top of page

Mwandishi;

Dkt. Benjamin L, MD

Mhariri;

Dkt. Mangwella S, MD

30 Machi 2020 04:07:25

Kirusi Rota

Rotavirus

Kirusi Rota ni aina ya kirusi chenye RNA mbili katika familia ya Reoviridae. Kirusi huyu huongoza kusababisha ugonjwa wa kuharisha kwa watoto wadogo karibia duniani kote bila kujali utofauti wa kijamii na kiuchumi. Tafiti zinaonyesha kuwa kila mtoto ulimwenguni kabla ya kufikisha miaka mitano atakuwa ameambukizwa angalau mara moja na kirusi huyu. Kila maambukizi yanapotokea mtoto hupata kinga, kwa hivyo maambukizi yanayofuatia huwa hayana uzito sana, hata hivyo watu wazima huwa hawa athiriwi sana na kirusi huyu.


Aina za virusi vya Rota


Kuna aina kumi za genera za kirusi rota zinazojulikana ambazo ni A, B, C, D, E, F, G, H, I na J. Kirusi Rota A, B na C, husababisha maambukizi kwa binadamu. Kirusi Rota A huongoza kusababisha kuhara kwa watoto kwa zaidi ya asilimia 90 ya maambukizi ya Kirusi Rota kwa wanadamu.


Sifa za kirusi


 • Huwa na kipenyo cha nautikol mile 70 na huwa na kuta tatu za ikosahedro, lakini hana ukuta wa nje

 • Mwonekano wake wa nje huwa kama ringi ndogo ambayo ina spoku fupi zinazochomoza na hivyo mwonekano huu ki Latini unaitwa “rota” kwa Kiswahili ni ringi

 • Jinomu ya rota huwa na RNA mbili

 • Huwa imara kwenye joto

 • Huwa ni imara wenye joto dogo na PH ndogo (3.5-10)

 • Vimeng’enya vya tripsin huongeza maambukizi ya kirusi


Maambukizi na uzalianaji wa kirusi


Mara baada ya mtu kupata maambukizi, kirusi rota huenda kwenye utumbo mwembamba na kuathiri ukuta wa ndani ya tumbo. Kikiwa kwenye utumbo mwembamba, kirusi huchukua muda mfupi kuzaliana takriban masaa 48 kabla ya mgonjwa kupata dalili za homa, kutapika na kuharisha, marachache kuishiwa maji mwilini.


Dalili za maambukizi ya Kirusi Rota


 • Kutapika huwa ni kwa muda mfupi, huweza kuanza kama dalili ya kwanza

 • Kuharisha- Uharo huwa na sifa za majimaji, rangi ya kijani au njano lakini huwa hayana mlenda.


Maambukizi ya rota huhitaji dawa?


Ugonjwa wa rota huwa unapona wenyewe ndani ya siku 5 hadi 10 bila madhara yoyote.


Kinga dhidi ya kirusi rota


Kuna chanjo ambayo imegunduliwa tayari toka mwaka 1998 na inafanya kazi ya kuwankinga watoto wadogo dhidi ya maambukizi ya kirusi hiki.


Chanjo ya rotavirusi imekuwa ikitumika na inafanya kazi kwa asilimia 80 hadi 90 kukinga watoto dhidi ya kuharisha kwenye nchi nyingi isipokuwa nchi zinazoendelea kama peru na brazili ambapo chanjo hii huzuia kuharisha kwa asilimia 20 hadi 30.


Uenezaji wa kirusi Rota


Kirusi Rota huenezwa kwa njia ya kinyesi cha mtoto aliyeambukizwa. Kirusi Rota hupitia mdomoni kwa kula chakula kilichochanganyika na kinyesi , kupitia mikono iliyoshika kinyesi , vitu vingine kama maji yaliyochafuka na kinyesi na pia kwa njia ya kupumua. Kinyesi cha mtu aliyeambukizwa kinaweza kuwa na chembe zaidi ya trilioni 10 za kirusi kwa gramu moja.


Magonjwa yanayofanana na Rota


Magonjwa yanayoweza kufanana dalili na homa ya matumbo ni pamoja na;


 • Giardiasis

 • Kuishiwa maji kwa mtoto

 • Gastroenteraitiz

 • Gastroenteraitiz ya watoto

 • Maambukizi ya salmonella kwa watoto


Matibabu ya Ugonjwa wa homa ya kuharisha


Hakuna matibabu maalum kwa ajiri ya ugonjwa wa homa ya kuharisha, ila mgonjwa anaweza pata yafuatayo;


 • Hakikisha njia ya hewa, upumuaji na mzunguko wa damu uko vizuri

 • Mtoto atapatiwa ORS kwaajiri ya kunywa au kuongezewa maji kwenye mishipipa kama ana upungufu mkali wa maji. Maji huwa na madini sodium, potassium, chloride na kalisiamu kwa njia ya mshipa

 • Mtoto anatakiwa apate muda mwingi wa kupumzika

 • Mtoto atapata panadol kushusha homa

 • Mtoto atapatiwa madini Zinc ili kupunguza kuharisha na kuponya utumbo

 • Mtoto atapatiwa dawa za kuzuia kutapika kama anatapika sana


Kinga


Fanya yafuatayo ili uweze kuwakinga wengine endapo umepata maambukizi;


 • Pata chanjo ya kirusi Rota kwa wakati sahihi

 • Nawa mikono yako mara kwa mara baada ya kugusa sehemu yoyote hasa mara baada ya kuingia na kutoka chooni

 • Nawa mikono ya watoto mara kwa mara kwa maji safi na sabuni

 • Zingatia usafi kwa ujumla


Je kuna chanjo ya kirusi Rota?


Chanjo kwa ajiri ya kirusi Rota ipo. Kuna chanjo aina mbili ambazo ni Rotateq inatolewa kwa mtoto wa wiki 6 hadi 32 na Rotarix inatolewa kwa mtoto wa wiki 6 hadi 24.


ULY clinic inakushauri uwasiliane na daktari wako siku zote kabla ya kuchukua hatua yoyote inayohusu afya yako


Wasiliana na daktari wa ULY clinin kwa ushauri na Tiba kwa kupiga nambza za simu au kubonyeza "Pata Tiba"chini ya tovuti hii

Orodha kuu


Rejea za mada hii;

 1. Epidemiology and prevention of vaccine-preventable diseases: Rotavirus. Centers for Disease Control and Prevention. https://www.cdc.gov/vaccines/pubs/pinkbook/rota.html. Imechukuliwa 29.03.2020.

 2. Estimated rotavirus deaths for children under 5 years of age: 2013, 215 000. World Health Organization.https://www.who.int/immunization/monitoring_surveillance/burden/estimates/rotavirus/en/. Imechukuliwa 29.03.2020 3.

 3. Subhash Chandra parija. Textbook of Microbiology and immunology toleo la 2 ISBN: 978-81-312-2810-4. p 526-527.pdf

Imeboreshwa;

27 Septemba 2021 12:18:38

bottom of page