top of page

Mwandishi:

Dkt. Charles W, MD

Mhariri:

Dkt. Benjamin L, MD

Ijumaa, 19 Novemba 2021

Majira yenye vichocheo viwili na saratani

Majira yenye vichocheo viwili na saratani

Saratani ya endometria na ovari

Matumizi ya vidonge vyenye vichocheo viwili huwakinga watumiaji kwenye aina mbili za saratani ambazo ni saratani ya ovari na saratani ya kizazi (saratani endometria) wakati huo huongeza hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizaz kwa kiasi kidogo.


Kinga ya saratani hudumu muda gani?

Kinga dhidi ya saratani hizo huednelea kwa miaka 15 au zaidi baada ya kuacha kutumia vidonge.


Saratani ya Matiti


Matokeo ya utafiti kuhusu vidonge vyenye vichocheo viwili na saratani ya matiti ni vigumu kuyaeleza;


  • Utafiti umeonyesha kuwa wanawake wanaotumia vidonge vyenye vichocheo viwili zaidi ya miaka 10 iliyopita wanakabiliwa na hatari ya kupata saratani ya matiti sawa na wanawake ambao hawajawahi kutumia vidonge hivi. Kinyume chake, watumiaji wanaoendelea kutumia vidonge vyenye vichocheo viwili na wanawake ambao wametumia vidonge vyenye vichocheo viwili katika miaka kumi iliyopita wana hatari kubwa zaidi wa kupata saratani ya matiti.

  • Wakati mtumiaji wa sasa au aliyekuwa akitumia Vidonge vyenye vichocheo viwili akipatikana na saratani ya matiti, saratani hizo zinakuwa hazijakomaa kama saratani zinazowapata wanawake wengine.

  • Haieleweki wazi kama matokeo haya yameelezwa kutokana na ugunduzi wa awali wa saratani ya matiti miongoni mwa watumiaji wa vidonge vyenye vichocheo viwili au kutokana na athari za awali za kimaumbile za vidonge vyenye vichocheo viwili kwa saratani ya matiti.


Saratani shingo ya Kizazi.


Saratani ya seviksi husababishwa na aina fulani za virusi papiloma au kwa Kiingereza vinaitwa “human papillomavirus” (HPV). HPV ni virusi vya kawaida vinavyoambukizwa kwa ngono ambavyo huondoka vyenyewe bila tiba, lakini wakati fulani huendelea kuwepo.


Matumizi ya vidonge vyenye vichocheo viwili kwa miaka 5 au zaidi yanaelekea kuongeza kasi ya kuendelea kuwepo maambukizi ya HPV kuwa saratani ya seviksi. Idadi ya saratani za seviksi zinazohusiana na matumizi ya vidonge vyenye vichocheo viwili inafikiriwa kuwa ndogo sana.


Iwapo upimaji wa saratani ya shingo ya kizazi unapatikana, watoa huduma wanaweza kuwashauri watumiaji na wanawake wengine wasiotumia kupimwa kila baada ya miaka mitatu (au kulingana na mapendekezo ya mwongozo wa taifa) ili kugundua mabadiliko yoyote ya dalili za saratani kwenye shingo ya uzazi yanayoweza kuchukuliwa hatua mapema.


Vihatarishi vya satarani ya shingo ya kizazi


Vihatarishi vinavyojulikana kuongeza hatari ya kupata saratani ya shingo ya kizazi ni pamoja na kuzaa watoto wengi na uvutaji wa sigara.

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

27 Novemba 2021 08:19:30

Rejea za mada hii:

1. Cooper DB, et al. Oral Contraceptive Pills. 2021 Aug 25. In: StatPearls [Internet]. Treasure Island (FL): StatPearls Publishing; 2021 Jan–. PMID: 28613632.

2. Baird DT, et al. Hormonal contraception. N Engl J Med. 1993 May 27;328(21):1543-9.

3. Maguire K, et al. The state of hormonal contraception today: established and emerging noncontraceptive health benefits. Am J Obstet Gynecol. 2011 Oct;205(4 Suppl):S4-8.

4. Committee on Gynecologic Practice. ACOG Committee Opinion Number 540: Risk of venous thromboembolism among users of drospirenone-containing oral contraceptive pills. Obstet Gynecol. 2012 Nov;120(5):1239-42.

5. Shulman LP. The state of hormonal contraception today: benefits and risks of hormonal contraceptives: combined estrogen and progestin contraceptives. Am J Obstet Gynecol. 2011 Oct;205(4 Suppl):S9-13.

6. ACOG Practice Bulletin No. 110: noncontraceptive uses of hormonal contraceptives. Obstet Gynecol. 2010 Jan;115(1):206-218.

7. CDC.Oral Contraceptives and Cancer Risk. https://www.cdc.gov/mmwr/preview/mmwrhtml/00001216.htm#. Imechukuliwa 19.11.2021

8. Asthana S, et al. Oral contraceptives use and risk of cervical cancer-A systematic review & meta-analysis. Eur J Obstet Gynecol Reprod Biol. 2020 Apr;247:163-175. doi: 10.1016/j.ejogrb.2020.02.014. Epub 2020 Feb 21. PMID: 32114321.

9. White, Nicole D. “Hormonal Contraception and Breast Cancer Risk.” American journal of lifestyle medicine vol. 12,3 224-226. 31 Jan. 2018, doi:10.1177/1559827618754833.

10. Gierisch JM, et al. Oral contraceptive use and risk of breast, cervical, colorectal, and endometrial cancers: a systematic review. Cancer Epidemiol Biomarkers Prev. 2013 Nov;22(11):1931-43. doi: 10.1158/1055-9965.EPI-13-0298. Epub 2013 Sep 6. PMID: 24014598.

bottom of page