mwenye ujauzito wa kwanza.
Kama ni ujauzito wako wa kwanza, utaanza kuhisi mtoto anacheza kati ya wiki 18 hadi 22 za ujauzito
Na kama una uzao uliopita, ujauzito huu wa sasa utaanza kuhisi mapigo ya mtoto tumboni kuanzia wiki ya 16 hadi 20
Kwa mara ya kwanza mtoto huanza kucheza taratibu, unaweza kuwa na hisia za kutoka kwa gesi tumboni au mapigo ya mishipa ya damu kisha kuanza kuhisi mapigo makubwa nay a mara kwa mara. Jinsi mtoto anavyokuwa, mapigo nayo huwa makubwa zaidi kiasi ukiweka mkono tumboni, utahisi pigo la mtoto kwenye muda na muda.
Hata hivyo kuna utofauti wa muda wa kuanza kucheza kwa mtoto kwa kila ujauzito na jinsi unavyokuwa na uzao mwingi, muda wa kupata hisia hizo huja mapema zaidi katika ujauzito.
Kipindi cha tatu cha ujauzito yaani kuanzia wiki ya 28 na kuendelea mtoto hucheza kwa nguvu zaidi. Hii ni hutokana na mtoto huyo kuwa na umbile kubwa zaidi na nguvu nyingi za kuweza kutikisa tumbo la mama kwa nguvu anapopiga ngumi, kujinyoosha, kujongea au kupiga teke. Kuongezeka umbile la mtoto kipindi hiki hupunguza nafasi tumboni kiasi kwamba mtoto hushindwa kugeuka. Huu ni wakati ambapo mtaalamu wa afya ataanza kupima mapigo ya mtoto kwa kuhesabu idadi ya mitikiso tumboni inayoletwa na mapigo hayo
Idadi ya uchezaji wa mtoto
Idadi ya kawaida ya mapigo ya tumbo kutokana na uchezaji wa mtoto tumboni ni mapigo 10 au zaidi ndani ya masaa 2 utakayoyahisi wakati umelalia upande mmoja na kuweka akili yako kuhesabu mapigo hayo. Mapigo utayoyapata huwa kama hisia za mpwito, kugeuka au kupiga ngumi au teke kwenye tumbo.
Kama umekaribia kujifungua, wastani wa mapigo ya mtoto tumboni huwa 31 kwa saa, lakini hutofautiana kati ya mjamzito mmoja na mwingine kuanzia mapigo 16 hadi 45 kwa saa.
Muda unaodumu kati ya mapigo ni dakika 50 hadi 75 kwa dakika. Mtoto anaweza kulala kwa dakika 20 hadi 40 na kipindi hiki hutapata hisia za mapigo yake, muda wa kulala mara nyingi hauzidi dakika 90.
Endapo mtoto hachezi auamepunguza kucheza unapaswa kufika hospitali kwa vipimo. Vipimo ambavyo utafanyiwa vitaangalia mapigo ya mtoto, mapigo ya moyo na hali ya afya ya mtoto kwa kutuma ultrasound au fitoskopi.
Visababishi na matokeo ya kupungua kwa mapigo ya mtoto tumboni
Visababishi vinaweza kuwa visivyo vya hatari mfano mtoto akiwa anataka kuzinzia au akiwa amelala, mapigo yake huwa kidogo. Hii ndio maana unabidi kuhesabu muda ule ule ambapo mapigo ni mengi.
Endapo mtoto hajalala na mapigo yamepungua huweza kumaanisha
Mtoto kuny’ongwa na kitovu kitovu chake
Mtoto hakui vema
Mtoto mwenye uzito mdogo
Kutojiweza kwa kondo la nyuma
Maji kidogo kwenye chupa ya uzazi
Ujauzito unaotishia kutoka
Kujiongezea damu kwa mama na mtoto
Maambukizi ndani ya mfuko wa kizazi
Matokeo yanayo ambatana na kupungua kucheza kwa mtoto tumboni ni;
Madhaifu ya kimaumbile kwa mtoto
Kujifungua kabla ya wakati
Majeraha kwenye ubongo wakati wa kuzaliwa
Kuharibika kwa mfumo wa neva
Uzito mdogo wa mtoto
Alama chache za Apgar
Kushuka kwa kiwango cha sukari kwenye damu ya mtoto
Kujifungua kwa upasuaji
Kujifungua kwa kuanzishiwa uchungu
Kufa kwa mtoto tumboni
Kufa kwa mtoto baada ya kuzaliwa
Namna ya kuongeza mapigo ya mtoto tumboni
Unaweza kufanya vitu vifuatavyo kuongeza idadi ya mapigo ya mtoto tumboni;
Kula au kunywa kitu kitamu kama juisi ya matunda n.k
Fanya mazoezi ya kutembea
Mulika mwanga wa kung’aa kwenye tumbo lako mfano unaweza kutumia tochi iliyowaka.( kuwa makini usiungue na mwanga)
Ongea na mwanao aliye tumboni
Sukuma tumbo upande mmoja kwenda mwingine bila kutumia nguvu
ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi
Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.
Imeboreshwa,
6 Oktoba 2021 16:01:28
Rejea za mada hii:
1. Flenady V, et al. Detection and management of decreased fetal movements in Australia and New Zealand: a survey of obstetric practice. Aust N Z J Obstet Gynaecol 2009;49:358–63.
2. Frøen JF, et al. Fetal movement assessment. Semin Perinatol 2008;32:243–46.
3. Hofmeyr GJ, et al. Management of reported decreased fetal movements for improving pregnancy outcomes. Cochrane Database Syst Rev 2012;4:CD009148.
4. New South Wales Health. Maternity – Decreased Fetal Movements in Third Trimester. Sydney: New South Wales Health, 2011.
5. Preston S, et al. for the Australia and New Zealand Stillbirth Alliance (ANZSA). Clinical practice guideline for the management of women who report decreased fetal movements. 1st edn. Brisbane: ANZSA, 2010.
6. Royal College of Obstetricians and Gynaecologists. Reduced fetal movements. www.rcog.org.uk/files/rcog-corp/GTG57RFM25022011.pdf . Imechukuliwa 06.08.2021
7. Smith GC, et al. Stillbirth. Lancet 2007;370:1715–25.
8. TveitJV, et al. Reduction of late stillbirth with the introduction of fetal movement information and guidelines - a clinical quality improvement. BMC Pregnancy Childbirth 2009;9:32.
9. Akelsson A, et al. Increased labor induction and women presenting with decreased or altered fetal movements - a population-based survey. DOI: 10.1371/journal.pone.0216216. Imechukuliwa 06.08.2021
10. Bradford BF. A diurnal fetal movement pattern: Findings from a cross-sectional study of maternally perceived fetal movements in the third trimester of pregnancy. DOI:
10.1371/journal.pone.0217583. Imechukuliwa 06.08.2021
11. Bradford B, et al. Maternally perceived fetal movement patterns: The influence of body mass index. DOI: 10.1016/j.earlhumdev.2019.104922. Imechukuliwa 06.08.2021
12. Bryant J, et al. Fetal movement.ncbi.nlm.nih.gov/books/NBK470566/. Imechukuliwa 06.08.2021