top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Salome A, MD

Jumatatu, 22 Machi 2021

Kulia machozi huondoa homoni zinazoleta msongo mwilini

Kulia machozi huondoa homoni zinazoleta msongo mwilini

Tafiti mbalimbali zinaoyesha kuwa, mtu akilia machozi kutokana na msongo mwilini, machozi yanayotoka hutoa sumu na homoni mbalimbali zinazosababisha msongo mwilini. Homoni za msongo zinapoachiliwa kwenye machozi baada ya kulia husababisha mfumo unaohusika kutuliza mwili ufanye kazi vema na hivyo husababisha kupata tumaini, kufikiria vema na wakati mwingine kupata usingizi mzuri.


Kwanini ulie machozi kama unahisi msongo moyoni?


Unapokuwa na msongo moyoni au mwilini, kutokana na mambo magumu yasiyo na majibu katika maisha yako, mambo yanayo kuletea mawazo mengi zaidi bila kupata majibu na kukukosesha usingizi, ni vema endapo unauwezo wa kulia machozi, ukalia ili upate tulizo la msongo huo.


Nini kinatokea mwilini unapokuwa na msongo?


Tafiti zinaonyesha kuwa homoni za msongo ikiwa pamoja na Cortisol huongezeka sana kwenye damu kwa watu wenye msongo, homoni hii huwa na shughuli mbalimbali ili kukabiliana na magumu unayokutana nayo katika maisha. Endapo kuna jambo la kusikitisha, jambo la hatari, jambo linalokufanya uwe na mawazo mengi, homoni hii huzalishwa kwa wingi ili kukabiliana na hali hizo kwa kukufanya uwe na nguvu zaidi na imara. Homoni hii ni nzuri endapo itadumu kwa muda mfupi, endapo itadumu kwa muda mrefu huambatana na madhara. Cortisol huwa na madhara mwilini ya kuongeza sukari kwenye damu, kuongeza shinikizo la damu n.k. Unaweza fikiria kuwa endapo utakuwa na homoni hizi kwa wingi kwenye damu, unahatari ya kupata matatizo ya kisukari pamoja na shinikizo la juu la damu hapo mbeleni.


Nini kinatokea mwilini ukiwa unalia machozi?


Unapolia machozi, unapunguza kwa kiasi kikubwa kwenye damu homoni cortisol pia kuamsha mfumo wa fahamu wa parasimpathetiki unaokupa tulizo la mwili. Kulia machozi kufuatia jambo linaloleta msongo mwilini ni njia inayoweza kukusaidia kukabiliana na magonjwa mbalimbali ya mwili na sio kukufanya uwe dhaifu kama inavyofahamika kwamba watu wanaolia ni dhaifu.


Sehemu gani unatakiwa kulia machozi?


Ni vema ukafahamu sehemu sahihi ambayo itakuwa vema kwako kulia machozi na kuondoa sumu zote mwilini. Endapo upo msibani unaweza kulia a wengine wanaolia, endapo upo kwenye kikao ofisini si vema ukamwaga machozi mbele ya watu kwani wataona wewe ni dhaifu au unajaribu kujitetea kwa machozi. Ikitegemea na mazingira, unashauriwa kutafuta shemu usiyoonekana au kusikika ili ulie vya kutosha na kutua mzigo ndani ya moyo wako.


Wapi unaweza pata maelezo zaidi kuhusu kulia machozi?


Pata maelezo zaidi kwenye blog kuhusu makala ya kulia machozi na wakati gani kulia machozi hakukusaidii kitu na wakati gani kulia kunaweza kuwa dalili ya ugonjwa wa msongo wa mawazo na uhaja wa kuonana na daktari kwa ajili ya matibabu.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

19 Julai 2023 20:40:43

Rejea za mada hii:

1. Asmir Gračanin , et al. Is crying a self-soothing behavior?. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC6402489/#R29. Imechukuliwa 21.02.2021

2. Breuer, Josef, and Sigmund Freud. Studies on hysteria. Hachette UK, 2009. Imechukuliwa 21.02.2021

3. Frey WH (1985). Crying: The mystery of tears Minneapolis, MN: Winston Press. Imechukuliwa 21.02.2021

4. Gračanin A, et al. Is crying a selfsoothing behaviour? Frontiers in Psychology, 28(5), 502. doi:10.3389/fpsyg.2014.00502. inapatikana https://pubmed.ncbi.nlm.nih.gov/24904511/. Imechukuliwa 21.02.2021

5. Bowlby J (1980). Loss: Sadness and depression New York, NY: Basic Books

6. Nelson JK (2005). Seeing through tears: crying and attachment New York, NY: Routledge.

7. Hasson O (2009). Emotional tears as biological signals. Evolutionary Psychology, 7, 363–370.

8. Nelson J. K. (2008). “Crying in psychotherapy: Its meaning, assessment and management based on attachment theory,” in Emotion Regulation: Conceptual and Clinical Issues eds Vingerhoets A. J. J. M., Nyklicek I., Denollet J. (New York, NY: Springer; ) 202–214

9. Hendriks M. C. P., Nelson J. K., Cornelius R. R, Vingerhoets A. J. J. M. (2008b). “Why crying improves our well-being: an attachment-theory perspective on the functions of adult crying,” in Emotion Regulation: Conceptual and Clinical Issues eds Vingerhoets A. J. J. M., Nyklicek I., Denollet J. (New York, NY: Springer; ) 87–96

10. Is Crying Good for You?. https://www.webmd.com/balance/features/is-crying-good-for-you#. Imechukuliwa 22.03.2021

11. Chronic stress puts your health at risk. Chronic stress can wreak havoc on your mind and body. Take steps to control your stress.https://www.mayoclinic.org/healthy-lifestyle/stress-management/in-depth/stress/art-20046037#. Imechukuliwa 22.03.2021

bottom of page