top of page

Kisukari na Chakula 

Kisukari na Chakula

Imeandikwa na daktari wa ulyclinic

Kisukari husababishwa endapo mwili unashindwa kutumia na kuhifadhi sukari kama ilivyo kawaida. Chanzo cha nguvu mwilini hutokana na sukari aina ya glukosi. Glukosi hupatikana kwenye matunda, baadhi ya mboga za majani, wanga na sukari yenyewe. Ili kudhibiti na kuweka sawa sukari yako mwilini ni lazima ule chakula chenye afya, fanya mazoezi na utahitaji kutumia dawa wakati mwingine au homoni ya insulin.

Kwenye chati  hapo chini utakutana na vidokezo vya kukusaidia kupanga chakula chako.

Vidokezo vya kula chakula chenye afya dhidi ya kutibu au kuzuia kupata kisukari

 • Kunywa glasi 1 ya maziwa na tunda ili kukamilisha mlo wako

 • Pombe huweza kudhuru kiwago cha sukari na kukusababishia kuongezeka uzito. Ongea na mtaalamu wako endapo unaweza kuongeza pombe katika mlo wako na kwa kiasi gani.

 • Kula mboga za majani kwa wingi, huwa na virutubisho vingi na nguvu kidogo

 • Chagua vyakula vya wanga Kama mkate usio wa kukobolewa, unga wa nafaka isiyokobolewa, mchele, viazi kwenye kila mlo. Vyakula vya wanga huvunjwa na kutengeneza glukosi mwilini ambayo huhitajika kwa ajili ya kuupa nguvu mwili wako.

 • Tumia samaki, nyama isiyo na mafuta, mayai au protini za kutokana na mimea mfano maharagwe, mbaazi kunde kama sehemu yam lo wako

 • Inashauriwa kila mtu mwenye kisukari apate ushauri kutoka kwa mtaalamu wa kisukari au mshauri wa kisukari.

 • Matibabu mazuri ya kisukari huhusisha kula chakula chenye afya, na kujishughulisha au kufanya mazoezi.

 • Hakikisha umekula chakula ch asubuhi ili kuanza siku vizuri.

 

Njia nyingine unayoweza kutumia ili kukadilia kiwango cha chakula unachotakiwa kula ni njia ya mikono yako

 1. Tumia matunda/mbegu na wanga kwa kiwango kinachofanana na ukubwa wa ngumi ya mkono wako mmoja

 2. Tumia mboga za majani nyingi iwezekanavyo kujaa katika mikono yako miwili

 3. Tumia nyama na mbadala wa nyama kiwango cha kujaa kiganja chako kimoja

 4. Tumia mafuta kiwango cha pingili ya juu ya kidole gumba chako

 5. Kuhusu maziwa na mbadala wa maziwa tumia mililita 250 ya maziwa yenye mafuta kidogo kwenye mlo wako mkuu. Kiwango hiki kinafanana na kile cha chupa ndogo ya soda kama cocacola.

 

 

Wasiliana na daktari wako siku zote kwa ushauri na tiba kabla ya kuchukua hatu yoyote

Pata ushauri na tiba kutoka kwa daktari wa ULY clinic kwa kubonyeza hapa au piga namba za simu chini ya tovuti hii.

Imeboreshwa 12.03.2020

Rejea

bottom of page