top of page

Mwandishi:

ULY CLINIC

Mhariri:

Dkt. Mangwella S, MD

Jumanne, 17 Agosti 2021

Umri mzuri wa kushika mimba

Umri mzuri wa kushika mimba

Mwanamke anapozaliwa huwa na mayai takribani milioni 2 yanayopungua kadri umri unavyoongezeka. Mayai elfu 25 husalia kwenye umri wa miaka 37 na elfu 1 kwenye umri wa miaka 51. Ili kushika ujauzito wenye matokeo mazuri kwako na mtoto, shika baada ya miaka 20 na kabla ya miaka 35.


Mahusiano ya ujauzito na umri


Kwa kawaida unaweza pata mimba mara unapoanza ona damu ya hedhi na kabla ya kuingia kipindi cha koma hedhi na wastani wa umri wa wanawake wengi kupata ujauzito huwa kati ya miaka 12 hadi 51.


Uwezo wa kushika mimba hupungua kwa jinsi unavyoongezeka umri kiasi cha kuwa vigumu sana kwenye umri kuanzia miaka 37 na kuendelea. Licha ya uwezo kupugnua, kupata mimba kwenye umri mkubwa zaidi huambatana na madhara mbalimbali kwa mama na mtoto.


Umri mzuri unaoshariwa kushika mimba yenye matokeo mazuri kwa mama na mtoto ni baaada ya miaka 20 na mwanzoni mwa miaka 30.

Je umri unadhuru vipi uwezo wa kubeba mimba?


Kwa kawaida mwanamke huzaliwa na mayai milioni 2 yanayo pungua idadi na ubora kadri umri unavyoongezeka. Mayai elfu 25 tu husalia unapofikisha umri wa miaka 37 na elfu 1 tu kwenye umri wa miaka 51. Uzazi hupungua kwa jinsi inadadi na ubora wa mayai unavyopungua


Mambo mengine yanayodhuru uwezo wa kubeba ujauzito kwenye umri mkubwa?


Kwa jinsi unavyoongezeka umri, hatari ya kupata matatizo mbalimbali ya uzazi kutokana na uzee na maambukizi huongezeka kiasi cha kuweza kusababisha usishike mimba kirahisi au kuwa na ujauzito wenye matokeo mabaya. Mfano wa magonjwa yanayodhuru ujauzito na hutokea ukubwani ni ugonjwa wa endometriosis na magonjwa ya mirija ya uzazi.


Mara unapofikisha umri wa miaka 32, uwezo wa kubeba mimba huanza pungua na unapoanza miaka 35 hadi 37, uwezo huo hupungua kwa kasi zaidi


Vihatarishi vinavyopunguza uwezo wa kushika mimba


Vihatarisi vingine vinavyopunguza uwezo wa kushika mimba ni;


 • Kuvuta sigra

 • Kutumia ya baadhi ya dawa za uzazi wa mpango

 • Matumizi ya baadhi ya dawa za kutibu saratani

 • Maambukizi kwenye via vya uzazi


Kuna hatari ya kubeba ujauzito kwenye umri mkubwa?

 • Kupata ujauzito baada ya miaka 35 huambatana na mambo yafuatayo;

 • Kisukari cha ujauzito

 • Ugonjwa wa shinikizo la juu la damu

 • Kifafa cha mimba

 • Kujipandikiza kwa kondo karibu na njia ya uzazi

 • Ujauzito kutoka

 • Kujifungua njiti

 • Mtoto kufia tumboni

 • Kujifungua kwa upasuaji

 • Kutokwa na damu nyingi wakati wa ujauzito

 • Kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua

 • Kujifungua mtoto mwenye uzito mdogo

 • Kujifungua mtoto mwenye sindromu ya down

ULY CLINIC inakushauri siku zote uwasiliane na daktari wako kabla ya kuchukua hatua yoyote ile kiafya baada ya kusoma vidokezo hivi

Wasiliana na daktari wa ULY CLINIC kwa elimu na ushauri zaidi kupitia namba za simu au kubonyeza 'Pata Tiba' Chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa,

7 Oktoba 2021 04:58:30

Rejea za mada hii:

1. Age and fertility. pregnancy.sogc.org/fertility-and-reproduction/age-and-fertility. Imechukuliwa 17.08.2021

2. Alcohol and fertility. yourfertility.org.au/for-women/alcohol-and-fertility/. Imechukuliwa 17.08.2021

3. Balasch J, et al. Delayed childbearing: effects on fertility and the outcome of pregnancy. Curr Opin Obstet Gynecol. 2012;24:187–93

4. Barclay K. Advanced maternal age and offspring outcomes: Reproductive aging and counterbalancing period trends. DOI: 10.1111/j.1728-4457.2016.00105.x. Imechukuliwa 17.08.2021

5. Births and natality.cdc.gov/nchs/fastats/births.htm. Imechukuliwa 17.08.2021

6. Briggs H. ONS: Mothers' average age hits 30. 2014

7. Carlo Bellieni, M.D, et al. The Best Age for Pregnancy and Undue Pressures. https://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC5241353/. Imechukuliwa 17.08.2021

8. Carter D, et al. Should there be a female age limit on public funding for assisted reproductive technology? J Bioeth Inq. 2013;10:79–91

9. Dietl A, et al. Pregnancy and obstetrical outcomes in women over 40 years of age. DOI:
10.1055/s-0035-1546109. Imechukuliwa 17.08.2021

10. Female age-related fertility decline. acog.org/Clinical-Guidance-and-Publications/Committee-Opinions/Committee-on-Gynecologic-Practice/Female-Age-Related-Fertility-Decline. Imechukuliwa 17.08.2021

11. Goisis A, Sigle-Rushton W. Childbearing postponement and child well-being: a complex and varied relationship? Demography. 2014;51:1821–41

12. Having a baby after age 35. acog.org/Patients/FAQs/Having-a-Baby-After-Age-35. Imechukuliwa 17.08.2021

13. Infertility.cdc.gov/nchs/fastats/infertility.htm. Imechukuliwa 17.08.2021

14. Lyngsø J, et al. Association between coffee or caffeine consumption and fecundity and fertility: A systematic review and dose-response meta-analysis. DOI: 10.2147/CLEP.S146496. Imechukuliwa 17.08.2021

15. Martin JA, et al. Births: Final data for 2012. Natl Vital Stat Rep. 2013;62(9):1–68

16. Matthews TJ, et al. Delayed childbearing: more women are having their First child later in life. NCHS Data Brief. 2009;(21):1–8

17. Mazza D, et al. Making decisions about fertility--three facts GPs need to communicate to women. Aust Fam Physician. 2012;41:343–6

18. Menopause 101: A primer for the perimenopausal. menopause.org/for-women/menopauseflashes/menopause-symptoms-and-treatments/menopause-101-a-primer-for-the-perimenopausal. Imechukuliwa 17.08.2021

19. Mirowsky J. Parenthood and health: The pivotal and optimal age at first birth. DOI:
10.1353/sof.2002.0055. Imechukuliwa 17.08.2021

20. Periods. nhs.uk/conditions/periods. Imechukuliwa 17.08.2021

21. Rossen LM, et al. Quarterly provisional estimates for selected birth indicators, 2014–Quarter 1, 2016 National Center for Health Statistics National Vital Statistics System, Vital Statistics Rapid Release Program. 2016

22. Setiawan VW, et al. Age at last birth in relation to risk of endometrial cancer: pooled analysis in the epidemiology of endometrial cancer consortium. DOI: 10.1093/aje/kws129. Imechukuliwa 17.08.2021

23. Sozou PD. Time to pregnancy: A computational method for using the duration of non-conception for predicting conception. DOI: 10.1371/journal.pone.0046544. Imechukuliwa 17.08.2021

bottom of page